Koigi Wamwere

Born

18th December 1949

Email

kwamwere@gmail.com

Telephone

0722905663

All parliamentary appearances

Entries 101 to 110 of 186.

  • 6 Dec 2006 in National Assembly: Bw. Spika, shukrani kwa kunipa nafasi na mimi nichangie angaa kwa kidogo tu Ripoti hii ya Kamati ya Bunge inayosimamia matumizi ya pesa za Serikali. December 6, 2006 PARLIAMEANTARY DEBATES 4265 Bw. Spika, sitaki kurudia yale ambayo nilisema jana isipokuwa kusisitiza kwamba haifai yale mambo ambayo huwa yamemulikwa katika ripoti zilizopita yanaendelea kumulikwa katika Ripoti hii mpya. Hiyo ni ishara ya kwamba matatizo huwa hayatatuliwi bali yanaendelea kuweko pamoja na kazi yote ile ambayo Bunge huwa inafanya katika juhudi za kumalizia nchi yetu matatizo ya ufisadi. Bw. Spika, niongezee ya kwamba wakati tulikuwa tunazunguka nchi hasa tukikagua miradi ya barabara, ... view
  • 5 Dec 2006 in National Assembly: Bw. Spika, si Bw. Nderitu, lakini ni mimi! view
  • 5 Dec 2006 in National Assembly: Bw. Spika, ninashukuru kwa kunipa fursa hii ili--- view
  • 5 Dec 2006 in National Assembly: Bw. Spika, kofia hii inafanana na koti langu. Kwa maoni yangu, mimi ni sawa kabisa! view
  • 5 Dec 2006 in National Assembly: Bw. Spika, nilikuwa nakutolea shukrani zangu kwa kunipa fursa hii ili nitoe mchango wangu juu ya Ripoti ya Kamati inayosimamia matumizi ya pesa za Serikali. Bw. Spika, uchunguzi dhidi ya ufisadi ni muhimu sana. Hakuna nchi ambayo inaweza kuendelea ikiwa ina tatizo la ufisadi. Ni lazima tukubali ya kwamba ufisadi ni tatizo kubwa katika nchi yetu. Shirika la Transparency International, katika ripoti yake kila mwaka huonyesha ya kwamba ufisadi unaendelea kukithiri hapa nchini. Ripoti hiyo inaungwa mkono na Ripoti hii ya Kamati ya Bunge. Hatuwezi, kwa upande mmoja, kusema tunataka kupiga vita umaskini ikiwa kwa upande wa pili tunaruhusu ufisadi ... view
  • 5 Dec 2006 in National Assembly: Hiyo ni kweli kabisa, Bw. Spika. Lakini jambo ninalosema ni kwamba, haya tukubali ya kwamba Kamati hii haiwezi kuongea juu ya wizi au ufisadi wa moja kwa moja kwa sababu haujathibitishwa mahakamani. Basi ni muhimu baada ya kuonekana mtu amejikopesha pesa asukumwe mbele ili kuonekane kama kulikuwa wizi au la. Lakini ikibaki tu kwa ripoti kwamba mtu alijikopesha pesa, itabaki hivyo hivyo bila kufuatiliwa. Utakuta ya kwamba mabilioni ya pesa ambazo zinaongewa juu yake katika hizi ripoti, hakuna mtu ambaye anafuatilia. Bw. Sika, kwa hivyo, kuna haja kubwa ya tume inayochunguza ufisadi, KACC, ichukue December 5, 2006 PARLIAMENTARY DEBATES 4139 ... view
  • 5 Dec 2006 in National Assembly: Kwa hivyo, ni muhimu shirika la Transparency International lituambie uchunguzi wao ulifika wapi. Ni Bw. Mwalimu Mati ambaye alikuwa na makosa au ni mkurugenzi mwenzake, Mungai? Ni nani alikuwa amefanya ufisadi? Tunangojea na hatutaki jambo hili lisahaulike. Wengine ambao wako na jukumu la kujimulika ni watu wa habari. Wanahabari ni watu ambao wako na jukumu kubwa la kumulika ufisadi. Na mara nyingi nimejiuliza kwamba wanapomulika ufisadi wa mhe. Wamwere au mhe. Maj. Madoka, nani huwa anamulika ufisadi wao? Kukifanyika ufisadi kule kwao, hawawezi kutangaza. Ni lazima namna ya kumulika kila mtu itafutwe. Hatuwezi kuwa na wanahabari ambao ni kama wako ... view
  • 5 Dec 2006 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, tuseme kwamba yaliyopita si ndwele. Lakini, tunafaidika kwa sababu--- view
  • 5 Dec 2006 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, kusema kweli ningetaka sana kuleta hiyo faili. view
  • 5 Dec 2006 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, najua haiko lakini ninalinganisha matukio. Ninasema kwamba--- view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus