All parliamentary appearances
Entries 81 to 90 of 186.
-
22 May 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, ni ajabu ya kwamba mheshimiwa anayedai ninafanya upinzani nikiwa Serikalini, yeye alipokuwa Serikalini alikuwa mpinzani mkubwa kuliko mimi.
view
-
22 May 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, lakini jambo muhimu ni kwamba Serikali dhabiti haiogopi kukosolewa. Ninaiunga mkono Serikali hii kwa sababu ya uhuru wa kusema. Ninaweza kuikosoa bila ya kutimuliwa. Kama ingekuwa tofauti, mheshimiwa Mbunge angesema ya kwamba hii ni Serikali ya kidikteta. Tunajua ya kwamba kuna wanaokalia viti vya mbele ambao wana maoni tofauti, lakini hawawezi kuyaeleza kwa sababu wanaogopa kutimuliwa. Sasa hakuna uoga huo. Hili ni jambo la kusifiwa wala si la kukosolewa. Kwa hivyo, ninachosema ni kwamba---
view
-
22 May 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, sijakuwa fisi na sitakuwa fisi milele. Mimi hulka yangu ni ya kondoo na ndio sababu nimejiunga na Chama Cha Mwananchi (CCM) ili kutetea kondoo wengine. Hata Serikali inaweza kuwa ya kondoo nikimaanisha ya kwamba jukumu lake kubwa litakuwa ni kutetea kondoo wasije wakaliwa na fisi. Bw. Naibu Spika, nilichokuwa nasema ni kwamba Wizara hii imekuwa katika usingizi. Ni sawa Waziri kusema sababu yake hawakuwa na sheria ambayo ingewawezesha kuwalinda na kuwatetea wafanyikazi. Sasa tuna sheria hiyo. Vile tumempa sheria na uwezo---
view
-
22 May 2007 in National Assembly:
Haya, Bw. Naibu Spika. Lakini tunaelekea kule. Tutakapompa sheria hiyo basi aamke pamoja na maofisa wake. Anasema ukosefu wa sheria ulifanya walale kazini. Tukipitisha Mswada huu sioni sababu ya wao kuendelea kulala. Ni lazima waamke na kuwatetea wafanyakazi. Hakuna Wizara muhimu kuliko hii katika maisha ya wafanyakazi. Ninakumbuka vizuri Wizara hii ilikuwa maarufu sana ilipokuwa ikisimamiwa na marehemu Tom Mboya. Umuhimu wake umekuwa ukididimia. Ni lazima Waziri awatetea wafanyakazi, hasa wale wanyonge. Kwa sababu yeye ndiye mwenye uwezo, ni lazima afanye kazi zaidi.
view
-
22 May 2007 in National Assembly:
Asante sana, Bw. Naibu Spika. Ninashangaa kwa nini mheshimiwa anaogopa Mswada huu. Tuko hapa kuongea na hiyo ndio kazi yetu. Dunia nzima inalia ya kwamba tunalipwa mishahara mikubwa sana halafu tena tuogope kuongea? Tutashitakiwa kwa ufisadi. Tunakuja hapa tunakula pesa na 1512 PARLIAMENTARY DEBATES May 22, 2007 wakati wa kuongea, hatupatikani. Bw. Naibu Spika, sitaongea zaidi. Kuna makampuni ambayo yamekuwa na sifa mbaya kwa muda mrefu sana. Hii ni sifa ya kutojali afya na usalama wa wafanyakazi wao. Mfano ni kampuni ya Eveready. Nakumbuka zamani sana kama miaka 20 iliyopita nilipokuwa mhe. Mbunge hapa, nilikuwa nalia juu ya wafanyakazi wanaolazimika ...
view
-
17 Apr 2007 in National Assembly:
Ahsante, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili niuchangie machache mjadala huu juu ya Ripoti ya PAC. Ninataka kuongeza sauti yangu kwa sauti za wenzangu waliosema kwamba tatizo kubwa la Kamati za Bunge, ambazo hukagua matumizi ya pesa za umma, ni kwamba, hatimaye, mapendekezo ya Ripoti za Kamati hizo hayatekelezwi. Hatimaye, inakuwa Kamati hizo zimefanya kazi ya bure, ambayo ukiitizama vizuri utaona kwamba inaweza pia kutajwa kama ufisadi. Ninasema hivyo kwa sababu sielewi ni kwa nini Bunge, ambalo linauwezo mkubwa, haliwezi kutumia uwezo huo kuhakikisha kwamba mapendekezo ya Ripoti za Kamati zake yanatekelezwa. Bw. Naibu Spika wa ...
view
-
17 Apr 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, ningependa kugusia swala la wapiga firimbi. Hao ni watu ambao wanatusaidia. Wanatuambia ufisadi uko wapi. Wanaiambia Serikali ufisadi huko wapi. Wanasema: "Ewe Serikali, tumesikia umetangaza vita dhidi ya ufisadi! Ufisadi uko hapa! Kuja!" Lakini ubaya ni kwamba, wanapotuambia palipo ufisadi, na ufisadi unatoa macho ya vita na kuelekea kuwapiga, sisi wenyewe hatusimami nao! Bw. Naibu Spika wa Muda, tunamkumbuka Munyakei! Ni shujaa ambaye anastahili kutuzwa na Serikali na Rais, hata kama atatuzwa baada ya kifo chake. Yeye ni mmoja wa wale waliofutwa kazi, akaishi katika taabu na hatimaye, akafa na kuiacha familia yake katika taabu ...
view
-
17 Apr 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, baada ya kupata pesa, sasa ni kutafuta namna ya kumhonga Mungu. Sijui kama Mungu anahongeka!
view
-
17 Apr 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, nilikuwa naongea juu ya wapiga firimbi. Ninachosema ni kwamba kulikuwa na wapiga firimbi 11---
view
-
17 Apr 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, nakupongeza kwa sababu una moyo thabiti wa kupigana na ufisadi.
view