All parliamentary appearances
Entries 91 to 100 of 186.
-
17 Apr 2007 in National Assembly:
Na ni lazima nikushukuru kwa jambo hilo. Kama tungekuwa na Maspika kadhaa kama wewe---
view
-
17 Apr 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, nilikuwa naongea juu ya wapiga firimbi. Nilikuwa nasema kwamba kuna wapiga firimbi 11 ambao walikuwa wameajiriwa kazi katika Hoteli ya Grand Regency ambao hatimaye ilijulikana kwamba walifutwa kazi kimakosa. Walitakikana kurudishwa kazini lakini mpaka sasa wafanyakazi hawa 11 hawajarudishwa kazini, ingawa tumepitisha sheria ambao inaruhusu Serikali kuwapa ulinzi na kuhakikisha ya kwamba wamerudi kazini kama ilivyo haki yao. Utatokwa na machozi ukifahamu ya kwamba wafanyakazi hao wamemwandikia mhe. Michuki barua wakimtaka awape ulinzi ili waweze kurudi kazini. Walipokuwa wakiandika hiyo barua, walisema ya kwamba watoto wao walikuwa wametoka shuleni kitambo kwa sababu hawana pesa za ...
view
-
17 Apr 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, nasikitika, lakini naomba kuunga mkono.
view
-
22 Mar 2007 in National Assembly:
Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii na mimi nichangie Hotuba ya Rais. Ningetaka kuisifu Serikali sana kwa kazi nzuri ambayo imefanya. Lakini pia, ni vizuri kukumbuka kwamba mgema ukimsifu, ni rahisi sana kuitia tembo maji. Kwa hivyo, ningetaka kusema machache kuhusu yale ambayo kama tutayafanya, yataweza kutusaidia zaidi. Bw. Spika, furaha kubwa ya Serikali inaonekana ni kwamba uchumi umefufuka na unaendelea kukua kwa asilimia 6 kwa mwaka. Ningetaka tu kuikumbusha Serikali ya kwamba kuvua numbi si kazi; kazi ni magawiyoni! Ni lazima kilichokuwa kikuliwe na wote. Ningetaka kuongeza ya kwamba uchumi ambao utamsaidia mtu mmoja kuchuma Kshs2 billioni ...
view
-
22 Mar 2007 in National Assembly:
Bw. Spika, lingine ambalo labda mheshimiwa hana habari nalo, wilaya kama ya Nakuru haipewi nyadhifa kama zile za District Commissioner (DC), Provincial Commissioner (PC), Permanent Secretary (PS), balozi na hata wakurugenzi wa makampuni makubwa. Mpaka wa leo, sijaelewa ni kwa nini jambo hili halifanyiki. Nimelifanyia utafiti; najua ninachoongea na ninajua ya kwamba ninasema ukweli mtupu. Tunataka jambo hili lirekebishwe. Wengine watasema ya kwamba tunanyimwa kwa sababu kura zetu zinasemekana ziko mifukoni na kwa hivyo hakuna haja ya kubembelezwa. Lakini sioni kwa nini kama kura zetu ziko mifukoni mwao, wasitushukuru kwa kutupa kazi zile ambazo wanapea wale ambao wanataka kuwashawishi wawape ...
view
-
22 Mar 2007 in National Assembly:
Udikteta huu unapuliziwa hewa na vyama vya kikabila. Hata sisi ambao tunapinga ukabila tunaitwa wasaliti na watu wanakuja kutuchomea kwetu. Mhe. Mbunge mzima aliongoza jeshi la kuja kutuchoma eti kwa sababu tumejiunga na chama kingine. Watu ambao wanaamini kwamba wataelekeza nchi hii kwingineko tofauti na kule tulikoelekezwa na KANU - naongea kuhusu wafuasi wa chama cha NARC(K) - lazima wakifanye kile kilichofanywa na Serikali ya KANU wakati wa enzi ya giza. Ni jambo la kushangaza kwamba kila siku tunashinda tukihubiri kuhusu majimbo. Majimbo hayo ndiyo yatamaliza nchi hii na lazima ieleweke hivyo.
view
-
22 Mar 2007 in National Assembly:
Hata kuna wagombea viti vya Bunge ambao wanakataza watu kuingia katika maeneo yao ya uwakilishi Bungeni---
view
-
22 Mar 2007 in National Assembly:
Bw. Spika, ningependa kusema kuwa ni bahati kubwa kwamba ninaongea leo hii hapa Bungeni. Hii ni kwa sababu waliokuja kuchoma sanamu yangu wangepata nafasi wangenichoma miye. Mara nyingi mimi husema bahati yangu ni kwamba nilifufuliwa na Yesu alipokuwa akifufuka.
view
-
22 Mar 2007 in National Assembly:
Bw. Spika, jambo jingine linalonishangaza ni kwamba wale wanaogombea Urais, badala ya kutafutia nchi hii Rais Mkenya, wanazunguka nchi hii wakisema eti wanataka nchi hii iwe na Rais Mkikuyu, Mjaluo, Mkamba, Mnandi, na kadhalika. Ikiwa nchi hii itakuwa na---
view
-
22 Mar 2007 in National Assembly:
Bw. Spika, kwa hayo machache, naomba kuunga mkono.
view