23 Oct 2019 in Senate:
Nikirudi kwa Arifa iliyoletwa na Seneta wa Makueni, ningependa kuiunga mkono kwa jambo moja. Kwanza, ningependa kukemea uamuzi wa Serikali wa kuvunja Bodi ya usimamizi ya Kenya Ferry Services. Wameondoa wale waakilishi ambao ni raia, ambao ni members of the public, yaani wananchi wa kawaida, lakini wakaacha wale watumishi wa Serikali ambao wanakaa katika Bodi ile. Kwa mfano, kuna Katibu Mkuu ama Katibu wa Kudumu katika Wizara ya Fedha ambaye anakaa katika Bodi ya Kenya Ferry Services. Kuna Katibu wa Kudumu katika Wizara ya Usafiri na Uchukuzi ambaye pia anakaa katika Bodi ile na kuna mwakilishi kutoka Shirika la Kenya ...
view
23 Oct 2019 in Senate:
Bw. Naibu Spika, Serikali inapaswa iteuwe Tume maalum ya kuchunguza mkasa kama ule ama kuwe na tume ya kudumu ambayo itakuwa inachunguza mikasa kama hii ambayo inatokea katika nchi yetu. Kwa kumalizia ni kwamba mimi mwenyewe binafsi nilizuru Shirika la Kenya
view
23 Oct 2019 in Senate:
wakati mkasa ulipotokea na vile vile wakati miili za marehemu zilikuwa zinatolewa, nilikuwa pale na nikashuhudia zoezi lile likiendelea. Kazi ambayo ilifanyika pale ilikuwa kazi ngumu sana kwa wanamaji wetu. Pia, tungependa kuchukua fursa hii kuwapongeza wanamaji wetu kwa kazi yao nzuri waliofanya. Ukiangalia katika kile kivuko cha ferry, ni kama Thika Highway kwa sababu meli zote kubwa zinaingia pale, zinazoleta makasha na kutoa mizigo katika Bandari ya The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
23 Oct 2019 in Senate:
Mombasa. Hii ni kama kuweka pikipiki katika Thika Super Highway ambapo unaona pikipiki zinaruka wakati magari makubwa yanapita na kurudi. Kwa hivyo, katika kivuko cha feri, mpaka sasa kuna hatari kubwa ya wananchi kupata hasara kwa sababu pale katika kivuko, meli kubwa ambazo zinaingia kuleta mizigo katika Bandari ya Mombasa zinatumia sehemu ile na hakuna njia yoyote ambayo mpaka sasa Serikali imefanya kudhibiti ajali ambazo zinatokea katika sehemu ile. Bw. Naibu Spika, nilitangulia kusema wakati nilipotoa taarifa tarehe moja mwezi huu kwamba uwekezaji wa Serikali katika Shirika la Feri umekuwa duni sana. Katika bajeti ya Kshs1.2 billion, Serikali inatoa Kshs400 ...
view
22 Oct 2019 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, the Chairperson of the County Public Accounts and Investment Commitee (CPAIC) is 10 minutes away from the Chamber. Could we deferr that Order and then we revisit it in the next half an hour? I will be obliged.
view
22 Oct 2019 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii ili kuchangia Hoja ya Sen. Nyamunga kuhusiana na wafanyikazi wanaohudumia jamii kwa mambo ya kiafya. Bw. Spika, wengi wetu waliozaliwa katika miaka ya sitini walipitia mikononi mwa wakunga, ambao ndio waliokua wafanyakazi wa kwanza wa jamii waliokuwa wakisaidia katika masuala ya afya. Hadi sasa, wakunga hawa bado wako katika jamii ambazo ziko mbali na mahospitali. Wakunga hawa wanasaidia pakubwa kuzalisha bibi, dada na mama zetu, ili wapate watoto. Njia wanayotumia sio salama, lakini ndio njia pekee wanayoweza kusaidia ili kuhakikisha kwamba wameweza kupata watoto. Bw. Spika, baada ya janga la UKIMWI kutuingilia, wafanyikazi ...
view
22 Oct 2019 in Senate:
hawana vifaa vya kujikinga na magonjwa ambayo wanayohudumia kwa Wakenya wengine. Bw. Spika, Hoja hii imekuja wakati mwafaka kwa sababu tumeona kwamba katika kaunti nyingi, wafanyakazi wa afya wa jamii hawana malipo. Serikali za kaunti hazijakuwa na rasilimali za kutosha za kuhakisha kwamba wameajiri kazi wafanyakazi ambao watahudumia wananchi katika kila zahanati ama hospitali. Katika kaunti nyingi, wengi wa ngariba ambao wanapasha vijana tohara ni wafanyakazi wa afya wa jamii lakini hawashughulikiwi kwa njia yoyote na serikali hizo. Bw. Spika, tumeona kwamba ziko baadhi ya kaunti ambazo zimeweza kuwajali wafanyakazi kama hawa. Wanawakatia kadi za NHIF ili wakiwa na matatizo ...
view
22 Oct 2019 in Senate:
On a point of information, Mr. Speaker, Sir.
view
22 Oct 2019 in Senate:
Bw. Spika, neno “mkunga” ni midwife kwa Kiingereza. Kwa hivyo si neno langu mimi bali ni neno la Kiswahili. Ijapokua mimi ni Mswahili, hilo ni neno linalotumika kuanzia, Sofala, Msumbiji, Kisimayu na hata Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
view
17 Oct 2019 in Senate:
Thank you, Mr. Deputy Speaker, Sir, for giving me this opportunity to make my comments on the ruling that you have just made. First and foremost, you made a ruling on Tuesday on a Motion to appoint a select Committee to consider the impeachment of Gov. Samboja, the Governor of Taita Taveta County. During the hearing of that Motion, there were objections on the fact that there was a court order which had been issued by the court. As a result, you made a ruling that the Houses of Parliament are not bound by court orders issued to injunct their ...
view