Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1631 to 1640 of 1994.

  • 17 Oct 2019 in Senate: Mr. Deputy Speaker, Sir, you alluded to Standing Order No. 1 (2) which states that--- view
  • 17 Oct 2019 in Senate: Mr. Deputy Speaker, Sir, I want to make those observations. Standing Order No.1(2) provides that:- “The decisions made in paragraph (1) shall be based on the Constitution of Kenya, statute law and the usages, forms, precedents, customs, procedures and traditions of the Parliament of Kenya and other jurisdictions to the extent that these are applicable to Kenya” view
  • 17 Oct 2019 in Senate: So, Mr. Deputy Speaker, Sir, in making the decision that you have made, I believe, with profound respect, that it is not in consonance with Standing Order No. 1(2). This is because it does not accord with the Constitution, statute law and precedents. view
  • 17 Oct 2019 in Senate: You alluded to the decision of the Supreme Court in Gov. Wambora’s case which provides that Houses of Parliament cannot be injuncted in the discharge of their duties. Secondly, if you look at the court process at the moment, we can cite our own case which has been lying in the High Court for the last three months. Proceedings have now taken place and we are going there for mentions to constitute a bench that will hear the case. So far, more than three months have passed and we have not had any tangible order that has been made. So, ... view
  • 16 Oct 2019 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Hoja ya kumpongeza Eliud Kipchoge, Brigid Kosgei pamoja na wanariadha wengine ambao waliipa Kenya sifa kubwa kule Doha. Bw. Naibu Spika, kabla ya kutoa mchango wangu, mnamo siku ya Ijumaa jioni, wanajeshi wetu wa Jeshi la Wanamaji waliweza kufaulu kupata miili miwili ya Mariam Kighenda na bintiye Amanda ambao walikuwa wamezama mnamo tarehe 29 Oktoba, 2019. Lilikuwa ni jambo ambalo liliwatamausha sana Wakenya wengi. Hata hapa Bungeni tulipolizungumzia, wengi wetu walitamaushwa na hali ilivyokuwa inaendelea. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version ... view
  • 16 Oct 2019 in Senate: Kwa hivyo, kupatikana kwa miili hiyo kulitoa afueni kubwa kwa Wakenya wote. Juhudi za wanajeshi zilizaa matunda wakati miili hiyo miwili ilipopatikana. view
  • 16 Oct 2019 in Senate: Siku ya Jumamosi ilianza vizuri. Sisi Waisilamu siku zetu zinaanza jioni, yaani baada ya Sala ya Magharibi ndipo tunaanza siku ya pili. Kwa mfano, leo ikifika magharibi, kesho itakuwa tumeanza siku ya Alhamisi. Tulichanganya ushindi wa Eliud Kipchoge pamoja na Brigid, ikawa yote ni siku ya Jumamosi. Kwa hivyo, siku ya Jumamosi kwetu ilikuwa nzuri sana. view
  • 16 Oct 2019 in Senate: Kama nchi tuliweza sote kuacha kazi zetu na tukakaa kuangalia Mkenya huyu ambaye alikuwa Vienna akiipa nchi hii umaarufu mkubwa kwa kazi aliyoifanya kwa juhudi zake peke yake. Tumeona kwamba Wakenya wengi ambao wanashiriki katika mbio tofautitofauti ulimwenguni, iwe ni Chicago, Berlin au mahali popote, huwa na uzalendo mkubwa. Wakati wanapeperusha na kujifunikia bendera ya nchi ya Kenya, sisi huona fahari ya nchi yetu. Lakini jambo hilo linaishia pale pale. Hata Wizara yetu ya Utalii haijaweza kuchukua rasilimali kama hii kuhakikisha kwamba Kenya inapata umaarufu na watalii wengi wanakuja kuangalia vitu vingi vya kitalii hapa nchini. view
  • 16 Oct 2019 in Senate: Ni heri tutumie fursa hii kuuza na kutangaza Kenya kama nchi ambayo ina amani na talanta tofautitofauti za kimichezo. Wengi huwa tunajulikana kwa mambo ambayo hatufai kuyataja kama vile ufisadi na mengine maovu ambayo hayafai katika jamii. view
  • 16 Oct 2019 in Senate: Bw. Eliud Kipchoge kama Mkenya ameweza kuushinda ulimwengu na kutoa fursa kwa watu wengine ili wapate fursa ya kufikiria vile wanaweza kupunguza muda ambao unaweza kutumika kukimbia mbio za marathoni. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus