Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1641 to 1650 of 2123.

  • 10 Mar 2020 in Senate: Katika muda mfupi ambao amehudumu kama Mbunge wa Msambweni, alifanya kazi kubwa sana katika nyanja ya elimu. Aliweza kusaidia kupitia kwa National The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 10 Mar 2020 in Senate: Government Constituency Development Fund (NG-CDF) kuanzisha Dori Girls’ Secondary School ambayo iko karibu nyumbani kwake na mahali alipozikwa jana. view
  • 10 Mar 2020 in Senate: Bw. Spika, mambo mengine ambayo ameweza kufanya ni kupigania haki za watu wa Pwani na Wakenya kwa jumla. Alikuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kwamba watu wake wa Msambweni wamepata mashamba na makazi yao kutokana na dhuluma za kihistoria. view
  • 10 Mar 2020 in Senate: Kama Mwenyekiti wa Muungano wa Coast Parliamentary Group, aliweza kutuweka pamoja sisi kama Wabunge kutoka sehemu ya Pwani. Alichangia pakubwa katika kuhakikisha kwamba jumuia za Kaunti za Pwani zimeweza kuimarika na kusaidia wananchi wa eneo lile. view
  • 10 Mar 2020 in Senate: Wiki iliyopita tulikutana na Mhe. Dori hapa katika Bunge. Vile vile, tulikuwa pamoja katika Health Club mpaka siku ya Alhamisi ya Tarehe 22.02.2020. Wiki iliyopita niliwahi kuongea naye siku ya Jumatano wakati tulikuwa tumepanga mkutano wa kupeleka mapendekezo yetu kwa kamati tekelezi ya Building Bridges Initiative (BBI). Alinipigia simu siku hiyo akaniambia kwamba hangeweza kufika Bungeni kwa hivyo, tupange kufanya mkutano wiki iliyofuata. view
  • 10 Mar 2020 in Senate: Siku ya Jumamosi asubuhi nilipata ripoti kwamba alilkuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika Agha Khan Hospital, Mombasa. Niliwahi kuenda hapo hospitalini lakini kwa bahati mbaya sikuweza kumwona kwa sababu hali yake ilikuwa mbaya kidogo. Vile vile, kutokana na maradhi aliyokuwa nayo madaktari walikuwa wameshauri kwamba asiweze kuonekana. Jana asubuhi tulipata habari za kuondoka kwake katika ulimwengu. Twaomba Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema. view
  • 10 Mar 2020 in Senate: Kifo kinaweza kupata mtu yeyote mahali popote. Kwa hakika, kifo cha ndugu yetu ni funzo kwetu sisi kwa sababu katika ulimwengu tumepewa fursa ya kusaidia binadamu wenzetu na kuhakikisha kwamba tunaacha alama kwa yale tumefanya. Mwenzetu ameweza kufanya mengi katika nyanja za elimu katika eneo lake la Msambweni na kuipatia jamii yake ardhi. view
  • 10 Mar 2020 in Senate: Mwenyezi Mungu ampeleke katika safari hii yake ya mwisho hapa ulimwenguni na tuhakikishe kwamba sisi ambao tunabaki nyuma tunayaangalia yale ambayo amefanya na kufanya bora zaidi. view
  • 10 Mar 2020 in Senate: Jambo la kusikitisha ni kwamba, Mhe. Dori aliacha familia changa sana. Watoto wake wote ninafikiri hawazidi miaka 15. Kwa hivyo, ni jambo la kusikitisha lakini analofanya Mwenyezi Mungu ndilo tunalokubali. Sisi kama binadamu hatuna la kufanya zaidi isipokuwa kumwombea Mwenyezi Mungu katika safari yake. view
  • 10 Mar 2020 in Senate: On a point of order, Mr. Speaker, Sir. I am disappointed by my neighbour here, Sen. Wambua. This is because whenever I go to the gym and he sees me there, it is because I will have already done my workouts at Nyayo National Stadium, where we go to play football every Tuesday, Wednesday and Thursday morning. He should withdraw the remark that I go to the gym to read newspapers. In fact, my record in Bondo the other day is very clear. Recently, I scored a beautiful goal at Nyayo National Stadium, and my record is there. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus