3 Oct 2019 in Senate:
Bw. Spika, World Bank kwa Kiswahili ni Benki ya Dunia sio benki kuu ya dunia. Hakuna benki ya kimataifa ambayo inajulikana kama World Bank.
view
3 Oct 2019 in Senate:
I have already contributed, Madam Temporary Speaker. Ningependa kumsaidia Sen. Kinyua ambaye pia ni mwanafunzi wa lugha ya Kiswahili na Sen. Sakaja kwa sababu sisi ndio Maseneta wa majiji. Tuko watatu tu hape kwa sababu wengine wote ni Maseneta kutoka vijiji na gatuzi ndogo ndogo. Amepata asilimia 70 kwa 100.
view
2 Oct 2019 in Senate:
Asante Bw. Spika wa Muda kunipa fursa hii ili kuwasilisha Hoja ya kuairishwa kwa Bunge ili tuweze kujadili kuhusu ajali iliyotokea katika kivuko cha feri cha Likoni, Mombasa County, mnamo Jumapili, 29th September, 2019. Vile vile, tunafaa kujadili hali ya huduma katika kivuko cha feri cha Likoni. Bw. Spika wa Muda, nasimama hapa leo kwa masikitiko makubwa kuzungumzia swala la ajali hiyo ambayo ilitokea katika kituo cha feri cha Likoni. Mnamo 29th September, 2019, mwendo wa 6:10 p.m., Mariam Kigenda na binti yake Amanda Mutheu waliabiri feri kwa jina MV Harambee kuvuka kutoka upande wa Likoni kwenda mjini. Feri ilipofika ...
view
2 Oct 2019 in Senate:
usalama wa Bandari ya Mombasa pamoja na kivuko cha feri cha Likoni umo mikononi mwa Harbour Master ambaye ndiye mkuu wa usalama katika Bandari ya Mombasa. Ni jambo la kusikitisha kwamba, Bandari ya Mombasa haina vifaa vya kutosha vya kuweza kupambana na majanga kama hayo. Bw. Spika wa Muda, lawama inaelekezwa kwa shirika la Kenya Ferry Services (KFS), Wizara ya Usafiri na Miundomsingi, Shirika la KPA, Kenya Coast Guard Services ambayo ilizinduliwa juzi na vilevile Kenya Maritime Authority (KMA) . Shirika la KMA lina jukumu la kuhakikisha kwamba vyombo wanavyoabiri binadamu katika bahari za Kenya viko katika hali nzuri na ...
view
2 Oct 2019 in Senate:
Mwisho ni kwa Jeshi la Wanamaji, Kenya Ports Authority (KPA) na Kenya Maritime Authority (KMA); wana mipango gani kuhusiana na usalama katika kivuko cha Likoni na Bandari kwa jumla? Tangu juzi hadi sasa, gari lao na wale waathiriwa hawajapatikana. Wameweka mikakati gani kuhakikisha kwamba iwapo kutatokea tukio kama hili wakati mwingine, uwezekano wa kuokoa maisha na mali utakuwa mzuri zaidi kuliko ilivyofanyika juzi? Mtakumbuka ya kwamba, tushawahi kupoteza maisha ya watu takriban 200 katika kivuko cha Mtongwe ambacho kinahudumia watu wengi.
view
2 Oct 2019 in Senate:
Tangu Shirika la Huduma za Feri kuundwa, ijapokuwa limetajwa kwamba ni Shirika la Kitaifa, mpaka sasa hawajaweza kutoka nje ya Kaunti ya Mombasa kufanya huduma yoyote. Hatujaweza kununua feri ambazo zinaweza kuhudumu katika Ziwa Victoria, Ziwa Turkana na kwengineko ambako kuna usafiri wa majini. Ni swala ambalo Kaunti ya Mombasa inaweza kusimamia kikamilifu kwa sababu ruzuku inayotolewa na Serikali imepungua pakubwa. Kwa vile imepungua, inamaanisha kwamba huduma katika eneo hilo zitaathirika na wananchi watakosa huduma bora. Hatuombi iwe hivyo, lakini kukitokea dharura nyingine, itakuwa shida kwa wananchi kuweza kupata huduma bora ili kuokoa maisha.
view
2 Oct 2019 in Senate:
Nikimaliza, ninatuma rambirambi zangu binafsi kwa familia ya mwenda zake, Bi. Mariam Kigenda, pamoja na mtoto wake. Ninaomba Mwenyezi Mungu awape subira wakati wa msiba huu.
view
2 Oct 2019 in Senate:
Ninamualika Seneta wa Kaunti ya Bungoma, Sen. Wetangula aunge mkono Hoja hii.
view
2 Oct 2019 in Senate:
It is over 100,000 people daily.
view
19 Sep 2019 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa ya kuchangia taarifa ya Seneta wa Kaunti ya Makueni, Sen. Mutula Kilonzo Jnr..
view