19 Sep 2019 in Senate:
Kwanza nina wakaribisha wanafunzi katika kikao hiki cha mwisho cha Seneti hapa Kaunti ya Kitui kabla ya kurudi makao yake makuu jijini Nairobi. Ninawaomba watie bidii katika masomo kwa sababu bila masomo, hawatafika hapa.
view
19 Sep 2019 in Senate:
Pili, jana asubuhi tulizuru Gereza la Kitui tukiwa na Maseneta wa Kamati ya Haki, Sheria na Haki za Binadamu na Kamati ya Usalama wa Nchi, Ulinzi na Uhusiano wa Kimataifa. Tulipata kwamba Jela ya Kitui, kama jela zingine zote, lina tatizo la msongamano wa wafungwa. Jela ya Kitui yenye uwezo wa kubeba wafungwa 300, ilikuwa na wafungwa 673 jana asubuhi. Wengi wa wafungwa hao wameshtakiwa makosa madogo madogo ambayo faini yake labda haizidi Kshs5,000 ama Kshs10,000. Mwisho, wanabaki kukaa ndani wakipewa chakula na hawafanyi kazi yoyote.
view
19 Sep 2019 in Senate:
Bw. Spika, mahali wanapoka ni chumba chenye urefu wa futi 10 kwa 10 ambapo wafungwa zaidi 100 wanalala. Hili ni jambo linalo dunisha maisha ya binadamu. Hii ni kwa sababu binadamu zaidi ya 100 hawapaswi kulala ndani ya chumba chenye ukubwa wa futi 10 kwa 10. Sisi Maseneta tuliguzwa moyo na tukachanga takribani Kshs80,000 kulipa faini ya baadhi ya wafungwa hao ili warudi nyumbani. Wafungwa 15 waliachiliwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
19 Sep 2019 in Senate:
hapo hapo baada ya kulipa hiyo faini. Zile pesa kidogo za per diem ambazo tulipewa juzi zote zilibaki hapo.
view
19 Sep 2019 in Senate:
Lazima mahakama ziwe macho kwa sababu utapata unawekewa dhamana kwa makoso madogo ambayo familia yako haiwezi kupata. Wale mabwanyenye wanaoshtakiwa na makosa makubwa wanapewa bondi ndogo ambazo wanalipa kwa urahisi. Masikini wanao shitakiwa katika makama nyingi wanapewa bondi kubwa ili wakose kulipa na warudi gerezani.
view
19 Sep 2019 in Senate:
Jambo lingine ambalo tuliona ni kwamba pia mahakimu wana utepetevu mkubwa katika kuendesha kesi zao. Utapata zaidi ya kesi 100 katika gereza hili hazina tarehe za kusikizwa. Ikiwa huna tarehe ya kusikizwa, ina maana kwamba unakaa ndani lakini hujui ni lini utatoka. Iwapo umefungwa, unajua unatumikia kifungo cha miaka miwili kisha uende nyumbani. Kama unangojea kesi, hujui utatoka lini.
view
19 Sep 2019 in Senate:
Bw. Spika, kuna mambo ambayo lazima mahakama ifuatilie. Hatuwezi kuwa na Katiba mpya inayolinda haki za Wakenya ilihali wale wanaotakikana kulinda hizo haki wanazikanyaga na kuendelea kunyanyasa Wakenya wasio na hatia.
view
19 Sep 2019 in Senate:
Mwisho ni kwamba tume elezwa kipande cha ardhi cha jela hii ya Kitui kimenyakuliwa na mabwanyenye wa kibinafsi. Ukiwa ndani ya jela, utaona jengo lenye ghorofa tano linaloongalia ndani ya jela. Haipaswi kuwa hivi kwa sababu ya usalama wa jela hilo na pia wafungwa kwa sababu hilo jengo linazidi ghorofa nne na ukuta wa jela ni ghorofa. Kwa hivyo usalama wa wafungwa na wale waliomo katika jela hiyo umo hatarini kwa sababu hatujui ni nani atakayekuja katika jumba lile linaloangalia ndani ya jela.
view
19 Sep 2019 in Senate:
Kama Kamati ya Haki, Sheria na Haki za Binadamu, tutarudi kuangalia mambo haya kwa undani zaidi. Hata hivyo, maswala kama haya hasa mahakama na ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka lazima wawe proactive na kuhakikisha kwamba wananchi wanapata haki zao. Katiba imewalizimisha kulinda haki za wananchi. Kwa hivyo mwananchi yeyote hatakiwi kudhulimiwa kwa sababu yuko gerezani.
view
19 Sep 2019 in Senate:
Asante Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada wa County Tourism ambao umeletwa bungeni na Seneta maalum, Sen. (Dkt.) Zani.
view