19 Sep 2019 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, ninampongeza dada yangu, Sen. (Dkt.) Zani, kwa kuleta Mswada huu ambao umekuja katika wakati mwafaka. Utalii ndio ulikuwa msingi wa uchumi wa Kaunti za Pwani, kama vile, Lamu, Kilifi, Mombasa, Kwale na Taita-Taveta. Lakini, kwa miaka sasa, utalii umeshuka na watalii wengi ambao tunapata ni ndugu zetu kutoka sehemu za bara. Wao ndio wanasafiri Mombasa kama watalii wa ndani kwa ndani wakitumia Reli ya Standard Gauge Railway (SGR) au ndege.
view
19 Sep 2019 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, Mswada huu utakapopitishwa kuwa sheria, utasaidia pakubwa kuangazia uchumi wa utalii katika maeneo ya kaunti za Pwani. Ningependa kutoa masikitiko yangu kwamba Serikali Kuu haiweka mikakati yeyote ikishirikiana na serikali za kaunti kujaribu kufufua uchumi. Kwa mfano, ingekuwa bora kwa Serikali Kuu kupitia kwa Wizara ya Utalii, kuanzisha kongamano la kitaifa na kaunti zote 47 kuhusu mikakati ambayo wanapanga katika mambo ya utalii. Ilivyo kwa sasa, yale yanayofanywa na Serikali Kuu mashinani hayajulikani. Kwa hivyo, hakuna mwelekeo kamili unaotoka kwa Serikali Kuu kuhusiana na maswala ya utalii. Jambo la pili ambalo limeleta upungufu wa utalii ni ...
view
19 Sep 2019 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, hatujakuwa na ubunifu katika mambo ya utalii. Kwa mfano, hapa Kitui, tulielezwa kwamba kuna mlima ambao ukizunguka mara saba kama wewe ni mwanamme unageuka mwanamke na kama wewe ni mwanamke unageuka mwanamme. Mlima huo unaitwa Nzambani Rock. Lakini, hatukuona mapango yote barabarani kama vile, barabara kuu ya kuelekea Nairobi, Mombasa, Mwingi au Thika kuonyesha ya kwamba kuna mlima unaitwa Nzambani Hills ambao una historia ya mambo mazuri The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
19 Sep 2019 in Senate:
kama hayo. Kwa hivyo, ili kukuza uchumi wa kitalii lazima kaunti zetu ziwe na mbinu za kutafuta vitu vipya ambavyo vinaweza kusaidia katika mambo ya utalii.
view
19 Sep 2019 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, katika maeneo ya Pwani kama vile Lamu, kuna maswala ya ukosefu wa usalama na madawa ya kulevya ambayo yamechangia pakubwa kuua utalii. Wengi wa watalii wanataka kupata fursa wajumuike na wananchi wa kawaida na watembee barabarani jioni. Lakini, ikiwa hakuna usalama, watalii hawataweza kutembea. Kama kuna vijana wanaotumia madawa ya kulevya, watalii hawatapata fursa ya kutembea na kujionea vile wenyeji wanaishi.
view
19 Sep 2019 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, nimetangulia kusema kwamba miundo msingi ni duni katika nchi yetu ya Kenya. Barabara zinazoelekea katika maeneo ya utalii zinaoshwa na mvua na hazipitiki.
view
19 Sep 2019 in Senate:
Mafunzo ya utalii pia yamerudi chini katika nchi ya Kenya. Pwani kunajengwa chuo kikuu cha utalii katika maeneo ya Kilifi lakini mpaka sasa, miaka saba kutoka ujenzi uanze, hatujaona mwelekeo wote wa chuo hicho.
view
19 Sep 2019 in Senate:
Kifungu cha 14 kinatoa fursa kwa waziri mhusika wa maswala ya utalii katika kaunti kufanya kanuni kuhusiana ni vipi atakeleza sheria hii. Lakini, kwa sababu tuna kaunti 47, kwamba kila kaunti itakuwa na kanuni zake, tutakuwa na kanuni 47. Hiyo kwa hakika, itakuwa nikurudiarudia mambo yale ambayo yanafanyika katika kaunti zetu. Kwa hivyo, ningependekeza kwamba waziri mhusika wa utalii aweze kutengeneza kanuni hizo na azipeleke katika kaunti nyingine na zipitishwe kama sheria.
view
19 Sep 2019 in Senate:
Kifungu cha 15 kinasema kuwa serikali za kaunti kupitia bunge za kaunti zitunge sheria kama hii ili ziweze kutumika katika kaunti zile. Hiyo pia itakuwa kurudia mambo yale yale. Ingekuwa bora kwamba iweze kuchukuliwa na serikali za kaunti na iwe sheria ambayo itatoa mwongozo kwa maswala ya utalii katika kauti zetu.
view
19 Sep 2019 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, utalii katika maeneo ya Mombasa unaweza kuchangia pakubwa katika kujenga uchumi. Lakini, kama nilivyotangulia kusema, hakuna uwekezajia katika swala hili. Kwa mfano, ukienda katika hoteli ya English Point Marina, iko karibu sana na ufuo wa O ld Port ambao unahesabika kama mita 200 kutoka upande moja hadi mwingine. Lakini, hakuna mashua za kuchukua watalii kutoka sehemu moja hadi upande wa mjini ili watembee katika mji wa zamani wa O ld Port na baadaye wapande mashua na kuelekea upande wa pili na kurahisisha maswala ya usafiri. Pia, ukipanda ferry inachukua zaidi ya saa moja kutoka Nyali hadi ...
view