Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1681 to 1690 of 1994.

  • 18 Sep 2019 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja ya kuundwa kwa kamati maalum ili kuchunguza mambo yanayohusu vifaa vya afya vinavyopelekwa katika kaunti. Kwanza, wazo la kuunda kamati ni nzuri sana kwa sababu kwa muda wa zaidi ya mwaka sasa, Bunge limekuwa likilalamika kuhusu mradi wa vifaa vya hospitali lakini hatujapata jibu lolote. view
  • 18 Sep 2019 in Senate: Bw. Naibu Spika, naomba unilinde kwa kuwa baadhi ya wenzangu wamesimama na wanapiga kelele. view
  • 18 Sep 2019 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika. Ijapokuwa wazo lenyewe ni nzuri, utekelezaji wake umekumbwa na utata kwa sababu Kamati ya Afya imekuwa ikizembea katika utendajikazi wake. Bw. Naibu Spika, wale watu waliochaguliwa kuwa wanakamati wa kamati hii maalum wengi wao wanatoka katika Kamati ambayo iko. Mwaka jana, tulipokutana na Waziri tarehe ishirini na saba mwezi wa kumi moja mwaka wa elfu mbili kumi na nane, maswala haya yalikuwa yako wazi na walikuwa na jukumu wakati ule wa kupambana nayo na kuhakikisha kwamba swala hili halirudi katika Bunge. Sijui ni matatizo gani ambayo yamekumba Kamati hii ya afya kuwa kakamavu katika kulifuatilia swala ... view
  • 17 Sep 2019 in Senate: Asante Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa kuchangia Mswada wa ugavi wa rasilimali kwa kaunti zetu. Kwanza ningependa kupongeza Kaunti ya Kitui na Seneta wao, Sen. Sen. Wambua, kwa makaribisho mazuri ambayo tumepewa. Jambo la pili ni kwamba sisi katika Kenya tuna Katiba lakini hatuna ukatiba. Hatuna ukatiba kwa sababu hatuheshimu sheria na utengamano katika nchi yetu. Ndio unaona kwamba katika kila sehemu kuna matatizo kadha wa kadha. Tunalalamika lakini Bunge bado linafanya yale amabayo linafanya. Tunalalamika kuwa bado Magavana wanawaibia wananchi pesa zao. Vile vile tunalalamika kwamba hatuna usawa katika ugawaji wa rasilimali za nchi hii. Nikikupa mfano wa ... view
  • 17 Sep 2019 in Senate: Railway (SGR) ambapo Serikali imetoa maagizo kwamba mizigo yote ibebwe na reli kutoka Mombasa mpaka Nairobi na baadaye hadi Naivasha. Katika Kaunti ambazo zinazalisha rasilimali zaidi katika nchi ya Kenya ni Nairobi, Kiambu, Nakuru na Mombasa. Tukiangalia zingine zote tatu zimeweza kupata ongezeko katika rasilimali ambazo zinapelekwa na Serikali Kuu katika kaunti hizo. Hatujui ni dhambi gani Mombasa ilifanya isiweze kupata rasilimali kama wanavyopata wengine. Nikiangazia swala la revenue, juzi tulipokua Mombasa tulielezwa na Kaunti kwamba wameweza kupata revenue kupita kiasi ambacho walipata mwaka uliokwisha. Kwa hivyo maswala ya revenue sio kigezo peke yake cha kuhakikisha kwamba pesa zinakwenda sawa ... view
  • 17 Sep 2019 in Senate: Bw. Naibu Spika, sijaongea leo na mara ya kwanza kuka--- view
  • 17 Sep 2019 in Senate: Naomba uniruhusu dakika moja nimalize pointi yangu. view
  • 17 Sep 2019 in Senate: Bw. Naibu Spika, tumeambiwa kwamba Seneti haiumi katika maswala ya magavana wanaoiba rasilimali. Tulipoenda Samburu, siku ya pili Gavana alishikwa. Kwa hivyo, tunataka viungo vingine vya Serikali kama Ethics Anti-Corruption Commission (EACC) na Directorate of Criminal Investigations (DCI) viwe macho zaidi, kwa sababu wao ndio wana uwezo wa kuchunguza na kushika watu wanaohusika katika maswala kama haya. Hata Seneti ikimpata Gavana wa hapa akiwa na hatia, hatuna nguvu ya kumshika na kuhakikisha kwamba amepelekwa katika kituo cha polisi na ashitakiwe. Mwisho, mahakama lazima iwe imara. Juzi Uingereza kulikua na tatizo la Bunge kuhairishwa. Mmoja wa Wabunge alienda kortini; korti ya ... view
  • 12 Sep 2019 in Senate: Asante Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Arifa iliyotelewa na Seneta wa Kitui; Sen. Wambua. Usalama wa nchi na mali yao ni jambo muhimu sana kwa taifa. Ni jukumu la kwanza kabisa la serikali yoyote kuhakikisha kwamba kuna usalama wa mali na wananchi katika nchi yake. Visa vya mauaji kama hayo yaliyotokea Kitui, yametokea Taita na sehemu zingine za nchi. Ni muhimu tuone kwamba yale mapendekezo ya community policing yanatekelezwa. Hii ni kwa sababu mauaji haya mengi yanatokea katika maeneo ambayo wananchi wanaishi katika kaunti zetu. Iwapo hatutachukua hatua za haraka, kila sehemu itapata matatizo ya ukosefu wa usalama. ... view
  • 12 Sep 2019 in Senate: Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Arifa ya Sen. (Dr.) Musuruve. Ningependa kumpongeza Sen. (Dr.) Musuruve kwa kutetea haki za wale ambao hawakubahatika katika jamii, hususan wale ambao ni walemavu. Wengi wetu hatukuwa tunajua kuwa kuna mwezi maalum ambao unahadhimisha siku ya viziwi. Lakini kwa uwezo wake ametuelimisha na sisi pia tutaendelea kuwaelimisha wengine ambao walikuwa hawajui swala kama hili. Tukiangalia hata sisi katika Bunge la Seneti na Bunge la Kitaifa, hakuna mkalimani wa lugha ya ishara ambaye anatafsiri mazungumzo ambayo yanaendelea katika Bunge kwa wale ambao hawasikii katika jamii. Kwa hivyo, kama Bunge la ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus