Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1691 to 1700 of 2095.

  • 13 Nov 2019 in Senate: inafanyika hivi sasa, kwa sababu, ukienda katika sehemu nyingi katika kaunti zetu, kwa mfano kule Mombasa, kuna sehemu ambayo iko katika eneo la Miritini katika Jomvu Constituency, ambapo kila Jumapili, watu walio na matatizo ya kijamii – kama matatizo ya ndoa na matatizo madogo madogo kama ya mipaka – wanakuja kukaa chini na kuna wazee ambao wanakuja kuyatatua matatizo kama hayo. Kwa hiyo, Sheria hii, itaweza kusaidia kuleta kutambulika kwa kazi ambazo zinafanyika kwa wale ambao tayari wanafanya kitamaduni, na vile vile watu wengine ambao wameingia katika taaluma hii kwa sasa. Kwa mfano hivi sasa, kuna vyama tofauti ambavyo vimeundwa ... view
  • 13 Nov 2019 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 13 Nov 2019 in Senate: nyingi, kiasi ambacho Wakenya hawawezi kupeleka kesi zao mahakamani ili zitatuliwe. Kwa hivyo, upatanishi na usuluhishi utasaidia pakubwa kupunguza gharama ya kupata haki katika jamii yetu. Kfungu cha nne, yaani Part 4, kinatoa fursa kwa wale ambao labda hawakuweza kuelewana, kwenda mahakamani kutatuliwa tatizo lao, baada ya kushindwa kutatua tatizo hilo kupitia kwa upatanisho na usuluhishi. Hii sheria inaleta mwongozo, kwamba kabla ya kwenda mahakamani, watu waweze kupewa fursa ili wakae chini, wajaribu kutatua mzozo ule bila ya kwenda kwa mahakama, kama nafasi ya kwanza ya kujaribu kutatua tatizo hilo. Sheria hii inatoa nafasi ya kukaa chini kabla ya kwenda ... view
  • 13 Nov 2019 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 13 Nov 2019 in Senate: Ningependa kuunga mkono Mswada huu wa Sen. Kasanga. Nawasihi Maseneta wenzangu wausome kwa kina, na waunge mkono swala kama hili. Asante, Bw. Naibu Spika. view
  • 12 Nov 2019 in Senate: Asante, Bw. Spika kwa kunipa fursa hii. Kwanza, ninaomba msamaha kwa kuchelewa kufika Bungeni kwa wakati uliyotengwa. Hii ni kwa sababu tulipata shida ya usafiri kutoka kiwanja cha ndege hadi hapa jijini kwa sababu ya msongamano wa magari. Tunaomba ile Express Highway itengenezwe haraka kwa sababu tunapoteza wakati mwingi barabarani. Hata hivyo, ninaomba kuuliza taarifa yangu. view
  • 12 Nov 2019 in Senate: Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa ambayo imeombwa Bungeni na Seneta wa Wajir, Sen. (Dr.) Abdullahi. Kwa hakika--- view
  • 12 Nov 2019 in Senate: Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa ya Senator wa Wajir, Sen. (Dr.) Abdullahi. Kwanza, ninampongeza kwa kuleta Taarifa hii Bungeni. Madeni yamekua ni donda sugu katika kaunti zetu. Hii ni kwa sababu kila kaunti ina madeni ya mamilioni ya pesa. Singependa kukosoa maelezo yaliyotolewa na Sen. Cherargei, kwamba, madeni yamebaki Kshs33 bilioni, lakini kusema ukweli, ripoti ya madeni yote ambayo yako katika kaunti iko mbele ya Kamati ya Uhasibu. Kamati hiyo imekua ikiwahoji magavana tofauti tofauti ili kuthibitisha ni pesa ngapi ambazo wanadaiwa na wananchi ambao ni wanakandarasi katika kaunti hizo. Sio kwamba hakuna sheria; sheria iko ... view
  • 12 Nov 2019 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 12 Nov 2019 in Senate: Mabibi wamekimbia kutoka kwa nyumba nyingi kwa sababu ya madeni ambayo yamekumba familia ambazo zimepatiwa kandarasi na kaunti. Ukiangalia gazeti siku ya Jumatatu na Jumanne, utapata kwamba kurasa zaidi ya kumi zimeandikwa orodha ya watu ambao wanadaiwa na benki, ambao nyumba zao na mali yao zinauzwa kwa sababu ya kushindwa kulipa madeni kutokana na kazi ambazo wamefanyia kaunti. Swala hili pia haliathiri serikali za kaunti pekee; ulipaji wa madeni umekuwa shida hata kwa Serikali kuu. Kwa hivyo, ningeomba kwamba Kamati husika, itakapoangalia swala hili, itoe mapendekezo ya mambo ambayo tunaweza kufanya kwa haraka; hata kama itabidi Controller of Budget aombwe ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus