Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1701 to 1710 of 2123.

  • 3 Dec 2019 in Senate: Asante sana Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa iliyoletwa na Sen. Mwaruma ambaye ni Seneta wa Kaunti ya Taita-Taveta. Taarifa hii imekuja wakati mwafaka. Ni karibu miaka mitatu sasa tangu pesa zianze kukusanywa lakini hakuna sheria ya kusaidia serikali za kaunti na jamii zinazoathiriwa na uchimbaji wa madini. view
  • 3 Dec 2019 in Senate: Ijapokuwa Kaunti ya Mombasa haina madini yoyote, tuna bandari inayosaidia kusafirisha madini. Kwa hivyo, wakaazi wa Mombasa wana haki ya kupata ruzuku zinazotokana na madini. Madini yanayosafirishwa kwa wingi ni Titanium lakini Kaunti ya Mombasa haijafaidika kwa vyovyote kutokana na uchimbaji wa madini. Pesa zote zimekuwa zikiwaendea wawekezaji na Serikali kama kodi. Ipo haja ya kuhakikisha kwamba maelezo haya yamefikishwa katika kamati husika ili kuwe na sheria ya kuhakikisha kwamba pesa zinagawanywa kwa haraka iwezekanavyo. view
  • 3 Dec 2019 in Senate: Asante sana, Bw. Spika. view
  • 21 Nov 2019 in Senate: Asante, Bw. Spika. Kuambatana na Kifungu cha 48(1) cha Kanuni za Bunge la Seneti, nasimama kuomba Taarifa kutoka kwa Kamati ya Usalama wa Taifa, Ulinzi na Maswala ya Nchi za Nje kuhusu kupigwa risasi na kuuawa kwa mwendeshaji pikipiki, Leonard Komora, na Mwanajeshi wa Jeshi la Wanamaji katika Kambi ya Jeshi la Wanamaji la Mtongwe, Kaunti ya Mombasa, jana asubuhi tarehe 20 November, 2019. Katika Taarifa hiyo, Kamati inapaswa - (1) Kuelezea sababu za mwendesha boda boda huyo, kijana Leonard Komora, kupigwa risasi na kuuawa. (2) Kuelezea mbona mbinu m’badala hazikutumiwa kumthibiti kijana huyo, iwapo alikuwa tishio kwa usalama. (3) ... view
  • 20 Nov 2019 in Senate: Asante sana Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia taarifa iliyosomwa na Seneta wa Bungoma, Sen. Wetangula. Taarifa hii imeletwa hapa kwa wakati mwafaka kabisa. Serikali imeendeleza utepetevu katika kutetea hadhi ya inchi ya Kenya. Itakumbukwa kwamba tuna mzozo wa mipaka na Somalia na kesi hiyo iko katika korti ya kimataifa inayohusiana na mambo ya bahari. Vile vile, kule Vanga katika Kaunti ya Kwale, wavuvi wengi hushikwa na wanamgambo wa Tanzania wakati wanavua katika Bahari ya Hindi. Kwa hivyo Bw. Spika wa Muda, bahari ama nchi yetu si jambo la kuchezewa ovyo ovyo kwa sababu kuna Wakenya wengi ... view
  • 20 Nov 2019 in Senate: Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Taarifa iliyoletwa na Sen. Cherargei. Labda angetujulisha kama ana interest yoyote kwa sababu tunajua kwamba alimaliza masomo hivi karibuni. Hata hivyo, hiyo haitaathiri umuhimu wa Taarifa hii kwa sababu wanafunzi wengi humaliza masomo katika vyuo vikuu na kupata shida ya kuajiriwa na kufungua biashara. Kwa hivyo, si rahisi wao kulipa mikopo ya HELB ambayo inaendelea kuwasonga kama watu wanaotakikana kunyongwa. Itakumbukwa kwamba Serikali ilileta mikopo ya HELB ili kusaidia wanafunzi kusoma na pia Serikali iweze kupata watu walio na tajriba na ujuzi wa fani mbali mbali nchini. Si sawa ... view
  • 20 Nov 2019 in Senate: Matokeo ya Darasa la Nane yalitolewa juzi. Ikiwa wale ambao wamesoma hawana kazi hadi sasa ilhali Serikali inawafuata kulipa mikopo, tutawafanyia nini wale wanaotaka kusoma? Itatoa taswira mbaya. Ni kama nchi inapigana na vijana wake kwa sababau hawana kazi. Pili, wanafuatwa kulipa mikopo ambayo hawawezi kulipia. Sheria ingebadilishwa ili kuwe na moratorium kwamba wasishurutishwe kulipia mikopo mpaka baada ya miaka kumi wakati wameanza kufanya biashara ama kupata kazi na kujistawisha. Bw. Spika wa Muda, nashukuru kwa kunipa fursa hii. Ningependa pia kukupongeza kwa sababu Maseneta wa Majiji katika Bunge hili ni watatu pekee. Kuna wewe, mimi na Seneta wa Kisumu. view
  • 20 Nov 2019 in Senate: Thank you, Madam Temporary Speaker. I beg to move that this House notes the report of the Parliament of Kenya Delegation to the 64th Commonwealth Parliamentary Conference (CPC) held in Kampala, Uganda from the 22nd to 29th September, 2019 laid on the Table of the House on Wednesday, 6th November, 2019. As you are aware, the Commonwealth Parliamentary Association (CPA) is an association of all Commonwealth Parliamentarians, an active network of over 17,000 parliamentarians from 180 national States, provincial and territorial Parliaments and Legislatures. The CPA organizes the Commonwealth Parliamentary Conference (CPC) annually to address the global political issues and ... view
  • 20 Nov 2019 in Senate: (1) Climate Change: Achievements, Challenges and Efficacy of Parliament Interventions. The workshop focused on the impacts of climate change and the interventions that Commonwealth Parliaments are employing to address them. Unless human beings stop fuelling climate change, it is expected that future impacts will increase evaporation hence water scarcity, shift in areas of disease patterns, biodiversity loss and extinction of species, reduced productivity of major crops and decline in pasture resulting into increased conflicts among pastoralists. I am happy to report that in this Senate, we have Sen. Olekina who is a champion fighting for the Mau Forest. (2)Innovation in ... view
  • 20 Nov 2019 in Senate: (6)Innovation in Parliament: The Possible Effects of the United Kingdom ‘Brexit’ on Small Branches. The workshop focused on the effects of ‘Brexit’ on the parliamentary procedures in the UK and how small parliaments can benefit, learn from the ramifications, and strengthen the workings of their legislatures. (7)Fostering a Culture of Respect, Fairness and Dignity: Sexual Harassment has no place in Legislatures. The workshop established that it is the responsibility of all political actors, men and women to delegitimize such deplorable and dehumanising cultures and create free and secure legislatures for all parliamentarians. (8)The role of Parliament in the doctrine of ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus