Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1911 to 1920 of 1994.

  • 16 Oct 2018 in Senate: Serikali imewapoteza vijana wasiopungua 300 sehemu ya Mombasa na kwingineko Pwani kwa sababu ya tuhuma kwamba wanashirikiana na magaidi. Mmoja katika vijana hawa ni Bw. Husni ambaye alichukuliwa mwezi wa tano mwaka huu na hadi sasa hajulikani alipo. Ijapokuwa sheria iliyoko sasa inalinda wananchi na mambo ya ugaidi, ina upungufu fulani ambao lazima ufanyiwe marekebisho ili iweze kusaidia. view
  • 16 Oct 2018 in Senate: Bw. Spika, nimefurahi kwamba kuna kifungu kilichobuniwa cha 12(e). Kifungu hiki kinasema kwamba kuwepo na County Education Board (CEB) ambayo itakuwa inaangalia mtaala unaofunzwa katika taasisi za kidini. Wengi wanaopoteza vijana wetu wanafanya hivyo kwa njia ya dini. Kwa hivyo, tukipata marekebisho katika mtaala au tuwe na mtaala mmoja katika mambo ya dini, vijana wetu watafunzwa mambo yanayojulikana ili kuepushwa na maswala ya itikadi kali. view
  • 16 Oct 2018 in Senate: Bw. Spika wa Muda, ninaomba unilinde. view
  • 16 Oct 2018 in Senate: Bw. Spika wa Muda, jambo lingine ambalo linafurahisha katika marekebisho haya ni kwamba kumependekezwa kuwa na mkuu wa taasisi ambaye atakuwa akisimamia mambo ya administration. Kwa sasa, taasisi nyingi ambazo sio za Serikali rasmi hazina msimamizi rasmi wa kuangalia kwamba wanafunzi wanafunzwa mtaala sawa. Katika Kifungu cha 12(g) majukumu ya wazazi yametolewa wazi. Wana majukumu ya kuhakikisha kwamba watoto wao hawaingii katika itikadi kali zisizojulikana. Hivi sasa, mtoto akipotea, mzazi anakua na hofu kubwa kwamba akienda kuripoti kwa polisi, yeye mwenyewe pia anaweza kuwekwa ndani kwa sababu hataweza The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. ... view
  • 16 Oct 2018 in Senate: kujieleza kwa ufasaha mtoto ameenda sehemu gani. Huenda akachukuliwa kama mtuhumiwa na itabidi abaki korokoroni, huku polisi wakitafuta habari kuhusiana na kijana yule. Kwa upande mwingine, mzazi ana hofu kwa sababu waliomchukua mtoto wake wanaweza kumuua wakisema kwamba amepiga ripoti kuhusu mwenzao na kwa hivyo, lazima wamuue ili kuepuka matatizo. Iwapo marekebisho haya yatakubalika, mzazi atakua na uwezo wa kuenda kuripoti iwapo mtoto wake amepotea kwa njia zisizojulikana. Polisi watakuwa na nafasi ya kufanya uchunguzi kujua kule kijana huyo ameenda. view
  • 16 Oct 2018 in Senate: Bw. Spika wa Muda, jambo lingine nzuri ambalo limekuja na Mswada huu ni kwamba kunatakiwa kubuniwa taasisi za kurekebisha tabia za wale waliosafiri kwa maswala ya itikadi kali na pia ugaidi. Kuna wakati ambapo wengi waliorudi walikuwa wakipelekwa Matuga Technical Training College, lakini baada ya kutoka kule, wengi wao waliachwa kivyao bila makaazi. Wale magaidi walioandamana nao safarini kule Somalia au kwingineko, wanarudi kuwaua kwa sababu wanachukuliwa kama wasaliti. Kwa hivyo, tukipata taasisi za kurekebisha tabia, wengi watapata mafunzo ili waweze kutumikia maisha yao kwa njia ya amani na kusaidia jamii katika mambo tofauti. view
  • 16 Oct 2018 in Senate: Tumeona pia wengi waliorudi kutoka kwa hizo safari za itikadi kali na ugaidi hawana makaazi. Wengi wao waliposafiri, labda walipewa USD1,000 na kuahidiwa mengi makubwa wakifika kule. Wanapofika huko na kupata shida, hawawezi kurudi huku kwa sababu inawasubiri kuwahukumu na pia jamii haiko tayari kuwakubali kwa sababu ya itikadi walizoendea kule. Kwa hivyo, taasisi za kurekebisha tabia zitasaidia pakubwa kurekebisha tabia za waathiriwa na kuwafanya wawe wananchi wa kutegemewa katika jamii. view
  • 16 Oct 2018 in Senate: Ninaunga mkono Mswada huu wa kurekebisha hii sheria ya ugaidi ili iwasaidie waathiriwa wa itikadi kali na vilevile wale waliofungwa kwa sababu ya ugaidi. Pia twaomba Serikali iangalie sana maswala ya vijana wanaopotea hivi sasa. Hii ni kwa sababu wengi wanapotea kwa mikono ya polisi ama taasisi za Serikali zinazolinda usalama wa nchi. Kwa sasa, kama nilivyotangulia kusema, kuna vijana zaidi ya 300 waliochukuliwa. Tulileta Hoja hiyo hapa na kutoa Statement, lakini hadi sasa hatujaona marekebisho yoyote ama dalili zozote kwamba hawa vijana wataachiliwa. view
  • 16 Oct 2018 in Senate: Bw. Spika wa Muda, ninaunga mkono Mswada huu wa kurekebisha sheria ya ugaidi. view
  • 2 Oct 2018 in Senate: Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii ili nijiunge na Maseneta wenzangu kulipongeza Bunge la Seneti na Karani wetu kwa vikao vyema ambavyo tulifanya mjini Eldoret. Vile vile, ninachukua fursa hii kumpongeza Sen. (Prof.) Kamar, Seneta wa Kaunti ya Uasin Gishu kwa makaribisho na kututunza vizuri kwa muda was siku tano. Ilikuwa ni tajriba nzuri kwa sisi ambao tunahudumia Seneti kwa mara ya kwanza, kwa sababu tumepata fursa ya kuonana na wananchi wengine wa Kenya ambao labda hatungeweza kuwaona katika kazi zetu za kawaida. Sio wengi wanaopata fursa kuja hapa kulitembelea Bunge la Seneti. Kwa hivyo, safari zetu katika eneo ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus