16 May 2024 in Senate:
(2) Confirm the amount of and fate of the money realized from the disposal of all scrap metals from the school, stating who was authorized to dispose and whether due process was followed in the disposition of the said scrap metals as per the relevant law. (3) The basis for the current policy of the school barring students from participating in co-curricular activities such as sports and explain the vandalism of sports facilities in the school. (4) Provide a report on the school policy on employment and deployment of the non-teaching staff in the school, giving the ethnic composition of ...
view
14 May 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia taarifa kuhusiana na kukataliwa na Bunge la Kitaifa kwa marekebisho ya Mswada wa Ugawaji wa Pesa za Kaunti. Ilikuwa sarakasi kubwa katika Bunge la Kitaifa jana wakati baadhi ya Wabunge walikuwa wanakejeli kazi zinazofanywa na serikali za kaunti. Tumeona kwamba pesa zilizo ongezwa na Serikali Kuu kwa kaunti zetu ni Kshs6 bilioni pekee yake. Zimetoka Kshs385 bilioni hadi Kshs391 bilioni. Lakini katika NG- CDF, Wabunge, wamejiongezea Kshs30 milioni kwa kila constituency . Ukifanya hesabu ya haraka, utapata ya kwamba NG-CDF imeongezewa Kshs8.6 bilioni. Haiwezekani kaunti zetu zinazofanya kazi kubwa, zipewe Kshs6 bilioni ...
view
8 May 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kutoa kauli yangu juu ya ripoti ya Kamati ya Afya iliyowasilishwa na Sen. Mandago, Seneta wa Gatuzi ya Uasin Gishu. Mgomo wa madaktari umekuwa donda sugu kwa sababu umeendelea zaidi ya mwezi mmoja sasa na hakujakuwa na muafaka wa kuutatua. Tukiangalia sehemu nyingi, wananchi wanapata shida, hususan wakati huu ambapo kumeingia mafuriko na mkurupuko wa magojwa kadhaa yanayosababishwa na maji. Ipo haja ya Serikali kukubaliana na madaktari kwa sababu wanawatumikia wananchi wa Kenya na pesa zinazolipwa wao ni za Wakenya. Sioni sababu gani Serikali ikae ngumu wakati wale wanaotaka kusaidiwa ni madaktari wanaofanya ...
view
8 May 2024 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate.
view
8 May 2024 in Senate:
Bw. Spika, masuala ambayo yanazungumziwa na madaktari ni ya kimsingi. Haya ni masuala ambayo mfanyakazi yeyote ni lazima awe nayo ili aweze kufanya kazi kwa utulivu akijua kuwa haki zake zimelindwa. Mwaka juzi tulipokuwa na janga la COVID- 19, madaktari wengi pamoja na wauguzi walipoteza maisha yao kwa sababu ya kukosa kinga. Mambo ambayo madaktari wanapigania ni mambo ya kimsingi kama ukosefu wa bima ya afya na mishahara ambayo iko chini ya kiwango wanachostahili kulipwa. Seneta Cherarkey alizungumza kuwa madaktari wanalipwa vizuri kuliko wakili ambao hawajahitimu. Ni kweli kwa sababu walinegotiate na Serikali na wakakubaliana kulipwa pesa hizo. Serikali haiwezi ...
view
8 May 2024 in Senate:
Thank you, Mr. Temporary Speaker, Sir. First of all, I also want to congratulate the hon. Cabinet Secretary for the good work he is doing even in the Coast province on the fight against illicit drugs. I have one question on the issue of extra judicial killings. I want the Cabinet Secretary to confirm whether the government policy is to still eliminate people extra judicially. So far, I have heard about three people who have suspectedly died in the hands of the police. One is Mr. Swaleh Ahmed Yussuf formerly known as ‘Kanderani’ whose body was found beside the Malindi ...
view
8 May 2024 in Senate:
Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kujibu hoja zilizotolewa na Maseneta kuhusiana na Hoja hii ya Kuidhinishwa kwa Ruzuku ya Masharti kwa Ujenzi wa Uwanja wa Munispaa ya Mombasa. Kwanza, ningependa kuwashukuru Maseneta wote ambao waliweza kuchangia Hoja hii: Sen. Madzayo, ambaye aliunga mkono wa kwanza, Sen. Maanzo, Sen. Cherarkey, Sen. Olekina, Sen. (Dr.) Khalwale, Sen. Beth Syengo, Sen. Mungatana, Sen. Omogeni, Sen. Oketch Gicheru, na mwisho, Sen. Mandago, ambao walichangia kwa lugha ya Kitaifa ya Kiswahili. Jambo la kufurahisha ni kwamba Hoja hii tumeizungumzia na kuichangia kwa lugha ya Kitaifa ya Kiswahili. Ni mara ya kwanza ...
view
8 May 2024 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate.
view
8 May 2024 in Senate:
Mchango mwingine umetoka kwa Sen. Mungatana. Unajua siku zote jicho linaona lakini jicho pia huingia kitakataka. Nashangaa Sen. Mungatana anazungumzia maswala ya Mombasa akisema kuwa tuangalie tusifuje pesa za serikali. Lakini tukiangalia Kaunti ya Tana River, haina hata uwanja wa stadium. Huu ni mchango ambao sio wa Mombasa pekee, lakini Pwani nzima. Uwanja huu utafaidi timu kutoka Tana River, Lamu, Kilifi---
view
8 May 2024 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, kauli niliyotoa ni kwamba jicho linaingia taka aka. Mhe. Bifwoli atakubaliana na mimi kuwa jicho linaweza kuingia kitakataka usiweze kuona sikusema takataka lakini kitakataka, yaani, particles kwa Kiingereza. Sen. Madzayo, fungua masikio wazi kwa sababu saa zingine maneno yataingia huku na kutoka kule. Uwanja huu hautafaidi Kaunti ya Mombasa pekee lakini utafaidi Pwani na nchi nzima. Hivi sasa tunapozungumza hatujui iwapo michezo ya Wabunge itafanyika wapi Mombasa. Hoteli tuko nazo lakini hatuna viwanja ambazo vinaweza andaa michezo kama hii. Huu ni wakati wa Serikali kunyoosha mkono kwa watu wa Pwani. Hivi sasa kuna maandalizi ya sherehe ...
view