Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 331 to 340 of 1994.

  • 15 Feb 2024 in Senate: Ningependekeza kwamba kabla Kamati iangalie swala hili, wapewe nafasi ya kuwaita the National Land Commission (NLC), Land Registrar wa Embu na landadjudication officer waeleze ni kwa sababu gani wale watu hawawezi kuruhusiwa kukaa pale mpaka wakati adjudication process itakamilika, ili wale ambao wameleta maombi yao kwenye Bunge hili wasiweze kufurushwa. Tumeona watu wanafurushwa sehemu tofauti kutoka makaazi yao. Hili jambo limekuwa la kawaida. Mapema katikati ya mwezi uliokwisha wakaazi wa Changamwe view
  • 15 Feb 2024 in Senate: walifurushwa asubuhi bila ya court order ama stakabadhi yoyote ya kisheria ya kuwataka waondoke mahali pale. Ni haki ya kila Mkenya kupata nyumba ama makao ya kudumu. Hii haki imebadilishwa na Serikali ambayo inavunja makao ya wananchi katika sehemu tofauti. Hili ni swala nyeti na lazima Kamati ya Ardhi, Mazingira na Maliasili ilivalie njuga kwa haraka ili wale wakaazi wa Embu wapate makao ya kudumu katika ardhi ambazo wamekaa kutoka jadi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate. view
  • 14 Feb 2024 in Senate: Asante Bw. Spika kwa kunipatia fursa hii kuchangia Hoja ya kuweka muda katika kujadili Hotuba ya Rais ambayo inatarajiwa mwezi wa nne. Kwanza, ninachukua fursa hii kukutakia wewe binafsi na masenata wote mwaka mpya wa elfu mbili na ishirini na nne wenye manufaa na afya njema. Pili, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwamba ametufikisha mwaka mpya na tuko tayari kufanya kazi katika kujenga taifa na kuhakikisha ya kwamba maisha ya wakenya yamebadilika. Hoja hii ni muhimu sana kwa sababu, tumeona kwamba mwaka uliyokwisha, watu wengi hawakupata fursa ya kuchangia Hotuba ya Rais na Hotuba ile ilikuwa na mambo mengi ambayo ni kinyume ... view
  • 14 Feb 2024 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Maji ya 2016. view
  • 14 Feb 2024 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate. view
  • 14 Feb 2024 in Senate: Kwanza, najiunga na wenzangu ambao wametangulia na kupinga marekebisho haya. Hii ni kwa sababu maji ni haki ya kimsingi ya kila mwanadamu. Sisi kama Wakenya, hii ni kati ya haki zetu za kimsingi. Mswada huu unajaribu kufanya maji iwe kama biashara. Hii itasababisha wananchi wa Kenya kukosa maji na kupata taabu ya kupata maji. Tukiangalia mfumo wa sasa, kule pwani, kuna Coast Water Services inayomilikiwa na Serikali Kuu. Kuna shirika ambalo linauza maji katika kila kaunti. Kwa mfano, la Mombasa ni Mombasa Water and Sewerage Services. Linanunua maji kutoka kwa Coast Water Services halafu linawauzia watu wa Mombasa. Iwapo huu ... view
  • 14 Feb 2024 in Senate: Bw. Spika wa Muda, hakuna haja ya kuwa na shirika la kuhifadhi maji kwa sababu hakuna maji ya kuwatosha binadamu na pia wanyama pori katika mbuga zetu kwa matumizi yao. Napinga Mswada huu. Nitakomea hapo. Asante kwa kunipa fursa hii. view
  • 5 Dec 2023 in Senate: Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii ili kuomboleza mwenda zake Mhe. Lawrence Sifuna ambaye alihudumu kama Mbunge katika Bunge la Kitaifa. Kifo cha mwenda zake Sifuna kimepokonya nchi hii mmoja wa viongozi wa ukombozi wa pili ambao walijitolea kihali na mali kuhakikisha ya kwamba tunapata ukombozi wa pili ambao ulikuwa ni ukombozi ambao sisi zote tunaweza kujivunia. Kujitolea kwake na wale wengine ambao walipigania ukombozi wa pili, akiwemo Baba Raila Amollo Odinga na wengine ni ushahidi wa kutosha ya kwamba wale ambao wamepigania nchi hii, wameweza kuipeleka nchi mbele na kwa sasa tunajivunia demokrasia ambayo tuko nayo katika nchi ... view
  • 5 Dec 2023 in Senate: Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii ili kuomboleza mwenda zake Mhe. Lawrence Sifuna ambaye alihudumu kama Mbunge katika Bunge la Kitaifa. Kifo cha mwenda zake Sifuna kimepokonya nchi hii mmoja wa viongozi wa ukombozi wa pili ambao walijitolea kihali na mali kuhakikisha ya kwamba tunapata ukombozi wa pili ambao ulikuwa ni ukombozi ambao sisi zote tunaweza kujivunia. Kujitolea kwake na wale wengine ambao walipigania ukombozi wa pili, akiwemo Baba Raila Amollo Odinga na wengine ni ushahidi wa kutosha ya kwamba wale ambao wamepigania nchi hii, wameweza kuipeleka nchi mbele na kwa sasa tunajivunia demokrasia ambayo tuko nayo katika nchi ... view
  • 5 Dec 2023 in Senate: Bw. Spika, jambo lingine la kusikitisha ni kwamba juzi, Shirika la Kenya view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus