Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 791 to 800 of 1995.

  • 4 Oct 2022 in Senate: Asante, Bw. Spika kwa kunipa fursa ya kuchangia katika swala hili la hoja ya nidhamu. Katika nchi yetu ya Kenya, tumebahatika kuwa na sheria tofauti ambazo zinahusiana na ndoa. Tunaweza kulinganisha maswala yanayomkumba Sen. Ali Roba na wenzake hivi sasa, na ndoa katika jamii. Ndoa ya Kiislamu inampa fursa mwanamume kuoa wake zaidi ya mmoja. Unaweza kuoa hata mpaka wa nne. Lakini ndoa ambayo hufungwa kwa Msajili wa Ndoa, huwa ni mke mmoja na mume mmoja. Mkataba uliofanyika chini ya sheria ya Political Parties, ambao tuliufanyia marekebisho Januari mwaka huu, hapa katika Bunge hili la Seneti, hairuhusu chama kuwa katika ... view
  • 4 Oct 2022 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 4 Oct 2022 in Senate: Bw. Spika, hata Rais wa hustlers amesema kwamba ataiendesha nchi kwa sheria na Katiba. Tayari wameshaanza kuikiuka Katiba. Hapa katika Bunge hili, tunaruhusu watu wanajisi Katiba. Hiyo siyo sawa. Usawa ni kwamba, ikiwa Sen. Ali Roba na chama chake wamekosana na Orange Democratic Movement (ODM), wakae pale walipo mpaka Mahakama au Registrar of Political Parties waseme kwamba hawako tena pamoja. Talaka likishapita, hakutakuwa tena na mazungumzo. Sisi pia katika ODM tutuaona kuwa hamnna haja ya kuwa na bibi ambaye hataki hiyo uhusiano. Sisi pia kama view
  • 4 Oct 2022 in Senate: , hatuna haja ya kuwa na mtu ambaye hana haja na sisi. Kwa sasa, hao bado ni wanachama wa Azimio-One Kenya Coalition Party na lazima wabaki ndani ya Azimio-One Kenya Coalition Party mpaka wakati utabatilishwa. Bw. Spika, swali hili liliulizwa mapema na Sen. (Prof.) Tom Ojienda, SC. Swala hili lilipozungumziwa, tulilichukulia kama minongono. Sen. Cheruiyot ndiye Seneta mnongono. view
  • 4 Oct 2022 in Senate: Bw. Spika, Sen. Cheruiyot alizungumza maswala ya rumour mongering . Swala lililokuwepo lilikuwa ni la kikatiba ambalo lazima litatuliwe kabla ya kusonga mbele. Swala hili litarejea pale. Tutazunguka mzunguko na hatutoki. Sen. M. Kajwang’ alipendekeza ya kwamba jina la Sen. Ali Roba liondolewa, kwa sasa, katika Kamati hilo mpaka wakati atakaposahihisha mambo yake ndipo arejee katika Kamati hilo. Asante, Bw. Spika. view
  • 4 Oct 2022 in Senate: On a point of order, Mr. Speaker, Sir. view
  • 4 Oct 2022 in Senate: Nimeona baadhi ya Maseneta wakiinua mikono ni kama tuko kwenye darasa. Mwongozo uliotolewa mapema na Spika ulikuwa kwamba kama unataka kuongea ama kuchangia Hoja iliyoko kwenye meza, ni lazima ubonyeze kidude kilichoandikwa ‘ microphone.’ Nimeona Sen. Tabitha Keroche akipata shida. Anainua mkono akiregesha. Juzi tulipokuwa Nakuru County alitukaribisha vizuri sana. Kwa hivyo, nasikitika kwamba hajaweza kupata utaalamu na nafikiri hasaidiki pale. Mimi nimekaa na Sen. Betty Montet na Profesa na ninawaongoza jinsi ya kuchangia. Mimi nashangaa kwamba Sen. Tabitha Keroche, Deputy Minority Leader, ameshindwa kujieleza. view
  • 4 Oct 2022 in Senate: Bw. Spika, sijachangia Hoja hii ya kuundwa kwa Kamati. Nimezungumza kwa hoja ya nidhamu . view
  • 4 Oct 2022 in Senate: Bw. Spika, Kamati inayobuniwa ni muhimu kwa Bunge la Seneti. Ni Kamati ambayo itatoa mwongozo kwa kazi yote inayoendeshwa katika Bunge hili. Kwa hivyo, hatuwezi kupuuza hii Kamati. Kama Bunge la Seneti na ikiwa hili ndilo swala letu la kwanza ambalo liko mbele yetu, ni lazima tufuate sheria kulingana na Katiba na Kanuni zetu za Bunge la Seneti. Tumeona kwamba baadhi ya majina yaliyopendekezwa yameleta utata. Utata ni kwamba; je, Sen. Ali Roba amependekezwa na upande wa walio wengi ama upande wa walio wachache? Mheshimiwa Spika, swala la ni nani walio wengi au wachache katika Bunge hili ni swali ambalo ... view
  • 4 Oct 2022 in Senate: Bw. Spika, ungenilinda kwa sababu ya Sen. Cherarkey. Tafadhali naongea. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus