Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 801 to 810 of 2110.

  • 22 Nov 2022 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 22 Nov 2022 in Senate: utafiti wa Kisayansi wa kutosha kuthibitisha kuwa vyakula hivi vilikuwa salama kwa Wakenya. Mpaka sasa, hatujapata utafiti kamili wa kuthibitisha vyakula hivi viko salama kwa wakenya. Kule Kitui, kuna wakati ndugu zetu walifariki kwa kula mahindi yaliyokuwa yameharibiwa na sumu ya kuvu. Bw. Spika wa Muda, naomba unilinde kwa sababu sitaweza kumaliza. Nimekwisha washiwa taa hapa, point of order zinakuja pia. Angeniliwacha nimalize kuchangia halafu yeye atapewa fursa nyingine. Bw. Spika wa Muda tunasema kwamba-- - view
  • 22 Nov 2022 in Senate: Bw. Spika wa Muda wakati wangu mwingi umetumika kwa hoja za nidhamu ambazo hazina msingi wa nidhamu yoyote. Bw. Spika wa Muda, Sen. (Dr) Khalwle anazungumzia germs ambavyo ni virusi. Lakini genetics ni viini ambavyo vinaunda mwili wa binadamu ama mwili wa mnyama yoyote ambaye anahusika. Hivyo basi tunasema kwa sasa hatujakuwa na utaalamu katika nchi yetu ya Kenya kuthibitisha kwamba vyakula hivi ni salama kwa wananchi wetu. Kwa sababu hiyo, haitakuwa sawa ile marufuku kuondolewa kwa sababu watu wengi watapata shida ya vyakula ambavyo hawajui vinatoka wapi. Bw. Spika wa Muda, kuna nchi nyingi ambazo zina vyakula hivi na ... view
  • 22 Nov 2022 in Senate: Bw. Spika wa Muda, ni kweli tuna upungufu wa mahindi lakini, tayari katika East view
  • 22 Nov 2022 in Senate: tunaweza kupata mahindi kutoka Tanzania, Malawi, CommonMarket for Eastern and Southern Africa (COMESA) na Uganda. Kwa hivyo, kwa wakati huu, haifai kuleta vyakula kama hivi ambavyo vina utata na hatujui madhara yake. view
  • 22 Nov 2022 in Senate: Kwa kumalizia, wiki tatu zilizopita, nilizungumzia zile dawa za kututumua mwili ambazo dada wengi wanatumia kupanua makalio. Hivi vyakula vya Kisaki ama Genetically Modified Organism (GMO) vitakuwa na athari kama hiyo ambayo kwa sasa hatujui. Tayari, kuna mkurupuko ya magonjwa ya cancer nchini mwetu. Cancer za koo na za matiti kwa kina dada. Saratani za tumbo kwa watu wengi zimeongezeka haza kwa wanaume ambao zaidi wanapata athari kama hizo. Kwa sasa, tukiruhusu vyakula hivi, itakuwa tunahatarisha maisha ya wananchi wa Kenya. view
  • 22 Nov 2022 in Senate: Bw. Spika wa Muda, mwisho ni kuwa, ilikuwa ni kejeli kwa Waziri Moses Kuria kusema kuwa wananchi wa Kenya tayari wanakufa na wanaendelea kufa kwa hivyo hata wakifa kwa GMO itakuwa hakuna hasara yoyote. Hiyo ni kuonyesha kwamba hajali maisha ya Mkenya katika nchi yetu. view
  • 17 Nov 2022 in Senate: Bw. Spika, niko na hoja ya nidhamu. Hoja yangu nikwamba Seneta wa Kaunti ya Nandi, anazungumzia ripoti ya Ruaraka iliyoletwa katika Bunge la Kumi na Mbili. Yeye ni mmoja kati ya wale Maseneta waliopiga kura kuangusha Ripoti hiyo. Je, ni haki kuzungumzia Ripoti ambayo yeye mwenyewe alikuwa ni mmoja wa wale ambao walipiga kura kuangusha? view
  • 17 Nov 2022 in Senate: Mgogoro huu wa shamba la Ruaraka ulichunguzwa na Kamati iliyoongozwa na Seneta wa Homa Bay, Sen. M. Kajwang’. Baadhi ya mapendekezo kwenye Ripoti ya Kamati ilikuwa wale wote walihusika katika malipo ya ile ardhi ya Ruaraka wachunguzwe na wafunguliwe mashtaka kutokana na ulipaji wa pesa taslimu billioni moja na laki tano za Kenya kwa ardhi ya serikali. view
  • 17 Nov 2022 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus