Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 811 to 820 of 1995.

  • 16 Jun 2022 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 15 Jun 2022 in Senate: Asante Bi. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa iliyoletwa Bungeni na Sen. Olekina kuhusiana na ongezeko la mafuta na usimamizi wa mafuta ya petroli katika nchi yetu. view
  • 15 Jun 2022 in Senate: ya Sen. Olekina imegonga ndipo kwa sababu kwa muda wa karibu mwaka mmoja, tumeona bei ya mafuta ikiendelea kupanda. Kwanza tuliambiwa ya kwamba hii shida imesababishwa na vita ambavyo vipo kati ya Russia na Ukraine. Lakini tumeona ya kwamba vita vinaendelea kwa muda wa miezi minne na hakujakuwa na upungufu wowote wa mafuta haya ambayo yanaongezwa bei mara kwa mara hapa nchini kwetu. Tutakumbuka ya kwamba bei za mafuta ilianza kupanda wakati kiwanda cha Kenya Petroleum Refineries kilipofungwa katika Mji wa Mombasa. Bi. Naibu wa Spika, hili ndilo jambo ambalo lilipelekea wengi kuagiza mafuta kibinafsi. Hiyo ndiyo inayosabisha mkurupuko wa ... view
  • 15 Jun 2022 in Senate: Asante, Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Kwanza, ningependa kuipongeza Kamati hii kwa kazi kubwa ambayo wamefanya kwa muda waliokuwa nao. Mimi nilibahatika kuhudumu katika Kamati hii kutoka mwaka wa 2018 mpaka 2020. Katika kipindi hicho, tulifanya kazi kubwa sana kwa sababu zile ripoti zote za mkaguzi kabla ya mwaka wa 2017, zilikuwa hazijachunguzwa bado. Kamati yetu ilihudumu na ikachunguza hizo ripoti zote na tukazileta katika Bunge hili la Seneti. Tuliidhinisha nyingi ya ripoti hizo lakini jambo la kusikitisha ni kwamba mpaka leo, hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na taasisi za Serikali. Ninazungumzia taasisi view
  • 15 Jun 2022 in Senate: kama vile ofisi ya Auditor-General, Ethics and Anti-Corruption Commission (EACC) na Directorate of Criminal Investigations (DCI). Hizi taasisi zilitakiwa kuchukua hatua kisheria kutokana na ripoti hizo. Ripoti nyingi zilionyesha ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma. Ubadhirifu wenyewe ulifanywa na magavana waliokuwa ofisini. Mpaka sasa, wengine wao bado wako ofisini. Bi. Spika wa Muda, Seneti imefanya kazi kubwa. Hata hivyo, hakuna hatua zozote za kisheria ambazo zimeidhinishwa kwa baadhi ya maafisa waliochukua imprest na kukosa kurudisha. Wanatakiwa kushitakuwa na wapokonywe mali yao kulingana na sheria kwa sababu ya kutorudisha imprest . Waliovuja pesa hizi kwa njia moja au nyingine, pia hawajakuchukuliwa ... view
  • 15 Jun 2022 in Senate: . Madeni ya kaunti zetu yanaongezeka licha ya kwamba kulikuwapo na kamati maalum, ambazo ziliundwa na Council of Governors (CoG) pamoja na watu wengine. Walifanya uchunguzi wa madeni haya lakini mpaka leo, madeni yanaendelea kuongezeka. Haya yote yanatokana na unyonge ambao uko katika mabunge ya kaunti. Tumeona kwamba baadhi ya fedha hazichunguzwi na Seneti. Kwa mfano, fedha ambazo kaunti inakusanya yaani o wn source revenue, h aziangaliwi wala matumizi yake kuchunguzwa na Seneti. Inatakikana utumizi wa fedha hizi uchunguzwe na bunge la kaunti. Kuna unyonge mkubwa katika mabunge haya, hivi kwamba hawawezi kuchunguza hesabu hizo. Hata wakichunguza, wanafanya hivyo kwa ... view
  • 15 Jun 2022 in Senate: Bi. Spika wa Muda, pia tumeona ya kwamba ofisi ya Auditor-General mara nyingi wanakwenda vitandani na serikali za kaunti. Katika repoti zao unapata mambo ya kuwa mambo yale mazito; mambo yale makubwa ya ubadirifu wa pesa hawayaangazi, bali wanaangazia mambo madogo madogo kama vile kukosa kufanya bankreconciliation, kukosa kufanya cash and bank balances kwa usawa. Hayo ni mambo madogo madogo ambayo hayaonyeshi ubadhirifu wa pesa lakini zile fedha nyingi ambazo zinaliwa katika miradi ambayo haikamiliki zote huwa zinazibwa na ofisi ya Auditor-General na hivyo inakuwa vugumu kwa Bunge la Senate kuweza kuziangalia kama fedha hizo zimetumika kisawasawa. Jambo la nne ... view
  • 15 Jun 2022 in Senate: kutoa huduma kwa wananchi katika sehemu zile. Mabaraza hayo yalikuwa yanakusanya fedha nyingi kiasi ambacho kiliweza kulipa mishahara, kutoa huduma na vilevile kupanga miradi ya maendeleo katika maeneo yao. Tukiangalia sasa, kaunti nyingi zinategemea pesa zinazotoka kwa Serikali kuu. Hii inazidi kutia unyonge kwa sababu pesa zikichelewa unasikia mishahara haijalipwa, watu hawaji kazi; unaskia mradi umekwama, watu wanagoma. Na hivyo basi, inatatiza huduma. Kama leo, kuna mambo mawili yamezungumziwa hapabunge kuhusiana na Garissa Teaching and Referral Hospital ambapo huduma zimedorora. Mhe. Sen, Ndwiga ameguzia kwamba katika Kaunti ya Embu pia huduma za afya zimedorora. Yote imesababishwa na kuwa pesa ambazo ... view
  • 15 Jun 2022 in Senate: Ahsante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Mswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Watoto ambao umewasilishwa Bungeni na Kiongozi wa Wengi katika Bunge hili la Seneti. Kwanza kabisa, ningependa kusema kuwa Mswada huu unatilia nguvu Kipengele cha 53 cha Katiba ya Kenya kinachozungumzia haki za watoto. Ni Mswada unaolenga kutia nguvu haki za watuto, majukumu ya wazazi katika malezi ya watoto na njia mbadala za kulea watoto, uhifadhi wa watoto, kulinda watoto na jinsi ya kushughulikia watoto ambao wamekiuka sheria. Kwa sasa, mtoto akifanya makosa, polisi humweka pamoja na watu wazima. Hiyo inahujumu haki za watoto ... view
  • 15 Jun 2022 in Senate: Bi. Spika wa Muda, kulinda haki za watoto na kuwawekea masilahi bora ndio lengo kuu la sheria hii. Ni jukumu letu sisi kama Senate kuweza kupitisha sheria hii ili kuweza kuona kwamba masilahi ya watoto yamelindwa. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus