15 Jun 2022 in Senate:
Tumeangalia zile vipengele tofauti vya sheria hii na tunaona kwamba vyote vitasaidia pakubwa. Ni sheria ambayo italinda watoto wetu katika mambo tofauti. Kwa mfano, katika kifungu cha pili, haki za watoto zimetajwa. Watoto wanastahili kupata maisha na malezi bora, licha ya kuwa wana ulemavu au bila. Tunaona jamii nyingi zikipata mtoto mwenye ulemavu, mara nyingi watoto wale hawapelekwi shule na hawapati huduma za matibabu. Inakuwa ni kama wamelaaniwa. Watoto wote wako sawa na wana haki ya kupata huduma sawa kama watoto. Malezi ya watoto pia yamezingatiwa na mzazi ana jukumu ya kumlea mtoto wake hadi afike miaka kumi na nane. ...
view
15 Jun 2022 in Senate:
Mwisho kabisa ni kwamba watoto wale watalindwa na sheria ya kiislamu. Kwa hivyo, haiwezekani kwamba upande mmoja umesukumwa kuingia katika Mahakama za Watoto na upande mwingine wamesukumwa kuingia katika Mahakama ya Kadhi. Wakati Kadhi inaaamua maswala ya ndoa, anaamua pia maswala ibuka kama ya maangalizi ya watoto ambao wanatokana na ndoa hili.
view
15 Jun 2022 in Senate:
Bi, Spika wa Muda, nikimalizia, ijapokuwa ipo sheria ya watoto kwa sasa ina changamoto nyingi. Kwa mfano, ni wakati mtoto amefiliwa na mzazi wake na anchukuliwa na nyanya au babu kuangaliwa.
view
15 Jun 2022 in Senate:
Mara nyingi huwa ni shida kuwapatia kwa mfano, huduma za afya kupitia kwa bima ya afya kwa sababu watoto wale hawana vitambulisho na vitambulisho vya wazazi wao vimekwisha. Kwa hivyo, ni lazima wapate kitambulisho cha babu ili aweze kuwasimamimia kuhusiana na maswala yale. Mara nyingi huwa ni vigumu kupata amri ya mahakama ya kadhi kuweza kuwapa jukumu wazazi wale kuangalia watoto ambao ni wajukuu ambao wamo mkononi mwao.
view
15 Jun 2022 in Senate:
Nafikiri Sheria hii itafanya mambo hayo kuwa mepesi. Mtu ambaye ameondokewa na mtoto wake na akaachiwa wajukuu kuangalia itakuwa rahisi kupata idhini ya kumwezesha kusimamia watoto wale kikamilifu.
view
15 Jun 2022 in Senate:
Kuna pia Suala la mahali pa hifadhi ama rescue centre. Tumeona watoto wengi wakichukuliwa kwa mfano katika misako mjini na kupelekwa katika vituo vya polisi ambapo wanakaa seli na watu wazima ambao ni kama wazazi wao.
view
15 Jun 2022 in Senate:
Kama tunavyojua, seli za polisi hazina vyumba tofauti vya wafungwa. Wafungwa wote wanawekwa pamoja kama mahabusu na labda yule mtoto hakufanya uhalifu wowote. Lakini, atakapotoka pale, kwa sababu ameingiliana na wahalifu, anaanza kuwa na hulka za kuwa mhalifu.
view
15 Jun 2022 in Senate:
Ni vizuri Mswada huu upite ndipo tupate rescue centres za kuwahudumia watoto kama hawa ambao wanahitaji huduma lakini hawana mahali pa kupata huduma hizi. Zamani kulikuwa na taasisi nyingi. Kwa mfano, kule Mombasa kulikuwa na approvedschool ambayo ilikuwa inawahudumia watoto kama hao ambao wamechukuliwa barabarani na ambao wameshindwa na shule za kawaida kwenda kusomeshwa masomo ya ufundi katika sehemu zile.
view
15 Jun 2022 in Senate:
Hivi sasa kutokana na upungufu wa fedha na serikali zetu za kaunti, huduma hii imeeza kugatuliwa lakini hawatowi pesa za kutosha kuzisimamia huduma kama hizi. Kwa hivyo ni bora ninaona jukumu la serikali za kaunti limeangaziwa katika Mswada huu. Itakuwa bora Mswada huu utakapoidhinishwa serikali zetu za kaunti ziweze kutenga fedha fulani za kusimamia mambo kama haya.
view
15 Jun 2022 in Senate:
Vile vile tunaona kwamba katika miji mingi utapata wako watoto wengi ambao wametumwa kuomba. Utaona wanasimama kwenye mabarabara wakiomba pesa kwa wazazi wao. Inatoa taswira mbaya ya nchi yetu na mji yetu. Kwa hivyo sehemu kama hizi zitasaidia pakubwa kuwachukuwa watoto kama wale waende shule na kufundishwa ufundi. Wakitoka pale watakuwa wananchi wa kuaminika na kusaidia kujenga nchi yetu.
view