10 Nov 2022 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa iliyowasilishwa na Sen. Crystal Asige. Naunga mkono Taarifa hii ya Sen. Crystal Asige kwa sababu mambo yanayoangaziwa katika Taarifa hii ni ya kimsingi. Nilibahatika kuwa mwanachama wa Rotary Club of Mombasa. Kila baada ya wiki mbili, huwa tunakwenda kuwalisha watoto walemavu katika Shule ya Port Reitz. Ukiona wale watoto wanavyoishi, utagundua kwamba ipo haja ya kuwasaidia ili waishi angalau maisha mazuri kidogo. Wakati tunapokwenda kuwatembelea wanafunzi katika Shule ya Port Reitz ambayo ni ya watoto walemavu, huwa tunapata kuwa walimu hawatoshi ukilinganisha na idadi ya wanafunzi. Mbali na kuwapelekea chakula, sisi ...
view
10 Nov 2022 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
10 Nov 2022 in Senate:
Mwisho, Bw. Spika, ni kwamba wakati watoto hao wanapokua, ni vigumu sana kupata vyeti kuonyesha kwamba ni walemavu. Lazima mtoto kama huyo alipe Kshs1,500 katika hospitali za kaunti ili apewe cheti cha kuonyesha kwamba ni mlemavu, ndiposa aweze kupata marupurupu ama fadhila zingine za kuonyesha kwamba ni mlemavu. Katika jamii, sisi tunatakikana tuwasaidie zaidi kuliko tunavyojisaidia sisi wenyewe. Bw. Spika, naunga mkono Taarifa hii.
view
10 Nov 2022 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Nimesikia Mhe. Munyi Mundigi, Seneta wa Embu akizungumzia swala la Muguka. Swala hili kwa watu wa Mombasa limezua utata kwa sababu ulaji wa Muguka umeharibu nyumba nyingi na vijana wengi sana. Hao vijana badala ya kufanya kazi wanarandaranda, wanawacha mabibi zao nyumbani---
view
10 Nov 2022 in Senate:
Bw. Spika, singependa kujulishwa chochote na Seneta wa Meru kwa sababu najua athari za Miraa na Muguka . Vijana wengi wameathirika na mambo haya. Mbali wanalia kwamba ushuru na kodi wanazotozwa ziko juu, ningependekeza ziongezwe maradufu ili mmea huo usiweze kufika Mombasa na Pwani kwa jumla ili vijana wetu waokoke. Kila kijana ambaye amemaliza shule hukimbia kukaa kula
view
10 Nov 2022 in Senate:
. Wengi hawataki kufanya kazi na wengi hawataki kuoa.
view
10 Nov 2022 in Senate:
Hawataki kuoa kwa sababu uwezo wao wa kushika nyumba umeathiriwa na mmea huo.
view
10 Nov 2022 in Senate:
Bw. Spika, kushika nyumba ni neno la kistaarabu linalomaanisha kwamba wameshindwa kustarehe na wake zao. Ukiniambia kustarehe ni nini, ni bwana kumuingilia mke wake wa halali ama yule kimada ambaye yuko naye.
view
10 Nov 2022 in Senate:
Bw. Spika, hili swala la Miraa na Muguka ni nyeti katika eneo la Kaunti ya Mombasa na tumelizungumzia. Tuko na utafiti ambao umefanyika unaonyesha athari hizi za mimea hii miwili. Ni kama bhangi. Bhangi ilipigwa marufuku kwa sababu ukivuta bhangi inafanya kichwa chako kuruka. Kwa hivyo, ukila Muguka na “miraa” kwa siku mbili mfululizo---
view