Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 841 to 850 of 1995.

  • 14 Jun 2022 in Senate: Bi. Spika wa Muda, kulingana na tarakimu ambazo zilisomwa Bungeni, kutakuwa na upungufu wa karibu Kshs800 billion. Hizi zinatakikana ziweze kupata ufadhili ama ulipaji ili ndio bajeti iweze kuwa sawa sawa. view
  • 14 Jun 2022 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 14 Jun 2022 in Senate: Iwapo nchi itaweza kupita kiwango chake cha deni cha Kshs9 trillion, itasababisha mkurupuko wa ongezeko la bei. Vile vile shilingi yetu ya Kenya itazidi kudorora dhidi ya dola na hapo itakuwa kizungumkuti katika uchumi wa nchi yetu ya Kenya. view
  • 14 Jun 2022 in Senate: Sababu ambazo zimesababisha ongezeko hili ziko wazi. Uchumi uliadhirika zaidi kutokana na janga la korona kwa muda wa miaka miwili na mpaka sasa zile hatari za korona zinaendelea kuadhiri uchumi wetu. Vile vile, swala la vita kati ya Urusi na Ukraine limechangia pakubwa sana kwa sababu kulikuwa na bidhaa nyingi kwa mfano mafuta ambayo bei yake inaendelea kuongezeka na pia bei ya bidhaa kama chakula na mbolea ambazo zinatoka sehemu ya Ukraine zimeongezeka maradufu. view
  • 14 Jun 2022 in Senate: Bi. Spika wa Muda, kwa hivyo inamaanisha nchi haitaweza kutumia fedha nyingi zaidi kukopa na kuweza kuagiza bidhaa ambazo hazipatikani hapa nchini Kenya. Jambo lingine ni kwamba sarafu ya dola pia imeimarika kiuchumi. Ina maana ya kwamba shilingi yetu itazidi kudorora dhidi ya dola mpaka wakati uchumi wetu utaimarika. view
  • 14 Jun 2022 in Senate: Sen. Mwaura amesema haimanishi kwamba kama kuna mkurupuko ama ongezeko la idadi ya watu inamaanisha pia kuna ongezeko la matumizi. Hilo ni swala ambalo liko wazi. Wale watoto wanaozaliwa watahitaji shule na matibabu. Kwa hivyo, ikiwa tulikuwa na hospitali za kutibu watu hamsini na tuna watu mia moja inamaanisha ni lazima tuongeze idadi ya hospital ama uwezo wa hospitali zile kuweza kuhudumia watu mia moja. view
  • 14 Jun 2022 in Senate: Bi. Spika wa Muda, si ukweli kwamba ongezeko la watu halimaanishi ni ongezeko la matumizi ya Serikali. Watu wale wanahitaji shule, masoko, barabara za kupita na usalama. Huduma zote zinaotolewa na Serikali zinaongezeka wakati ongezeko la wananchi katika nchi linapoongezeka. Sio kweli kwamba bajeti itakuwa ile ile. Ikiwa bajeti ni ile ile inamaanisha uchumi haukui. Kama uchumi haukui ina maana tutakuwa tuko sehemu ile ile ya maendeleo kuliko vile ambavyo ingefanyika kama uchumi ungekua unakua. view
  • 14 Jun 2022 in Senate: Swala la ufisadi ni donda sugu. Kuna baadhi ya watu katika Serikali ambao wameshtakiwa tayari kwa maswala ya ufisadi. Tunajua kuna kesi ambazo ziko mbele ya mahakama kuhusiana na mabwawa ya Kimwarer na Arror. Pesa zote zilitumiwa katika miradi ile ni za kukopa. Mradi haujafanyika mpaka sasa. Kwa hivyo, ina maana kwamba Serikali inalipa mkopo wakati pesa ambazo zilitumika kwenye mkopo hazikutumika kisawasawa kiuchumi. view
  • 14 Jun 2022 in Senate: Bi. Spika wa Muda, baadhi ya mikopo imekwenda katika mifuko ambayo haikustahili na tunakubali hiyo. Lakini, hiyo haimaanishi kwamba tuikataze Serikali kuw na pumzi za kupata mikopo ingine ili waweze kuendeleza maendeleo katika nchi yetu. view
  • 14 Jun 2022 in Senate: Nampongeza Sen. (Dr.) Musuruve kwa mchango wake. Sen. Olekina pia amechangia kwa ufasaha zaidi swala hii kwamba uchumi uliadhiriwa na korona na kwa mazingara mabaya ya nchi baada ya korona. Uchumi unaendelea kuadhirika sababu ya vita baina ya Ukraine na Urusi. Uchumi umeadhirika kwa sababu dola ni sarafu ambayo imeimarika kiuchumi ulimwengu mzima. Hii ina maana zile sarafu zingine bado zitakuwa zinapata shida kushindana na dola kikamilifu. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus