29 Apr 2015 in Senate:
Mr. Temporary Chairperson, Sir, I oppose that amendment. I am talking on behalf of the people of Kilifi who normally take their drinks straight from the coconut tree at a very reasonable price. Therefore, I do not think that it is going to be practical and necessary to bottle our drinks.
view
1 Apr 2015 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda. Waswahili husema, “Mwanzo wa ngoma ni lele.” Sisi kama Wakenya tunaona tuna mwanzo mwema hapa. Ukiangalia ndani ya Seneti hii utaona kuna matumaini na hamu ya kuona Kenya inapoelekea. Bw. Spika wa Muda, wangapi kati yetu wanaomba msamaha? Mhe. Rais ametoa mfano mwema hata mpaka kwa watoto wetu na vizazi vyetu. Nimesimama hapa kama mama ambaye amejifungua na ukiangalia huduma hospitalini, ni kitu cha kufurahisha sana. Kitu ambacho ninaomba tukitilie mkazo ni kuangalia pia kabla ya kuzaa. Akisha jifungua mama tutafanya aje ili nchi yetu ielekee na kujua kwamba mwanamke amezalishwa bure. Kwa hivyo, tutafanya ...
view
17 Mar 2015 in Senate:
Asante Bw. Spika wa Muda. Naomba hata mimi nichangie Hoja hii. Bwana Kerrow ana kero nyingi tangu jana kulingana na vile nilivyomuona kwenye runinga. Swala la usalama ni la muhimu sana. Saa hizi, mimi kama mama nashangaa vile kulivyo huko Mandera. Shule zilifungwa huko Mandera na itakapofika mwezi wa nane, watoto wa Mandera wahitajika kufanya mitihani kama wengine. Lazima tutie nywele maji kabla ya Boko Haram kuja hapa.
view
12 Mar 2015 in National Assembly:
Asante, Bw. Spika wa Muda. Hoja hii imeniacha hoi kwa sababu mwamba ngoma huvutia kwake. Je, ni kweli dada Sen. (Dr.) Zani kama Mpwani anataka tuiunge Hoja hii mkono? Kama Wapwani tuna nini? Mimi nikiwa na uwezo ndio ningefanya choyo niseme kila mtu ale chake. Je, tulipofika sasa baada ya miaka 50 kutoka tupate Uhuru, tunasema kila mtu ale chake? Naipinga Hoja hii kwa sababu mimi mwenyewe nilianzia shule ya chekechea mashambani. Nikaenda shule mjini ya secondari na chuo kikuu. Nilijiunga na Aga Khan nikiwa mtu mzima. Bw. Spika wa Muda, labda dada Sen. (Dr.) Zani anaongea kwa niaba ya ...
view
12 Mar 2015 in National Assembly:
Bw. Spika wa Muda, nilitumia neno ‘labda.’ Kwa hivyo, kama sen. (Prof.) Anyang’-Nyong’o anajiweza, leo jioni nitajua kama anaweza kuzungumza lugha ya Kiswahili.
view
12 Mar 2015 in National Assembly:
Asante, Bw. Spika wa Muda. Nafikiri atakuwa na wakati wa kunikosoa kwa sababu hapo mbeleni, Sen. Kagwe alikuwa akitaka sekta ya elimu igatuliwe. Kwa hivyo, siko mbali na Hoja aliyotoa. Sidhani kama nimeteleza. Unikosoe kama nimeteleza. Nilikuwa tu najaribu kutetea. Mambo yaliyo katika Hoja hii yakigatuliwa itakuwa vipi? Wacha nimalize hapo kwa sababu naona kama nakosea. Hata hivyo, wapwani hatujafikia kile kiwango cha wenzetu. Hatujafikia kima cha shule za upili za Alliance na Maranda. Kwenye gazeti la leo, mwanafunzi wa kwanza katika shule moja huko Kwale alipata Gredi C-. Wale waliopata Gredi E, ambayo yaitwa reki, ni 37. Huo ndio ...
view
10 Mar 2015 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa muda zaidi ili niendelee na kuchangia Mswada huu ambao tunataka kupitisha. Maana ya harambee ni kujumuika, kutabaruku na kuvuta pamoja. Tukiangalia tutaona ya kwamba huwezi kusema kama kitu si kizuri ama hakifuatwi vile ipasavyo, kitupiliwe mbali. Harambee zinatujenga sana. Nimefanya utafiti na watu wangu kule vijijini na wakanipasha ya kwamba, wao wanaenda kwa harambee, kwa sababu kadha wa kadha.Kwa mfano,malipo ya hospitali hayaepukiki. Sio kila mmoja wetu ana ule uwezo, kibali fulani ama analipiwa na shirika fulani. Hapo ndio watu wangu hutafuta harambee. Lakini tukiangalia mbali na yale malipo ya hospitali, utaona ya kwamba ...
view
5 Mar 2015 in Senate:
Asante sana Bw. Spika wa Muda. Kusema kweli, kichwa kimeniuma mchana mzima. Mimi ninatoka katika Kaunti ya Kilifi na sipingi sheria hii. Lakini hata mtoto pia akizaliwa, atanyonyeshwa halafu utaangalia njia zingine za kumpa chakula kabla ya kuamua kuwa hautamnyonyesha tena. Tukiangalia wanyama vile vile, utaona kwamba hakuna mzazi anayemuacha mtoto wake mara moja. Nilivyosema kuwa natoka Kilifi, ni kwamba sisi huko hatuwezi kuishi bila ya harambee. Sipingi Hoja hii, lakini lazima tuangalie njia nyingine mbadala za kuwasaidia watu wetu kwenye sheria hii. Je, kutakuwa na hazina fulani ambayo wale ambao wako kwenye kaunti ambazo ziko chini kimaendeleo na ambazo ...
view
19 Nov 2014 in Senate:
Asante Bw. Spika wa Muda. Pia, natandaza wingu la simanzi hapa Seneti. Kazi ya Mungu haina makosa. Ule ucheshi, umahiri, sifa, na haiba yake Sen. Kajwang hatuwezi kusahau. Ni huzuni kubwa. Niliona ujumbe wa 411 lakini ni kama kichwa changu hakikukubali kuwa ni Sen. Otieno Kajwang. Nilipokuja Seneti leo na kuona picha ya Seneta Kajwang, nilipata huzuni kubwa sana. Niliona sasa ni kweli kuwa kifo kimetupokonya mtu mahiri na shujaa. Kifo kimetuleta pamoja na wale wa upande mwingine, na sisi wa huku Serikalini ndio tumesikia majonzi makubwa kwa sababu pale ninapoketi, Bw. Spika wa Muda, ni upande wa pili kabisa. ...
view