17 Oct 2024 in Senate:
Bw. Spika, naunga mkono Hoja hii ili tuwe na nafasi ya kumsikiliza Naibu wa Rais siku ya Jumamosi. Tunaelewa kwamba hii ni kesi muhimu sana na macho yote nchini yanaangalia Seneti. Napeana pole zangu kupitia Senior Counsel, Mhe. Paul Muite, kwa sababu client wake ni mgonjwa. Ugonjwa ni jambo la Mwenyezi Mungu. Hatuwezi kusema kwamba mtu hawezi kuwa mgonjwa. Mtu yeyote anaweza kuwa mgonjwa. Kwa hivyo, ningependa afikishe pole za Seneti. Tunamtakia kila la heri. Mwenyezi Mungu ampe nafuu ili tupatane hapa. Bw. Spika, tuko katika njia panda; ni mgonjwa. Je, tuendelee ama tusiendelee? Tumpe nafasi. Kama binadamu, hii ni ...
view
17 Oct 2024 in Senate:
Asante, Mhe. Spika. Naunga mkono Hoja hii inayohusu kumng’atua mamlakani Naibu wa Rais. Katika Kanuni zetu za Kudumu, Kipengele 145, kinaongea jinsi Rais ama Naibu Rais anavyoweza kuondolewa mamlakani. Kwanza, mashtaka yote yalioko mbele yetu kuhusu ukosefu wa nidhamu au nidhamu kwa Wakenya, inasikitisha kusikia Naibu Rais akisema kwamba Kenya ni kampuni na kwamba iko na hisa na kama hukuwapigia kura kama walivyotaka, utangojea sana kupata maendeleo. Mtu akiwa Naibu Rais anakuwa kiungo muhimu cha kuunganisha taifa. Ukiwa Naibu Rais uliyechaguliwa, maendeleo ni lazima yafike mashinani kote nchini kwa waliokupigia kura na hata wale ambao hawakukupigia kura. Wewe ni kama ...
view
17 Oct 2024 in Senate:
kutoka Mombasa hadi Malindi iligeuzwa katikati na ikaenda kwa hoteli inayoitwa Vipingo Beach Resort Limited. Huo ni mradi ambao ungefaidisha zaidi watu wa Kilifi hususan wakulima, wafanyibiashara na wananchi lakini yeye akaigeuza ikaenda kwake. Nilipata fursa ya kuenda huko. Barabara hiyo imehepa mikanju na miembe ikienda kwenye hiyo hoteli. Hivyo sio namna barabara zinavyotengenezwa. Huo ni ukiukaji wa nidhamu. Mhe. Spika, sisi sote tunaamini kwamba kuna Mungu na ukimkosea atakuadhibu wakati fulani. Wale waliokosewa sasa hivi, kuna malipo yanayoendelea. Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba ukifa mali yako haitaenda kwa watoto wako bali kwa ndugu yako na bibi yake na ...
view
15 Oct 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Kwanza, ninamsifu dada yetu, Fatuma Dullo, Seneta wa Isiolo, kwa kuleta malalamishi kama haya mbele ya Bunge la Seneti. Ni jambo la kusikitisha sana kuona gavana aliyeitwa kwa Bunge la Seneti aje ama gavana ameitwa na Kamati ya Seneti ajitokeze na akose kuitika. Ni jambo pia la kusikitisha kwamba, yeye kama kiongozi wa gatuzi la Isiolo, ni lazima azingatie sheria na ajue kwamba, Bunge la Seneti ndio linalomshugulikia na kumtafutia pesa ili atumie na kufanya maendeleo ndani ya Isiolo. Ule uamuzi, Bw. Spika, umeutoa hivi sasa kwamba yeye aitwe tena mbele ya Kamati, kupitia kwa Jenerali Mkuu ...
view
15 Oct 2024 in Senate:
gatuzi la watu wa Isiolo na akiitwa na Isiolo au Kamati ya Seneti, ni lazima afike hapo. Asipofanya hivyo, hatua itachukuliwa.
view
14 Oct 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Kwa sasa, watu wa Kaunti ya Kericho wanajua ya kwamba kesi yao sasa hivi iko kwa Seneti. Hoja iliyo mbele yetu ni ya kusimamisha kusikilizwa kwa kesi dhidi ya gavana ama kuimaliza wakati huu. Tumekuwa na mifano tofauti tofauti mbele ya Seneti. Kulikuwa na Kesi ya Mhe. Mike Sonko aliyekuwa Gavana wa Jimbo la Nairobi City. Jambo kama hili lilitendeka lakini Seneti iliamua kusikiliza kesi yote kwa ujumla ndiposa iamue. Ninataka tuchukue uamuzi huo huo ambao ulichukuliwa wakati ule na Bunge hili. Bunge hili na Maseneta wengine sio waliokuwako lakini wale ambao wako sasa hivi wanaweza kufanya ...
view
14 Oct 2024 in Senate:
kando kidogo ili tuweze kuichukua pamoja na hizi zingine kama tulivyofanya katika mfano wa kesi ya Mhe. Sonko.
view
14 Oct 2024 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, reading the mood, let me second.
view
9 Oct 2024 in Senate:
Thank you, Mr. Speaker, Sir. I second.
view
2 Oct 2024 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, I rise pursuant to Standing Order No.52(1) to make a Statement on a matter of national general tropical concern, namely, the rise in cases of fraudulent overseas jobs by unscrupulous recruiting and travel agencies in Kenya. Since last year, Kenya has experienced a disturbing increase in job fraud, leaving many desperate job seekers vulnerable to unscrupulous schemes. A particular alarming The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate.
view