19 Nov 2024 in Senate:
Madam Temporary Speaker, I beg to second.
view
13 Nov 2024 in Senate:
Asante Bw. Naibu Spika. Ni jambo la kusikitisha kuona kila kuchao, tukiwaita Mawaziri ambao wanatakikana kuja kuwajulisha wananchi wa Kenya na kujibu maswali ambayo yana umuhimu katika taifa la Kenya, hususan, upande wa afya, kunakuwa na upotevu wa kuja katika Bunge la Seneti kueleza Wakenya ni shida gani iliyoko. Mara nyingi, kumekuwa na vifo vya wagonjwa na ukosefu wa insurance wanaosema wananchi wanapata, ila wakifika hospitali wanajereshwa. Ni muhimu ikiwa Mawaziri hao wanaweza kujitokeza na kujibu haya maswali. Bw, Naibu Spika, la mwisho ni kwamba, itakuwa aibu na kusikitisha, ikiwa Waziri ameitwa kuja kujibu maswali katika Seneti na akose kuja. ...
view
30 Oct 2024 in Senate:
Starehe and Kianda are big schools in Nairobi City County. I would like to welcome them to Senate. However, we have the distinguished Senator for Nairobi, my brother, Sen. Sifuna. I would like to give this opportunity to Sen. Sifuna to do the welcoming remarks.
view
30 Oct 2024 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, I second.
view
30 Oct 2024 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda. Kwanza, ningependa kutoa rambi rambi zangu kwa familia, jamii na marafiki wote wa hizi familia ambazo zimeathirika kwa wapendwa wao kuuwawa katika hali ya kinyama na sintofahamu. Pia, ninatoa heko kwa ndugu yangu na mdogo wangu, Eddy, kwa kuwasilisha Hoja hii ambayo imeleta msisimko mpya ndani ya Bunge letu la Seneti. Tumeona Wakenya wanauwawa kiholelaholela na bila sheria na bila hatua yeyote kuchukuliwa na polisi. Kitu cha kwanza ningependa kutafakari vizuri ni kwamba, kuua watoto wadogo, tena watoto wa kike; watu ambao hawezi hata kupigana ama kujiregeshea ngumi au kusukuma mtu. Wewe unaenda unapata watoto ...
view
30 Oct 2024 in Senate:
Tunawaona tu wakati wanataka kututupia teargas, mimi nikiwa na Sen. Sifuna. Tunawaona tu wakati wanataka kuonyesha sehemu zetu za siri kwa magazeti
view
30 Oct 2024 in Senate:
Hawana maana. Washindwe kabisa! Bi. Spika wa Muda, ni jambo la kusikitisha. Si jambo la kucheka. Mtu kama Willies Ayieko, alikuwa anafanya kazi kwa Wells Fargo.
view
30 Oct 2024 in Senate:
Sen. Sifuna anasema amebeba. Sikuona mimi. Nasema tu ya kwamba ni jambo la kusikitisha hivi leo ikiwa mtu mzima kama yule, aliyekuwa hana ubaya na mtu anaweza kupoteza maisha yake kiholela namna ile halafu anatolewa macho. Hata kama ni uhalifu, umefikaje kiwango hiki? Mwisho, huyu Inspector-General wa Polisi, Bw. Kanja, tuliyemchagua hivi majuzi, ninataka kumwambia aamke kutoka kwa huo usingizi; aamrishe askari wake wafike kila mahali. Vile vile, vitengo vingine vya uchunguzi kama vile Kitengo cha Ujasusi wawape wananchi ripoti za ujasusi na hatua zilizochukuliwa. Tunakemea sana. Lazima hatua kali zichukuliwe dhidi ya wahalifu hao. Hoja hii ambayo imeletwa na ...
view
27 Oct 2024 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, ndugu yangu anayetoa maoni yake kuhusu ripoti yetu ya Kamati ya Usuluhishi amesema kwamba pengine mwenzetu haelewi lugha ya Kiingereza anayoitumia. Namuuliza, je, ni haki kwamba hasemi kwa uwazi? Sen. Munyi Mundigi hujiita daktari. Kama daktari anafahamu lugha ya Kiingereza sana. Nishamsikia akiongea lugha ya Kiingereza. Je, ni haki ndugu yangu ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Barabara na Usafiri kusema kwamba Sen. Mundigi ana upungufu wa kufahamu lugha ya Kiingereza? Asante, Bw. Spika wa Muda.
view
27 Oct 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda. Kwanza, ninataka kuwapa kongole wale Maseneta wetu hususan katika Seneti. Haya The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate.
view