19 Aug 2024 in Senate:
Ni jambo muhimu kuzingatia ya kwamba mambo yaliyo mbele yetu ni mambo ya kitaifa. Kwa sasa tuko hapa kwa sababu ya jambo hili la gavana kuwachishwa kazi. Ni jukumu letu kuchukua hatua ya kufanya uamuzi dhidi ya hii kesi ya gavana Kawira. Itakuwa vyema ikiwa tutaweza kugeuza kalenda ili tuwapatie nafasi Maseneta ambao wamekuja, wako hapa, waweze kurudi na kushughulikia wananchi mashinani. Naunga Hoja hii mkono.
view
19 Aug 2024 in Senate:
Can the Counsel go slowly? We are trying to catch up with these volumes as he keeps on leading the witness. We are also recording.
view
19 Aug 2024 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda. Nilikua nataka kujua jina la yule alikua akiongea.
view
14 Aug 2024 in Senate:
Asante Bw. Spika. Jina langu ni Stewart Madzayo, si kama alivyosema ndugu yangu. Amesema Mathayo kwa sababu ile “d” na “z” ameweka “t” na “h”. Ni sawa kwa matamshi ila amekosea kidogo kwa jina lenyewe. Bw. Spika, cha kwanza ninachotaka kuunga mkono ni kwamba twende kwa njia ile---
view
14 Aug 2024 in Senate:
Twende kwa njia ya kamati kwa sababu njia ya kamati au ile njia ya Bunge lote kuhusishwa, uamuzi huo utafanywa na Maseneta. Kila Seneta hapa ana usemi wake. Kuna tetesi tofauti lakini tukiwa kama The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate.
view
14 Aug 2024 in Senate:
Maseneta, ni lazima tuweze kuamua ikiwa tunataka kwenda ile njia ya kamati au Seneti nzima ambapo Maseneta wote wanachangia katika Hoja hii iliyo mbele yetu. Najua Bunge la Seneti linajulikana kwamba lipo na Maseneta majabali, maseneta ambao wanaweza kuketi wakasikiza kesi na kukata kisawasawa. Sintofahamu ni kwamba pengine kukatokea cheche za maneno kutoka nje na kunakuwa na lawama tofauti tofauti kulinganishana na Maseneta wetu. Hizo huwa ni cheche tu. Tunaelewa kwamba cheche zingine ni kama maji moto, haiwezi kuchoma nyumba. Kwa hivyo, hawawezi kutuambia maneno yanayowezafanya tukose mwelekeo na pengine tusikate kesi kulingana na zile stakabadhi zilizowekwa hapa mbele; stakabadhi ...
view
25 Jul 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika, Seneta Osotsi ni rafiki na ndugu yangu na tunasikizana sana. Hoja yangu ya nidhamu ni kwamba, ifikapo mambo na sheria za Bunge, hawezi kumtaja mtu ambaye hakuitwa na Bunge ama, hakujakuwa na taarifa fulani kwamba aje na hakuja, halafu yeye anamtaja kwa njia ambayo si ya kisawasawa. Mimi nauliza kama ni haki kumtaja mtu kabla hajaitwa katika Bunge kwa njia mbaya na hajapata nafasi ya kujitetea?
view
24 Jul 2024 in Senate:
Thank you, Mr. Speaker, Sir. First and foremost, I would like to react by saying that the amendments that we have decided to put in place in this Motion are viable and can be handled. As regards the positions of the principal secretaries, what we are saying is that the Committee on Justice, Legal Affairs and Human Rights has done these amendments, which we believe will go a long way to help the vision of what the Senator would wish to achieve. Mr. Speaker, Sir, moving on to further amendments that have been of equal opportunity to all Kenyans, we ...
view
24 Jul 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda. Kwanza, ningependa kumpatia kongole ndugu yetu, Sen. Abass, kwa kutengeneza sheria ambayo ni ya kuzima moto na kuokoa watu wakati wa janga la moto. Sheria hii inaleta mwelekeo mpya. Tumekuwa kwa muda mrefu na nafasi ambazo hazingeweza kukamilika kutengenezwa kwa sheria ambayo itahusikana sana na uzimaji wa moto. Kama tunavyoelewa, kazi ya kuzima moto hivi sasa inafanywa na magavana wa kaunti. Lakini kuna kasoro, ikiwa nitakosoa kidogo, upande wa magavana wetu wanaohusika na kuangalia jukumu hili muhimu sana. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this ...
view