24 Sep 2024 in Senate:
Hii ni kwamba sasa, hata kwa familia kama mtu mmoja alikuwa haendi shule, basi watoto wengine pia watafuata hiyo kauli. Hii ni kwa sababu hakuna pesa katika familia na lazima wao pia wakae nyumbani wasiende shule.
view
24 Sep 2024 in Senate:
Jambo ambalo nataka kusisitiza zaidi ni kwamba tusirudi nyuma. Tuangalie safari ya kuenda mbele. Tabia hii ya kuletewa Mswada na wale wenzetu na kusema kwamba The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate.
view
24 Sep 2024 in Senate:
tumepitisha pesa za juu, sisi tumesema tunataka shilingi bilioni 400 ziende katika serikali za ugatuzi. Naunga mkono kamati yetu iliyofanya kazi njema. Nawatakia kila la heri waweze kusimama kidete pale pale waliposimama.
view
19 Sep 2024 in Senate:
Asante Bw. Naibu Spika. Kwanza, ni jambo la kusikitisha ikiwa utatoa taarifa ambayo haina ushahidi wowote kutumia jina la mtu mwengine ambaye hakupewa taarifa yoyote. Kama ingewezekana, pia yeye angeitwa kwa televisheni wakajibizana ili ijulikane nani ni mkweli au muongo. Lakini si vizuri kuchukua upande mmoja kutoa taarifa ya kushambulia upande mwengine. Watu wengine na wengi wetu tuliopo hapa kama ndugu yangu, Sen. Kinyua, ni mtu aliyetengeneza jina lake kule Laikipia kwa miaka mingi mpaka sasa amekuwa Seneta. Bw. Naibu Spika, pia wewe kule Meru, umetengeneza jina lako kamili, kwa hiyo itakuwa ni makosa mtu akitaja jina lako kwa ubaya ...
view
19 Sep 2024 in Senate:
Ndio, niko barabarani kuelekea huko. Barabara ni ndefu sana. Tunalaani vikali kitendo kilichotendeka kwa taarifa ya habari. Nikirudi upande ule mwengine, ni jambo la kusikitisha vile vile kuona kwamba Kenya hii kuna watu wanaovaa magwanda ya kuficha sura na hatujui kama ni polisi ama majambazi. Kwa mfano, leo utapata mtu anakuja nyumbani kwako na humjui ni nani, na unapotoka kwa gari lako, anakuvamia na unatoweka. Tuliona kitendo hicho wakati Mhe. Alfred Keter alishikwa na polisi. Alishikwa akiwa barabarani wakati yeye ni mheshimiwa. Si jambo nzuri kwa Mkenya kushikwa kiholela akiwa Kenya. Nikija upande wa dada yangu, watu wake watatu wameshikwa ...
view
19 Sep 2024 in Senate:
Jambo la kusikitisha zaidi, watoto wa kiislamu---
view
19 Sep 2024 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate.
view
19 Sep 2024 in Senate:
Jambo la kusikitisha zaidi, watoto wa kiislamu wanashikwa kila uchao na baadaye hawapatikani, ama wapatikane wamekufa ama wasiachiliwe. Tunataka jambo hili likome. Polisi wakishika mtu, wampeleke kortini na kumshataki ili afungwe kisheria. Wakifanya hivyo, jamii yake itaamua kama itamuwekea mawakili ama itamsaidia namna gani ili arudi nyumbani. Asante Bw. Naibu Spika.
view
18 Sep 2024 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika. Ningetaka kumuuliza Waziri kama anaelewa kwamba wote waliopata majeraha na kuumia wakati wa kile kitendo cha ugaidi kwenye nyumba ya ubalozi wa Marekani walikuwa Wakenya na wananchi ya Kiamerika. Je, Waziri ana habari kuwa wananchi wote wa Amerika walilipwa fidia, majeraha yao kuhudumiwa hospitalini na kuwa walitunzwa vizuri na nchi yao? Kwanza---
view