Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 61 to 70 of 2266.

  • 12 Feb 2025 in Senate: Asante Bw. Spika wa Muda. Ilikuwa ni mtihani mkubwa sana kufikia hapa ambapo tumefikia kwa sababu kuchagua maseneta na kuwaweka katika kamati hizi zilizoko ndani ya Seneti sio kazi rahisi. Kwa upande wa maseneta walio wachache tumejaribu iwezekanavyo kuona ya kwamba kila tuliyemchagua ni seneta mkakamavu katika kitengo ambacho tumempatia. Mimi ninaunga mkono na kusema kwamba Maseneta hawa wote ambao wamewekwa katika Taarifa hii ya leo wana ujuzi, taaluma, akili na uwezo wa kutekeleza wajibu wa majukumu ambayo tumewapatia. Vile tumewachagua hawa Maseneta ambao watakuwa katika kamati hizi sio kazi rahisi. Mara nyingi tunaona kamati nyingi kwa mfano ule wakati ... view
  • 12 Feb 2025 in Senate: Asante Mstahiki Spika wa Muda. Naanza kwa kuunga mkono wale wote waliochaguliwa hapa katika hizi Kamati zote tatu. Kamati hizi ni nguzo ya Seneti kwasababu ni Kamati ambazo ziko na majukumu ya hali ya juu hususan mambo ya utekelezaji wa pesa na matumizi na pia kuchunguza kama hizo pesa tunazopeleka mashinani zinatumika vyema. Kwa hivyo, tukiwa tunajidai na hizi Kamati, ni kwamba tuko na imani ya kwamba zitatekeleza wajibu wake. Hao waliochaguliwa hapa wote katika hizi Kamati ni wakakamavu. Niko na imani ya kwamba watatimiza vile inavyotakikana kufanywa hasa matumizi ya pesa katika kaunti. Asante. Ninaunga mkono. view
  • 11 Feb 2025 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika. Kwanza ninakubaliana na majina yaliyoko hapa, ya Maseneta ambao wataketi katika kamati inayoongoza Bunge katika itifaki zake. Waliochaguliwa hapa ni Maseneta walio na ukakamavu wa mambo ya Seneti. Tuna imani ya kwamba hawa waliochaguliwa wataweza kutimiza ile hadhi ambayo wamepewa. Nikiendelea kuunga mkono majina haya saba, ningependa kutangazia ndungu zangu ya kwamba ni jambo ya kusikitisha ninaposimama na kutangaza kifo kilichotokea cha babake Spika wetu wa Seneti, Hon. Amason Kingi. Kifo hicho kilitokea jana wakati madaktari walipokuwa wakiendelea kumpatia matibabu mzee wetu. Ijapokuwa sisi tulimpenda, Mwenyezi Mungu alimpenda zaidi. The electronic version of the Senate Hansard ... view
  • 11 Feb 2025 in Senate: Ningependa tu kuwajulisha ndugu zangu kwamba tutaweka kwenye mitandao. Mimi nilikuwa wa kwanza kuwajulisha Maseneta na kuwaambia kuwa kifo cha mzee kimetokea. Hayo yote yaliyotendeka ni mambo ya Mwenyezi Mungu. Tutaendelea kushirikiana na familia ya Spika na ndugu zangu. Mjuavyo, kifo kama hicho sio cha kawaida; ni kifo cha babake Spika wetu na ninajua sisi sote tutajumuika naye. Mimi ninaweza kutangulia nyumbani lakini watakaobaki nyuma mtaendelea kuweka nguvu za Seneti hapo mbele. Jambo la wisho, ingekuwa bora zaidi ikiwa utafafanua hili jambo. Katika ratiba hii ambayo tunasema kuwa sisi tuko katika Broad-based Government na tukijua ya kwamba mahakama ilitoa uamuzi--- ... view
  • 3 Dec 2024 in Senate: Thank you, Mr. Speaker, Sir. I would like to join you in welcoming the delegation from Namibia. I hope their stay here has been very fruitful and that they have managed to learn a lot from our members of staff with regards to how we operate here as a Parliament. At the same time, I hope they have been able to enjoy themselves in the course of their stay here. Additionally, when they go back home, I am sure they will have learnt one or two things from us. I also believe they have shared their experience from Namibia to ... view
  • 3 Dec 2024 in Senate: Bw. Spika, ningependa kuzungumza kuhusu taarifa aliyoleta Sen. Faki. Watu wanaofanya kazi kwa miaka mingi hawalipwi mapato waliokuwa wakiweka baada ya kustaafu. Mara nyingi tunaona watu waliokuwa katika mamlaka wakiishi maisha ya uchochole baada ya kustaafu. Wanaishi maisha mabaya kana kwamba hawakuwa na heshima wakati walipokuwa wakifanya kazi. Haya yote yanachangiwa na taasisi zinazoweka mapato ya wafanyikazi. Wanawafanyia madharau kwa sababu wanachukua pesa hizo na kufanyia kazi zingine. Sasa imekuwa kama mchezo. Kila mtu anayefanya kazi nchini Kenya hana uhakika kwamba pesa ambazo amekuwa akikikatwa ili kuwekwa kwenye hazina zitamfaidi wakati amestaafu na kumhakikisha maisha mema. Langu ni kwa wale ... view
  • 26 Nov 2024 in Senate: I second. view
  • 26 Nov 2024 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda. Hoja yangu ya nidhamu ni kwamba, ameongea juu ya Sen. Maanzo na si vizuri kuharibiana majina ndani ya Mbunge saa zingine na Wakenya wote wanaangalia. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate. view
  • 26 Nov 2024 in Senate: Heshima lazima tuiweke mbele, tusiketi hapa na kuanza kusema maneno ambayo baadaye yataleta kashfa, nikizingatia kwamba, ndugu yangu Sen. Maanzo kila asubuhi yuko kwenye maruninga. Kwa hivyo, itakua si heshima kwa jina lake kuharibiwa namna hiyo. Nataka kuuliza tu, alisema kwamba anataka kutoboa siri kuwa Sen. Maanzo alienda kumuona Waziri. Ana maanisha nini? Je, anaweza kufafanua? view
  • 26 Nov 2024 in Senate: Asante sana Bw. Spika wa Muda. Kwanza, nampa kongole Rais kwa kutoa Hotuba yake ya hali halisi ya nchi ya Kenya ya mwaka huu. Sikudhani angefanya hivyo kwa sababu siku zilikuwa zimeyoyoma na mwaka unaenda kuisha. Kalenda ya Bunge ilikuwa imefika mwisho, kwani tumebaki na siku saba ili Bunge liende kwa likizo. Lakini ni vyema alikuja kutoa Hotuba ya hali halisi ya Taifa ya mwaka wa 2024. Kitu cha muhimu katika Hotuba ya Rais ni kugusia mambo mbalimbali ya muhimu ambayo wananchi wa Kenya wangependa kusikia na kuona suluhisho limepatikana. Bw. Spika wa Muda, katika Hotuba ambayo Rais alitoa, hakuweza ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus