Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 41 to 50 of 2202.

  • 26 Sep 2024 in Senate: Asante, Bw. Spika. Tuko na wageni kutoka nchi mbalimbali za Bara letu la Afrika. Kuna watu kutoka nchi ambazo zinaongea Kiingereza, wengine wanaongea Kifaransa na pia Kiswahili, kwa upande wa watu wa Congo Brazzaville. Kwa ujumla, ni bora uniruhusu niongee kwa lugha ya Kiswahili. Kwanza, najiunga na wewe kuwakaribisha hawa wageni wetu kutoka Makueni kwa ndugu yangu, Sen. Maanzo, na vilevile wale kutoka Bara la Afrika wa ile Kamati ya Tabia Nchi. Tunaona Afrika sasa inakuwa kitu kimoja. Ni muhimu kuwa tunalinda mazingira yetu. Tunawaunga mkono kwa safari yao ya kutoka nchi zao za mbalimbali za Afrika. Wamekuja hapa kujionea ... view
  • 26 Sep 2024 in Senate: Bw. Spika, mwisho, ningependa kuwaambia hawa ndugu zetu ambao wametoka Bara nzima la Afrika, karibuni sana katika Bunge letu la Seneti. Najua mkifika nyumbani, mtawajulisha ndugu zetu vile mmeona kazi ikiendelea katika Seneti ya Kenya. Karibuni Kenya, ni nchi iko huru. Mnaweza kuzunguka mpaka saa kumi au saa tisa. Kuna mahali kwingi pa kwenda hapa Nairobi. Nairobi ni kwenu. Jisikieni kabisa kwamba mkiwa Kenya, ni kama mko nyumbani katika nchi zenu tofauti tofauti za Afrika. Asante, Bw. Spika. view
  • 26 Sep 2024 in Senate: Asante, Bw. Spika. Najiunga na wewe kumkaribisha dada na mtoto wetu kutoka Kaunti ya Kilifi na pia Mkenya. Ni Mkenya kwa sababu ametoka katika nchi yetu na amefanya mengi ya ajabu katika Kenya. Natoa kongole kubwa kwa Bi. Akida kutoka Kilifi. Wanawake wengi katika ulimwengu wanacheza kadanda lakini wengi wao hawatafika kile kiwango chake. Huyu dada - Ms. Esse Akida - amefanya bidii, akatia juhudi na kushughulika sana kufanya mazoezi na kuangalia taaluma mbalimbali za wale walio mbele yake ili kujifunza na hatimaye akafika kile kiwango cha kucheza kadanda ya kulipwa katika nyadhifa za juu za nchi za ng’ambo. Bw. ... view
  • 26 Sep 2024 in Senate: Yes, Asante. Siyo rahisi kwa msichana mdogo kama huyu kutia juhudi na kufika kile kiwango. Katika harakati zake amepatana na pingamizi nyingi. Tumesoma katika vitabu kuwa ikiwa wewe ni mchezaji pengine una watu wanaokufunza au kukusaidia. Kumekuwa na chnagamoto nyingi katika maisha yake lakini ameweza kuzivuka na ameandika kitabu. Katika kitabu chake anasema kuwa ni kama alikuwa amefungwa minyororo lakini sasa amejifungua na anaweza kwenda kwa sababu yale mawingu hayatakuwa ya mwisho. Huenda akayavuka pia na kuingia katika ulimwengu mwingine wa uchezaji kadanda. Sisi tunamtakia kila la heri. Nawaomba Masenata na dada zangu hapa katika Bunge hususan dada yangu pale ... view
  • 26 Sep 2024 in Senate: Sisi kama Maseneta tunafaa kukisoma kitabu hicho. Niko na copies kwa bei nafuu. Unaeza kuja katika ofisi yangu na nitamwelekeza Sen. Cherarkey apatie kila mtu. Asante. view
  • 24 Sep 2024 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia suala la ugavi wa pesa zitakazokwenda katika serikali za kaunti 47 katika nchi yetu ya Kenya. Jambo la kusikitisha ni kwamba hapo awali, tulikuwa tumekubali kwamba kiwango tulichokuwa tumeweka cha shilingi bilioni 415 kingetosha vizuri. Bw. Spika wa Muda, sisi tukakubaliana ya kwamba irejeshwe chini mpaka ifike shilingi bilioni 400. Limekuwa ni jambo la kusikitisha kuona ya kwamba kuna marekebisho zaidi ya kurudisha chini mpaka shilingi bilioni 350. Nguzo za uchumi wa nchi yetu ya Kenya zinategemea serikali zetu za ugatuzi. Kwa sababu katika miaka mingi, tumekuwa katika Serikali ya ... view
  • 24 Sep 2024 in Senate: barabara, shule za chekechea na maendeleo kadha wa kadha wanayotakikana waendelee nayo. Ni sisi tunaoelewa shida ambayo zinakuba serikali za ugatuzi na kazi zetu tulizonazo hapa. Ikiwa nitakupa taarifa, niruhusu niseme kwamba Kipengele cha 96, sheria ya kwanza, inasema kuwa kazi kubwa ya Seneta ni kuwakilisha kaunti na pia kuleta mahitaji ya kaunti ya ugatuzi na kulinda maslahi hayo. Hii ni kazi ambayo inahitaji uangalifu na udhalilifu wa hali ya juu sana kuona ya kwamba mahitaji haya yameweza kupatikana. Lakini cha muhimu zaidi kulingana na Mswada huu ambao upo mbele yetu, ni Kipengele cha 96(5) ambacho kinaongea juu ya taratibu ... view
  • 24 Sep 2024 in Senate: Jambo la kusikitisha ni kwamba ikiwa huu Mswada utapitishwa vile ulivyo na tunawatuma hawa wenzetu ambao watatuwakilisha pale katika majadiliano haya, kuona ya kwamba wamesita, wameweka miguu yao kisawasawa kwa kusimama kidete na wasikubali hizi pesa ziweze kupunguzwa. Zikipuunguzwa, hatari itakuwa kwa watu waliochaguliwa kama Maseneta hapa kwa sababu wana swali la kujibu kule wanapotoka katika serikali za ugatuzi. view
  • 24 Sep 2024 in Senate: Bw. Spika wa Muda, nataka kumalizia nikisema kwamba shida za serikali za ugatuzi ni nyingi sana. Hivi sasa tunaona ya kwamba hata mishahara katika serikali za ugatuzi haijalipwa. Watu kule pia kama vile wafanyakazi wana haja za kulipa na kuna mengi ambayo wanatakikana kufanya kama wafanyakazi. Majukumu yote yanafanywa na serikali za ugatuzi. Kulipwa mishahara ni haki ya wafanyakazi. view
  • 24 Sep 2024 in Senate: Hivi sasa utaona wako wasichana na wavulana ambao wameachishwa shule. Wengine wameshidwa kuenda vyuo vikuu kwa sababu baba zao bado hawajalipwa pesa. Ikiwa sasa hawajalipwa, itakuwaje sasa ikiwa hizi pesa zitapunguzwa? view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus