Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1001 to 1010 of 2266.

  • 9 Nov 2021 in Senate: nilipomaliza unanasheria yeye ndiye alikuwa tajiri wangu wa kwanza kuniajiri kama view
  • 9 Nov 2021 in Senate: Ningekuwa mtu wa mwisho kabisa kusimama na kuuliza swali hili na kujaribu kumrekebisha. Ninajua anaelewa ni ulimi unateleza lakini mara anakupatia wewe majina mawili la kiume na la kike halafu la kazi unayofanya. Hatujui katika hayo matatu, madam na Spika ni sawa lakini kuna hilo lingine alilokuita si mara moja, mbili, tatu au nne. Pengine ingekuwa vizuri afafanue. view
  • 9 Nov 2021 in Senate: Ahsante, Bi. Spika wa Muda. Kwanza, ningependa kumshukuru ndugu yetu Okong’o Omogeni, wakili mashuhuri sana katika Jamhuri ya Kenya yeye akiwa mwenyekiti wa kamati yetu ya Sheria na Haki za Binadamu kwa kuleta ripoti hii. view
  • 9 Nov 2021 in Senate: Kila alivyo nakili katika hii ripoti, yamewahi kutokea katika Kenya, hususan katika mkoa wa Pwani. Tunajua kabisa katika sheria na Katiba inasema ya kwamba, kila mtu katika Jamhuri ya Kenya ana haki ya kuishi na kuweza kulindwa kimaisha na Serikali. Lakini yale yanayojiri tunayaona ni mambo ya kustaajabisha. view
  • 9 Nov 2021 in Senate: Bi. Spika wa Muda, tunavyoongea kuhusika na vifo hivi, nasikitika kwa sababu mimi mwenyewe katika familia, tumepatikana na kisa kama hiki. Pia vilevile, visa vya wavulana katika Pwani vimekithiri. Ukweli wa mambo ni kwamba, visa kama hivi view
  • 9 Nov 2021 in Senate: vinafanywa na polisi. Ningependelea kusema ya kwamba, ni vyema ikiwa polisi wataambiwa kwamba mambo ya kupiga watu risasi, kuua watu au kuangamiza wananchi yakome. Yasiweze kutokea tena katika maeneo yetu ya Pwani. view
  • 9 Nov 2021 in Senate: Ni jambo la kusikitisha hivi leo ikiwa tutaketi hapa na tutaongea jinsi vile watu wanapotea na wanauwawa na polisi. Jambo kubwa la kusikitisha ni ukisikia polisi wameenda mahali kuondoa wananchi na wako na court order, saa zingine hio court order inaeza kua ni bandia. Tena utapata ukisikia polisi wameenda mahali na wanaketi kwa muda mrefu kuondoa ni kwa sababu kuna bwenyenye, atawapa pesa na wataenda hapo kufurukisha watu ambao wapo katika mashamba yao. Watu wengine wameishi hapo kwa zaidi ya miaka sabini au themanini, maanake miti yetu inasema. Mnazi ukikua mpaka ukifa, inakua ni zaidi ya miaka sabini. Utaona polisi ... view
  • 9 Nov 2021 in Senate: Stewart Madzayo. Ama iwe kuna George. Kwanini saa zote iwe Rashid, iwe Feisal, iwe Abdullahi au Salim? Tunajiuliza maswali. Ni kwa sababu, katika akili za polisi, mtu akiwa amekua barobaro na kuna makosa fulani yametendeka katika mtaa fulani, inajulikana wale wanaweza kuwa rounded up au kuzungukiwa wakashikwa, ni wale wavulana Waislamu. Kubagua hakufai. Laziwa watu wote wawekwe katika sheria kisawasawa. Familia hizi zinateseka kiuchumi kwa sababu yule ambaye anapeleka mkate nyumbani, yule mtu anayeweza kupeleka mamake hospitali na yule mtu anayeweza kusomesha mtoto wake; anakua anapotezwa hali si sawa kupitia kitengo ambacho si cha kisheria. Bi. Spika wa Muda, ile ... view
  • 9 Nov 2021 in Senate: , ilikua na ripoti nzuri sana. Ilieleza chanzo cha polisi kutumia nguvu, chanzo cha watu wa Pwani kupoteza mashamba yao na chanzo cha vile mashamba yalinyakuliwa. Hili jopo liliandika ripoti. Bi. Spika wa Muda, ni miaka mingi sana, zaidi ya miaka kumi sasa tokea hii ripoti ya Truth and Justice Reconciliation Committee ambayo ni Ukweli na Sheria na Uridhiano, na haijatolewa mpaka hivi leo. Ripoti hii ilikua hususan inaongea mambo ya Pwani. Watu ambao waliweza kupata uhuru tokea kitambo lakini watu wa Pwani hawakupata uhuru wao mpaka mwisho ikifikia mwaka wa elfu moja mia tisa sitini na tatu; Kenya ikipata ... view
  • 9 Nov 2021 in Senate: kuna mtu mzima mmoja kwa jina Mzee Abubakar. Alisingiziwa kuwa yeye ni jambazi. Hatimaye aliweza kuwekwa ndani. Badala ya kupelekwa polisi, sasa amepotea na hatujui aliko. Vile vile, hatuwezi kusahau. Kuna watu ambao wamepitia mkono wa polisi ambao hawakupelekwa kortini. Ukiangalia kule nyumbani, kama Mombasa, kuna mwalimu wa dini kwa jina Makaburi. Aliambiwa kwamba anafundisha watoto jinsia mbaya. Lakini hakuna hata siku moja tuliona Makaburi amepelekwa kortini na akaambiwa hivi ndivyo alivyo fanya na kwamba sio haki na akafungwa. Bi Spika wa Muda, bali tuliona Makaburi akipigwa risasi. Alikuwa ameshatabiri kwamba polisi wanamtafuta na watamuua. Mpaka leo, baada ya kusema ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus