2 Dec 2021 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Shukran sana kwa kunipatia nafasi ili nichangie Hotuba Rais alitoa kwa Taifa kuhusu maendeleo ambayo Serikali yake imefanya kufikia hivi sasa na yale matarajio ambayo anafikiria anaweza kuyafanya kwa hii miezi tisa au kumi iliyobaki kama Rais wa Jamhuri ya Kenya. Hatuwezi kusema kwamba asilimia, Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Muigai Kenyatta amefaulu. Hapana! Yeye kama kiongozi wa kisiasa pia ana makosa yake. Kuna pia unyonge wake mahali fulani. Kwa hivyo, tunasema kwamba alijaribu na hivi sasa amejaribu na atajaribu. Mengine yatakuwa mazuri na mengine hayatafaa. Jambo la kwanza ambalo ningependa kuongea juu yake ni kwamba ...
view
2 Dec 2021 in Senate:
tunasema kwamba angeweka mkazo zaidi ya kwamba wale vijana wa Lamu ambao tangu tupate uhuru mpaka hivi sasa, kusema ukweli ni kwamba, wengi wa vijana wa Lamu hawajapata ajira. Nafasi ile ya Lamu Port, yeye kama Rais angeweza kutoa ishara ikiwa kama kuna kazi zozote kama za mikono ama za aina yoyote, zile ambazo si lazima watu waende skuli wapate, zingepewa vijana wa kutoka eneo lile la Lamu na pia kuona kwamba ikiwa zingine zitapatikana, basi zipewe Wakenya na hususan watu wanaotoka katika maeneo ya pwani. Vilevile biashara zinazotendeka katika maeneo yale ya kule Port, nafasi hizo zipewe wale watu ...
view
2 Dec 2021 in Senate:
Jambo la kusikitisha ni kwamba wakishikwa, hawapelekwi kotini, wanauawa kiholela. Baadaye tunapata familia zinalia na hatuelezwi ni sababu gani familia zimekosa watu ndani ya nyumba. Tukiangalia kwa kina, tunaona kwamba wengi wamepoteza maisha yao katika mikono ya polisi. Kila mara tunaambiwa waliouawa walikuwa wanaume au wavulana ambao walikuwa wanaenda kujiunga na kikundi haramu cha Al Shabaab. Bw. Spika, lazima tuzingatie sheria zetu za Kenya. Mtu amaposhikwa na polisi ni sharti apelekwe ndani ya korti. Rais wetu hakuweza kutamka mikakati ambayo ameweka kisawa sawa ya kwamba ataongea na Wizara ambayo inahuska, ili kutetea maisha ya hawa vijana ambao huwa wanapotea kutoka ...
view
2 Dec 2021 in Senate:
Sijui ni kwa nini mpaka sasa wale walioiiba pesa za Covid-19 mpaka sasa hawajachukuliwa hatua. Hili Bunge lilileta ripoti yake. Ripoti ikapelekwa namna hii namna hii ikawa vile ilivyokua lakini kuna ushahidi wazi kabisa ya kwamba pesa za Covid-19 ziliibiwa. Walioiba wanajulikana wazi kabisa. Nampa kongole dadangu Senata Dullo na kamati yake maalum. Waliandika ripoti nzuri sana lakini ile ripoti yake mpaka hivi sasa hatua haijachukuliwa. Janga la ufisadi sio ya pesa za Covid-19 peke yake, katika kila sekta ya Serikali, kuna ufisadi. Hatua ambayo Rais angechukua hivi sasa ni kuweka mpango mbadala ili nchi hii iwe huru na ufisadi. ...
view
2 Dec 2021 in Senate:
Bw. Spika, tunasema ya kwamba, Hotuba yake ilikuwa kidogo iliweza kuweka mwelekeo, lakini kuna maeneo fulani ambayo itatakikana aweze kuyajaza yale matundu. Lakini jambo la mwisho ni kwamba, yeye mwenyewe alisema ya kwamba, sisi kama Wakenya wakati atakapoenda, tuhakikishe ya kwamba, Rais wa Jamhuri ya Kenya wa tano atakayekuja ataweza kumaliza mambo haya na anayeweza kumaliza mambo si mwingine bali ni baba Raila Amollo Odinga. Kwa hivyo, sisi tunasema ya kwamba, ikiwa yeye atakuwa, tuna imani ya kwamba ufisadi utaisha na kutakuwa na uchumi samawati. Kila kitu kitaelekea kisawa sawa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for ...
view
1 Dec 2021 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda. Pia mimi nataka niungane na wewe kwa kuwakaribisha wageni kutoka upande wa Narok, na kusema kwamba, wote waliokuja kujifundisha hapa na kujionea yanayoendelea hapa ndani ya Bunge la Seneti ni mambo ambayo ninauhakika wakati wowote wakirudi nyumbani wataweza kutafakari na kujua ya kwamba waliweza kupata faida ya kuja kutembelea Seneti. Ni jambo nzuri kuona watu kutoka Narok wamefika hapa leao. Wakati mwingi ni watu wa Nairobi ambao huja hapa. Watu wa kutoka kaunti kama ya Narok, Kilifi na kwingine, ni nadra kwao kupati nafasi kama hii ya kuja kutembelea Bunge la Seneti. Kwa vile ndugu ...
view
1 Dec 2021 in Senate:
Asante, Bi Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Ni jambo la kusikitisha sana katika hii Petition ambayo imeletwa hapa katika hili Bunge la Seneti. Nawapa kongole wale waliokuwa na imani na nguvu ya kuona ya kwamba ni lazima jambo hili lifike katika Bunge la Seneti. Seneti itaangalia yale maovu yanayotendwa na Gavana akijifikiria ya kwamba hakuna sheria. Anafikiri yeye ndiye sheria ya mwisho. Kuna sheria na watu wa huko Nyandarua wako na imani nayo. Ni jambo la kusikitisha kuona ya kwamba mtu anaweza kusimamisha kaunti nzima kutoendelea kwa sababu. Ukisimamisha County Assembly ni kama umesimamisha kaunti ya Nyandarua na ...
view
10 Nov 2021 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, I rise pursuant to Standing Order 48(1) to seek a Statement from the Standing Committee on National Security, Defence and Foreign Relations on the Status of compliance to the African Union (AU) legal instruments and policy frameworks.
view
10 Nov 2021 in Senate:
In the Statement, the Committee should-
view