22 Dec 2021 in Senate:
Asante Bi. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, ningependa kuwatolea shukurani sana ndugu zangu Maseneta wenzangu kwa kushughulika sana na shughuli za Bunge. Tumekuwa pamoja mwaka huu mzima; tunashukuru Mungu tumefika mwisho. Tuna jambo la kushukuru sana Mwenyezi Mungu. Pili, ningependa vile vile kuwashukuru sana Maseneta, kwa ukakamavu waliokuwa nao mwaka mzima. Tumeweza kufanya bidii kuhusiana na Bills na Motions . Kuna kazi nyingi sana ambazo tumeendelea nazo, ambazo hata rekodi yake iko na inaweza kuonekana. Kwa hiyo, nataka kuwapatia kongole ya hali ya juu sana Maseneta wote walioko hapa na wale ambao wako katika nyadhifa mbalimbali. Hawakuweza kufika ...
view
22 Dec 2021 in Senate:
Najua umefika hapa kwetu, lakini najua Wakenya ni watu ambao wanaelewa wakiambiwa kitu. Kwa hivyo, jukumu letu kama Seneti ni kuwaambia Wakenya popote walipo wazingatie zile amri za Wizara ya Afya; ya kwamba tuweze kujitenga na kuvaa barakoa wakati tunaongea na wenzetu ili huu ugonjwa usiweze kutapakaa ndani ya nchi yetu ya Kenya. La mwisho kabisa ni kwamba afya njema panapo majaliwa Mwenyezi Mungu atakapopenda tuonane tena - vile hapa katika shughuli zetu za Bunge tunasema “kesho” - tukiwa tutafungua Bunge vyema sote tuwe salama kwa amri yake Mwenyezi Mungu na rehema zake. Asante, Bi. Naibu Spika.
view
22 Dec 2021 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Tulipokua hapa leo mchana, kumetolewa amri na naibu wako. Sio Emeritus Sen. Wako. Nasema naibu wako wewe, Naibu wa Spika wa Bunge la Seneti.
view
22 Dec 2021 in Senate:
Akasema leo, kwa vyovyote vile, liwalo liwe, Maseneta wote ambao wako ndani ya Bunge la Seneti kuagana hapa leo, ikiwa ndio tarehe yetu ya mwisho, wataongea Kiswahili. Je, ni haki? Hata huyu mdogo wangu, ndugu yangu ninayemuenzi sana, Sen. M. Kajwang’ ana Kizungu mufti, lakini leo ameona aongee lugha ya mama.
view
22 Dec 2021 in Senate:
Bw. Spika, nataka nikuulize wewe kwa kauli moja, je, ni haki kwa Naibu wako, ambaye tunamuenzi sana hapa ndani ya Bunge letu, kuvunja amri yake mwenyewe aliyoweka hapa na kila mtu ameifuata?
view
21 Dec 2021 in Senate:
Asante, Bi. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, ningependa kuunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na ndugu yangu ‘ landlord .’ Amegusia mambo ya kuharakisha kuinua uchumi, yaani economic recovery, katika lugha ya Kiingereza. Katika Kaunti ya Kilifi tuko na maeneo ya Export Processing Zones (EPZ). Haya ni maeneo ya biashara za nje. Hivi karibuni, tumeona kwamba kampuni za EPZ zimeingia kwa wingi katika kaunti yetu. Zingine hata ziliwacha kufanya biashara zao katika Kaunti ya Mombasa na kwenda Kilifi. Hii ni kwa sababu ya nafasi ya kufanya biashara hizo na wanaweza kupata afueni ya kulipa kodi. Bi. Naibu Spika, ...
view
21 Dec 2021 in Senate:
wanafanya biashara ndogo ndogo, wamejikakamua sana kufanya hiyo biashara lakini ikifika saa ya malipo inachelewa. Bi. Naibu Spika, sasa utapata kwamba mtu amemaliza karibu mwaka mzima. Anaenda kwa kaunti kila siku akiomba kwamba deni langu katika benki linazidi kupanda na upande huu sasa sijui hata faida hakuna tena, niregesheni ile pesa ambayo nilikopa ili kuwafanyia kazi kama kaunti. Jambo kama hilo ni muhimu lingekuwa hapa na lizingatiwe, kwamba wale wanaofanya biashara na kaunti, wa kwanza walipwe kwanza na watakao kuja baadaye walipwe baadaye, badala ya kufanya mambo ya upendeleo. Tumeona katika Ripoti hii pia kwamba kuna uzembe mwingi sana ndani ...
view
21 Dec 2021 in Senate:
tunatengeneza barabara ya kusaidia watalii. Sisi tumechoka na habari ya kwamba ukifikiria kwenda Mombasa, Kwale, Kilifi, Taita-Taveta, Lamu au Tana River unafikiria utalii. Usisahau kwamba kule kuna binadamu. Maeneo ya Pwani sio ya utalii pekee yake. Pwani sio mbuga za nyika ya kwamba kunaishi wanyama. Bi. Naibu Spika, tunataka heshima ifanywe. Ikiwa wewe unaishi kule Pwani na Serikali imefikiria na kutafakari kutengeneza barabara, watengeneze kwa sababu wanajua kuna wakulima, wafanyibiashara, watu wanaishi kule, kuna shule na kila kitu kiko kule. Lakini tunaona kwamba upande wa barabara Serikali imekaba pesa kidogo kwa sababu ya uhaba wa barabara nzuri kule Pwani. Hivi ...
view