10 Feb 2022 in Senate:
Asante Bw. Spika. Kwanza, ningetaka kuunga mkono huu Mswada wa marekebisho katika unyunyizaji wa maji. Ukulima ni uti wa mgongo wa nchi yetu ya Kenya. Hususan Mswada huu ukiwa unahusika na unyunyizaji wa maji, ni jukumu muhimu sana katika nchi yetu ili kuona kuwa tumeweza kukuza chakula cha kutosha ama mimea ambayo inaweza kuzaa vyakula vya kutosha ili kustahimili Wakenya. Haya ni kwa sababu tunakumbwa na janga la njaa mara kwa mara. Kwa hivyo, hii ni sekta ambayo itawasaidia Wakenya kwa muda mrefu.
view
10 Feb 2022 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
10 Feb 2022 in Senate:
Baa la njaa katika Kenya ni donda sugu ambalo kila mwaka Wakenya wanapoteza maisha yao. Marekesbisho haya yanaweza kutengeneza sheria ikawa mwafaka kuhusiana na unyinyizaji wa maji katika nchi yetu. Bw. Spika, ninaunga mkono. Asante.
view
10 Feb 2022 in Senate:
On a point of information, Mr. Speaker, Sir.
view
10 Feb 2022 in Senate:
Asante Bw. Spika. Lile shamba la Galana Kulalu haliko tena. Kwa hivyo, haitamsaidia hata akisema lilitumika vibaya ama namna gani. Limefungwa na hakuna kazi yoyote inaendelea katika Galana Kulalu.
view
10 Feb 2022 in Senate:
Bw. Spika, pengine Kiongozi wa Walio wengi hajafahamu vyema. Hivi sasa, Serikali ndio inafanya mipango ya kuwekeza wale watu ambao wanataka kutengeneza shughuli ya Galana Kulalu, mambo ya mimea, huduma zao na kila kitu. Lakini, hivi sasa tukiongea, upande wa Galana Kulalu, ikiwa area yangu ninayo
view
10 Feb 2022 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
10 Feb 2022 in Senate:
wakilisha hapa, haifanyi kazi. Hakuna chochote ambacho kinatendwa katika lile shamba la Galana-Kulalu.
view
10 Feb 2022 in Senate:
Bw. Spika, sijui ni kwa nini tunajibizana na Kiongozi wa Walio Wengi na mimi ninaongea kuhusu upande ambao ninafahamu vizuri na ni eneo langu. Shamba hili sasa limepata mabwenyenye. Serikali imekata mapande nakugawanya ilhali watu wanaoishi pale, hawajapewa mashamba. Iko kesi kubwa sana ambayo tumeleta kwa Serikali ya kwamba wenyeji wapewe shamba katika maeneo ya Galana Kulalu ambayo ina pande mbili. Galana iko Kilifi na Kulalu iko Tana River. Kwa hiyo, lazima awezekuelewa yale maeneo. Maneno hayo sasa yanajibishiwa kwa hali ya kwamba watu wanazungumza lakini iweze kugawanywa kisawasawa na wakaaji wa pale wapewe hanki. Kama ni Wagiriama, wapewe mashamba ...
view
10 Feb 2022 in Senate:
Bw. Spika, jambo tulilokuwa tunaongea hapa ni la muhimu sana. Ni ukweli kwamba mimi na ndugu yangu, Sen. Poghisio, tuko upande moja wa kisiasa katika eneo la Azimio la Umoja. Sioni sababu yoyote ya mtu kuleta mambo ya Azimio la Umoja hapa ikiwa swala la mashamba linaloangaliwa hapo ni muhimu. Kwa hivyo, yeye anahaki yakuleta mambo ya kisiasa hapa ilhali hakuna mtu yeyote ambaye ameleta mambo ya kisiasa?
view