16 Feb 2022 in Senate:
Upande wa iliokuwa Western Province kuna majabali ya utalii ambayo yanalia. Watalii wanaenda kule kwa wingi kuangalia ni kwa nini majabali fulani yaliyoko pamoja yanatoa machozi. Hii ni kwa sababu Mungu ametupea mazingira ya utalii.
view
16 Feb 2022 in Senate:
Mahali kama India, ukiwa Delhi ununue shati ama rinda ya Kshs15 zile wanaziita Rupee, hata ukasafiri kilomita 1,000 ndani ya India na kwenda Madras, ile nguo uliopata New Delhi kwa Kshs15 utaipata kule chini pia kwa Kshs15. Hii inamaanisha zile jumuia za kaunti za kule ambazo ni regional governments wanafanya kazi wakiwa wamesikizana. Kila mtu anategemea mwingine kuona kwamba kila mwananchi anafaidika aliko nchini India. Hayo yanawezekana kufanyika humu nchini.
view
16 Feb 2022 in Senate:
Singapore ni nchi ndogo, lakini kwa sababu iko na ports imefanya maajabu. Ukienda kule watu wamefaidika na uchumi wa nchi yao. Singapore inajulikana kwa sababu iko na bandari. Bandari peke yake inafaidi kila mtu Singapore. Sisi hapa tuna bandari na hatujui pale ilipo kwa sababu inasaidiwa pia na Serikali. Tunashindwa kama bandari ya kule Singapore inaweza kusaidia serikali. Yetu hapa ni kinyume kwa sababu ya ufisadi. Jiji la Mombasa likiwa na bandari kama Singapore City, watu wa kwanza kufaidika na ile bandari ni wakaaji wa Mombasa. Tukiangalia uchumi wetu na hali yetu ya Maisha, ukifika Mombasa sasa hivi utaionea huruma. ...
view
16 Feb 2022 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
16 Feb 2022 in Senate:
Jumuia ya Kaunti za Pwani, ikiwa wanaweza kushirikiana vizuri na tukiwa tunaweza kuwa na bandari ambayo asilimia fulani inatolewa na kupewa kaunti za Pwani, maendeleo fulani inaweza kupatikana. Bi. Naibu Spika, tunaelewa kwamba Bandari ya Dubai inasifika sana ulimwenguni. Watu wa Dubai wanashirikiana kama Emirates .
view
16 Feb 2022 in Senate:
Kuna Sharja na hizo zingine ambazo ndugu yaki, Sen. Faki, amesema kama vile Abu Dhabi. Bi. Naibu Spika, hakuna mtu anaweza kuishi pekee yake. Ukienda Sharja, Dubai na pande zingine utapata kama nilivyotangulia kusema, ukiwa unapeleka gari kule, ukija huku kwingine petroli iko sawa sawa. Kuna usawa pia katika maendeleo ya pande zote. Nilikua natazama video ya mtaalam mmoja kutoka United States of America (USA) na alikua anashangaa. Alisema, ‘ you did this in 50 years ?’ Katika miaka 50 wamegeuza United Arabs Emirates (UAE) ikakua kitu ambacho ulimwengu mzima unashangaa. Kila kitu kinafanya kazi kisawasawa. Hiyo inamaanisha kwamba UAE ...
view
16 Feb 2022 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
16 Feb 2022 in Senate:
Pili, kaunti ambazo ziko pamoja zinafaa kushirikiana ili tuweze kufanikiwa kama Wakenya.
view
15 Feb 2022 in Senate:
Asante Bw. Spika. Namshukuru na kumsifu mama Julia Andifu ambaye ni Mkenya aliyeleta ardhihali hapa Seneti. Kitu cha kwanza, kwa mama ama familia kumpoteza mtoto katika ile miezi tisa alafu dakika za mwisho inaonekana kwamba maisha ya mtoto hayawezi kuwa au daktari kufanya uamuzi wa yupi ataponyesha na ni yupi hawezi kupona, ni jambo la kusikitisha na huzuni ndani ya familia. Nina hakika mama Andifu alipoandika ardhihali hii, akilini mwake alikuwa anatafakari uchungu wa mama. Kule nyumbani tunasema, uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi. Ardhihali hii ni changamoto sana kwa hili Bunge letu. Hakuna aliyependa kufiwa na mwana ama kumpoteza ...
view
10 Feb 2022 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Ni jambo la kusikitisha kwa ripoti ya Mwenyekiti kuja hapa na kuwa kama ripoti ya kawaida. Hususan ni kwamba Mkenya ama wakenya wamepoteza Maisha yao. Tunatarajia ya kwamba taarifa kama hiyo ambayo imeletwa hapa mbele ya Bunge iwe imeshikilia, inaweza kutegemewa na kutufikisha mahali pa kutuambia aliyetenda kitendo hicho, kwa sababu gani, na hatua gani itachukuliwa na serikali. Jambo la kusikitisha leo ni kwamba huyu mama anayeitwa Joannah aliuwawa na imekubalika kuwa aliuwawa. Lakini baada ya hapo ni hatua gani imechukuliwa kuona ya kwamba wale watu waliofanya kitendo hicho cha kinyama wamechukuliwa hatua. Maneno kama haya vilevile ...
view