2 Mar 2022 in Senate:
Asante sana Bi. Spika wa Muda. Ningependa---
view
2 Mar 2022 in Senate:
Yes, I want to make that intervention
view
2 Mar 2022 in Senate:
Asante sana, Bi. Spika wa Muda. Ningependa kujiunga na hio Kauli ya Nidhamu ambayo imeletwa na ndugu yetu Sen. Omogeni. Jambo la kwanza, nilikua katika hio safari ya kuenda ulaya na Sen. Omogeni. Utaona ya kwamba kutoka nchini kulikumbwa na maswali kwa kuwa hakukuwa na ruhusa ya kutoka nchini kwa kuwa kuna barua kutoka Serikali. Niliwauliza wanionyeshe barua hiyo ambayo inazuia mmbunge kufanya kazi yake. Tukitoka hapa, sisi huwa na idhini ya Bunge hili. Ikiwa barua ile imeandikwa na wewe mwenyewe kama Spika na umeandika kuwa huyu Seneta ameenda safari ya kikazi lakini tunaona kama barua hiyo imepuuzwa na kuna ...
view
2 Mar 2022 in Senate:
Bi Spika wa Muda, ni jambo la aibu kuona abiria wengine wanatoka ilhali kiongozi anawekwa kando na kukabiliwa na maswali asiyo yaelewa. Maswali kama mbona alitoka nje ya nchi, amerudi kutoka wapi, alitoka vipi na aliingia vipi. Ni jambo la kusikitisha na halina heshima.
view
2 Mar 2022 in Senate:
Kwa kukosewa heshima hivi na Serikali, tungetaka kujua kama Bunge, tukiongozwa na Kiongozi wa walio wengi, Sen. Poghisio, aliyepeana hiyo idhini ni nani? Tunamtaka aliyepeana hiyo idhini ya kuzuiliwa kwa Maseneta kutosafiri nje, aje mbele ya hili Bunge atueleze ni nani aliyempa hayo madaraka.
view
2 Mar 2022 in Senate:
Ni jambo la kusikitisha Bi. Spika wa Muda familia au watu wanakungoja nje unaporudi na huku unachakurwa na askari wakichunguza kwa nini ulitoka, kwa nini unarudi na sababu ya kuenda nje. Jambo hili lafaa tulichukulie hatua.
view
2 Mar 2022 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, naomba ulipeleke jambo hili kwenye kamati husika hata ikiwezekana Kamati ya Sheria iwe mojawapo itakayohusika katika uchunguzi huu, ili tuweze kujua na kulifikisha mwisho lisitendeke tena.
view
2 Mar 2022 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
16 Feb 2022 in Senate:
Thank you, Madam Deputy Speaker. I have a Point of Order on the fact that, my brother whom I respect so much, nominated Senator, Sen. (Dr.) Mwaura, is incidentally wearing a disco hat and something like a pajama.
view