Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 921 to 930 of 2266.

  • 2 Mar 2022 in Senate: Asante, Bi. Naibu Spika. Kwanza, nataka kutoa kongole kwa walimu ambao walijitoa mhanga kufundisha watoto wadogo katika shule za chekechea. Tunaelewa hiki ni chama cha walimu wa shule za chekechea na ni wanachama wa kile chama cha walimu. view
  • 2 Mar 2022 in Senate: Bi. Naibu Spika, ijapokuwa hawa ni watu wa chama, kuzingatia harakati zao ni kwamba waliweza kuachishwa kazi. Hili ni jambo la kusikitisha sana; kuleta hali ya uchumi mbaya kwenye nyumba za walimu. Walimu hawa wana taaluma ambayo walimu wengine hawana. Wanaanza kufudisha watoto wakiwa bado ni wachanga sana wakati hawajua chochote ikiwemo kusoma. view
  • 2 Mar 2022 in Senate: Kwa hivyo, ni walimu ambao wanatakikana kupewa heko. Lakini ni jambo la kusikitisha leo tukiona ya kwamba mahali kama Kaunti ya Nyamira wanaweza kuwafuta view
  • 2 Mar 2022 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 2 Mar 2022 in Senate: kazi walimu hawa ambao wanawaelimisha watoto hawa, kwa sababu ya nia zao binafsi, ili waweze kuweka walimu wao wengine wakifikiria kwamba hawa walimu hawana haki zao. view
  • 2 Mar 2022 in Senate: Bi. Naibu Spika, hawa walimu waliofutwa na wamefanya kazi miaka sita, wana haki mbele ya sheria za wafanyikazi na ndani ya hili Bunge la Seneti kuona ya kwamba haki zao hazizami na zimetekelezwa. view
  • 2 Mar 2022 in Senate: Wana bahati kwa sababu katika hiki kitengo ya kwamba wameachishwa kazi, katika Bunge hili la Seneti, kunaye mmoja wetu, ikiwa ni mimi, ambaye nilikuwa Jaji wa Mahakama Kuu hasa katika upande wa wafanyikazi. Kitendo kilichofanywa cha kuwafanya hawa wafanyikazi kupoteza kazi zao ni jambo la kusikitisha. view
  • 2 Mar 2022 in Senate: Bi. Naibu Spika, hivi sasa wako nyumbani; hawana kazi, wanateseka na wengine wana watoto ilhali kufutwa kwao kazi sio kwa ajili ya kupenda kwao, bali ni kwa sababu ya mtu mmoja ama mabepari wawili au watatu, walioketi katika ile kaunti wakaona ya kwamba katika maoni yao, hawa walimu wanafaa kuondolewa kwenye kazi. Tunasema hilo si jambo la usawa. view
  • 2 Mar 2022 in Senate: Bi. Naibu Spika, hii ni taarifa muhimu kwetu sisi. Kama hii ni taarifa muhimu basi ile Kamati ambayo inahusika kuangalia jambo kama hili, iweze kuona ya kwamba haki imetendeka kwa hawa walimu. Ikiwa itawezekana basi waweze kurejeshwa kazini. view
  • 2 Mar 2022 in Senate: Asante, Bi. Naibu Spika. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus