Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 901 to 910 of 2266.

  • 24 Mar 2022 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda. Nilikuwa pia nataka kumwambia yule ndugu yangu, Sen. Cheruiyot, Seneta wa Kericho, kama anataka hizi nakala, anawezazipata katika ofisi za maofisa wetu. Akienda hata sasa hivi, atazipata nakala hizo ambazo zitamueleza vyema. Ndugu yangu Sen, Cheruiyot na Sen. Olekina, waende huko watapata hizo nakala. view
  • 24 Mar 2022 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda kwa kunipa mda huu ili niweze kukupatia kokongole vile kamati ambayo ilihusika na kuandika ama kutengeneza--- view
  • 24 Mar 2022 in Senate: Bw. Spika wa Muda, nataka utetezi. view
  • 24 Mar 2022 in Senate: Bw. Spika wa Muda, ni jambo la heshima na la kusifu ya kwamba shughuli za bunge sasa zinaweza kuendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, Kizungu na pia lugha ya Ishara. Hili ni jambo ambalo linatufanya sisi kujivunia kuwa Wakenya, ya kwamba tuko na lugha tatu ambazo tunaweza kutumia katika nchi yetu. view
  • 24 Mar 2022 in Senate: Bw. Spika wa Muda, kuna umuhimu wa kunukuu hizi kanuni za kudumu za Seneti. Kwa mda mrefu sana, imekuwa vigumu sana kunukuu Standing Order s au Kanuni za Kudumu. Kwa hiyo ilikuwa ni jambo zuri kupata tafakari au tafsiri za Kanuni za Kudumu za Seneti ili Maseneta waweze kujua. Bw. Spika wa Muda, kumekuwa na uhaba kwa maseneta wengi. Hata huyu Seneta aliye mbele yangu, Sen. Olekina, ana tabia hiyo ya kuketi mbele ya wenzake wakiwa wanaongea. Nikiongea nataka nikuangalie sura. view
  • 24 Mar 2022 in Senate: Bw. Spika wa Muda, ni vyema kuona ya kwamba Kanuni Za Kudumu Za Seneti zimechapishwa kwa hii lugha ya Kiswahili. Ninatumai kuwa zitaendelea kusaidia. Na isiwe mwisho peke yake kutengeneza hizi Kanuni za Kudumu. Kanuni za Kudumu mara kwa mara zinageuka. Kwa hiyo itahitaji Kamati hiyo ya iketi na kuangalia zile kanuni zilizogeuka ziweze pia kutafsiriwa vingine. view
  • 24 Mar 2022 in Senate: Bw. Spika wa Muda, kuna wale wasomi ambao walihusika katika kutengeneza hizi Kanuni za Kudumu. Tumeelezewa kwamba wataalamu waliohusika walitoka katika view
  • 24 Mar 2022 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 24 Mar 2022 in Senate: , Moi University na Kenyatta University . Nawapongeza wenzetu hao walihusika sana kutengeneza hizi Kanuni Za Kudumu. Hususan, ningependa kupeana kokongole zangu, kwa wale Maseneta walioko hapa ndani, ikiwemo Seneta dada yetu msomi, Sen. (Dr.) Zani na ndugu yetu Sen. (Dr.) Mwaura, ambaye hayupo sasa hivi. Nafikiria ako katika ile hali ya kuzunguka huku na huku, akitafuta kura za United Democratic Alliance (UDA) badala ya kuja hapa ndani na kufanya kazi. Vilivile, yeye pia tunampatia kokongole, kwa sababu alikuwa mmoja ya wale watu ambao waliketi na wakatafakari ili kunukuu hizi kanuni za kudumu katika bunge letu la Seneti. view
  • 24 Mar 2022 in Senate: Bw. Spika wa Muda, kwa kumalizia, vile umesema mkoko ndio sasa unaanika maua, ni kumaanisha ya kwamba hakuna mwisho wa Kiswahili. Ikiwa mkoko umeanza kuanika maua sasa, ikiwa hizi kanuni za kudumu zitapatikana kuna kwengine kumekosewa na kwengine kutataka kurekebishwa, litakuwa jambo zuri sana. Nina hakika ya kwamba sio sisi tu bunge la Seneti limefika mwisho lakini hatimaye wale watakaokuja wakiwa wanataka kujifundisha ama kuongea Kiswahili ama kuongea kwa lugha ile ya Ishara am lugha ya Kizungu, basi watafaidika na hizi nakala ambazo tuko nazo. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus