Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 891 to 900 of 2266.

  • 31 Mar 2022 in Senate: Hivi sasa, tunaelekea katika mambo ya uchaguzi. Ningewauliza watu wa Machakos wenyewe, wakiongozwa na nyinyi kama viongozi, wafanyikazi wa huko na wananchi wanaoishi ndani ya Machakos, kwamba si jambo la kushutua sana ikiwa mama atapata nafasi ya kuchaguliwa tena katika uchaguzi utakaofuata. Kwa hivyo, asanteni sana kwa kuja hapa. Nafikiria yale mambo yote ambayo mmejifunza hapa yatakwenda kwa muda kusaidia Kaunti ya Machakos. view
  • 31 Mar 2022 in Senate: On a point of order, Mr. Speaker, Sir. view
  • 31 Mar 2022 in Senate: Bw. Spika, singependelea kabisa kumkatiza ndugu yangu kwa sababu sote tunasema kongole kwa wale waliokuja kutoka Machakos. Hata hivyo, sijui ametumia mistari gani ya Kizungu. Sikuelewa kama ni Kizungu, Kiswahili ama Kimaasai, vile alikuwa akisema kwamba angetaka Kimaasai kisajiliwe hapa pia. Ameongea katika lugha ambayo sikuifahamu. Sijui kama hivyo ni sawa ama si sawa. Naomba kama angeweza kufafanua kisawasawa. view
  • 31 Mar 2022 in Senate: Mr. Speaker, Sir, I second. view
  • 24 Mar 2022 in Senate: Asante sana Bi. Naibu Spika. Kwanza, natoa risala zangu za rambirambi kwa familia, jamii na wananchi wote wa Uganda kwa kumpoteza Spika wao. view
  • 24 Mar 2022 in Senate: Pili, tunajua kuwa kumpoteza Spika katika Bunge ni pengo kubwa sana. Halijatokea hapa kwetu na hatuombi litokee. Kumpoteza Spika katika Bunge, kunapatikana wakati mgumu sana. Majonzi kama hayo sio viatu vinavyoweza kuvaliwa na mtu mwingine. view
  • 24 Mar 2022 in Senate: Tulikutana na Mheshimiwa Oulanyah wakati wa michezo ya Waheshimiwa wa Bunge la Afrika Mashariki tukiwa Kampala, Uganda. Tulikuwa huko kwa wiki mbili. Wakati wa jioni, tulikukaa naye, tukala chakula cha usiku. Tunamkumbuka, Mheshimiwa Oulanyah kama mtu mcheshi. view
  • 24 Mar 2022 in Senate: Mkiketi naye hauwezi fikiria kuwa wakati unaenda. Baada ya muda, ndipo utaona saa zimeenda maana mkiwa naye, mnakula mkicheka na kuzungumza. Kwa hivyo, ni jambo la kusikitisha sana kwamba alipatatikana na ugonjwa wa saratani ambao haukugunduliwa mapema na hivi sasa umechukua maisha yake ilhali umri wake haukua mkubwa sana. view
  • 24 Mar 2022 in Senate: Kwa watu wa Uganda na Afrika Mashariki, kwa Maspika wote wa nchi za Uganda, Burundi, Rwanda, Kenya na Tanzania, tunawaambia pole kwa kumpoteza mpendwa wao. view
  • 24 Mar 2022 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus