Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 941 to 950 of 2266.

  • 16 Feb 2022 in Senate: I am not very sure that is the right attire for the House. I may leave it entirely up to you to make a decision. I do not think it is fair. I do not know whether that is him. I can see that is Sen. (Dr.) Mwaura. The other Sen. (Dr.) Mwaura, I am seeing on the other side is not properly dressed. view
  • 16 Feb 2022 in Senate: Hoja ya nidhamu, Bw. Spika view
  • 16 Feb 2022 in Senate: Bw. Spika, katika tafsiri ya ile Kauli anayoieleza sasa Sen. Faki, ikiwa unaitafsiri tofauti na vile ilivyoandikwa kwa Kingereza, mtu asimame na kusema yale makosa. Ikiwa yeye ana utaalam wa kutafsiri hii Kauli ya Kiingereza kwa Kiswahili hakuna makosa yoyote. Anayosema ni yale ambayo ameandika kwa Kingereza. view
  • 16 Feb 2022 in Senate: Asante, Bw. Spika. Ninamuunga mkono na pia ninamshukuru Seneta wa Mombasa Kaunti kwa kuleta Kauli hii. Bandari hii ni ya zamani. Tunakumbuka Bandari hii ilikuwa inatuika kwa biashara ndogo ndogo. Sio kama ile Bandari kubwa ya upande ule wa KPA . Bandari hii ilikuwa ya wafanyikazi na wafanyi biashara ndogo ndogo. Sio zile biashara kubwa kubwa za meli ama meli zile kubwa za kiutalii. Bandari hii ilikuwa inasaidia. Serikali inatakiwa kuwa na nia ya kusaidia wafanyikazi wadogo. Hii Bandari imekuwa ikiwasaidia wafanyibiashara wengi kama vile wa kuleta nguo kwa bei nafuu kutoka Kismayo ama Middle East . Vyakula kama tende ... view
  • 16 Feb 2022 in Senate: Bi. Naibu Spika, tumekuwa tukijadiliana pale chini na sikutaka kumkatiza Sen. Farhiya lakini sijui kama ni mazingaombwe ama ni sayansi ama ni kitu gani kinaendelea ndani ya hili Bunge la Seneti. Kuna taa moja linazunguka mataa mengine yote hayazunguki na hatujui sababu yake. Inaweza kuwa hatari kwetu sisi hapa ndani na kama kuna mtu anaweza kutufafanulia ni kwa nini taa moja lina zungukazunguka. zingine zote zimetulia na moja inatangatanga. view
  • 16 Feb 2022 in Senate: Ama kama sivyo tutoke basi maanake hii ni hatari. view
  • 16 Feb 2022 in Senate: Asante Bi. Naibu Spika. Pia ningependa kuunga mikono Mswada huu wa kuelekeza uchumi bora ndani ya hizi kaunti zetu. Huu Mswada umekuja wakati unaohitajika. Mswada huu una mambo mengi ambayo tunaweza kufanya. Ninawapa kongole wale magavana wote sita walioanzisha mfumu huu wa uunganishaji wa kaunti sita za Pwani, kuanzia Lamu, Tana River, Kilifi, Mombasa, Kwale na Taita-Taveta. Magavana hawa walianzisha mfumo wa jumuiya zote sita za kaunti za Pwani. Pengine kwa bahati mbaya au kwa msukosuko au kwa kukosa kuelewana hii jumuiya ya kaunti za Pwani ilififia. Tuko na muda mdogo uliobaki wao kuwa katika mamlaka. Mswada huu sasa hivi ... view
  • 16 Feb 2022 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 16 Feb 2022 in Senate: Hii si ndoto bali ni kwamba Mswada huu unaweza kutekelezwa. Hivi sasa macho ya kaunti zote 47 yanaelekeza katika Serikali ya Kitaifa ambayo imekuwa ikisaidia kaunti kwa kuzipelekea pesa. Hizi pesa tunazopigania hapa tukizipeleka, ingekuwa serikali zetu za mashinani ziko na utaratibu wa kutafuta pesa zao ziongezee juu ya hizo, zingeweza kuleta maendeleo mengi sana. Ninasisitiza kwamba hakuna kaunti kati ya zile 47 ndani ya serikali ambayo haina kitega uchumi. Tukianzia mambo ya utalii, tuko na mbuga za wanyama, bahari, upeo mzuri sana katika kila mahali, tukianza na upande wa Pwani. Nchi nyingi katika ulimwengu zimeweza kufaidika kwa sababu ya ... view
  • 16 Feb 2022 in Senate: Bi. Naibu Spika, ukiangalia pande kama za Turkana tuko na mafuta. Hiyo ni bora zaidi kwao kwa kuwa itawasaidia. Upande wa chakula, tuko na Bonde la Ufa ambako vyakula vya aina mbalimbali vinakuzwa. Cha muhimu ni mahindi ambayo inatumika kila mahali nchini. Upande wa samaki kuna Uchumi Samawati pande za Pwani lakini wanaoweza kutoa samaki wengi ni upande wa Nyanza katika Ziwa Victoria. Hiki ni kitega uchumi chao. Wakikichukulia kwa maana pamoja na vitega uchumi vingine vilivyomo pale, Kaunti ya Kisumu na zile zingine zote zilizoko kule Nyanza zitafaidika. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus