3 Nov 2021 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, kuna wengine katika mstari wanaopendelea kuongea pia. Mtu mmoja akichukua dakika nyingi, haitakuwa vyema. Ingewezekana, ingerejeshwa ili mtu mmoja achukuwe dakika tano ama tatu hivi. Ingekuwa vizuri zaidi ili kila mtu ambaye yuko hapa ndani apewe nafasi ya kuongea. Asante, Bwana Spika wa Muda. Hiyo ni kwa hisani yako.
view
3 Nov 2021 in Senate:
Bwana Spika wa Muda, nauliza kama Sen. Shiyonga siku hizi anaitwa Sen. Naomi Stewart ama namna gani. Mmechanganya majina hapo. Mnaweza kufafanua kwamba ni Sen. Stewart Madzayo kutoka Kaunti ya Kilifi ama ni Seneta mteule Sen. Naomi Shiyonga?
view
13 Oct 2021 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Kwanza ninawapa kongole walimu wa Kericho kwa kuleta malalamishi ya uandikishaji kazi na masaibu ya mishahara kwa walimu wa shule za chekechea. Tunaelewa kwamba shule za chekechea ndizo uti wa mgongo wa elimu ya watoto wetu. Kila mtoto anayezaliwa akifikia miaka mitatu au minne ni sharti aende shule ya chekechea ili awe na msingi mwema atakapoanza darasa la kwanza. Ni jambo la aibu hivi leo katika Kenya yetu. Jambo hilo haliko Kericho peke yake lakini katika kila mahali Kenya hii. Walimu wa shule za chekechea wanapata taabu sana. Wanabaguliwa na kutotiliwa maanani kabisa wakilinganishwa hata na wale ...
view
13 Oct 2021 in Senate:
.” Nikitafsiri ni kwamba mfanyakazi ambaye ana raha anaweza kufanya kazi na kuleta mazao ya ule utendakazi wake.
view
13 Oct 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
13 Oct 2021 in Senate:
Ikiwa walimu wa shule za chekechea hatutawaheshimiwa; ikiwa mwalimu wa shule ya chekechea atakuwa hajui kama leo anafundisha na kesho kazi yake itakuwa imekwisha, itakuwa hatuangalii siku za usoni. Bw. Spika, nitamalizia nikisema ni lazima zile ari za walimu wa chekechea zitekelezwe. Kamati ambayo itahusika na malalamishi haya yaliyoletwa na walimu kutoka Kericho, wasiangalie Kericho, bali tuweke mikakati kisawa sawa ambayo itaweza kuangalia walimu wote wa shule wanavyofundisha shule za chekechea katika nchi yetu ya Kenya. Asante, Bw. Spika.
view
12 Oct 2021 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda. Kwanza natoa kongole kwa Sen. Dullo. Ameileta Taarifa yake kwa wakati mwafaka, hususan wakati wa kujiandikisha kupata vitambulisho na hatimaye kuchukua kura ili kuweza kupiga kura zao mwaka ujao. Bw. Spika wa Muda, sio Isiolo pekee yake ambayo shida hiyo imetokea. Ameleta hii Taarifa sababu katika Kenya mzima, kila mahali, kumeweza kuhusikana katika huu uandikishaji wa kura. Katika Kaunti ya Kilifi kuna vijana wa kike na kiume zaidi ya 5,000 ambao hawajaweza kusajiliwa kupata vitambulisho vyao, na hatimaye kuweza kuchukua kura. Shida inayotokea ni kwamba, walivyotangulia kusema wenzangu, kunazo kamati za wazee na kamati za ...
view
12 Oct 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
12 Oct 2021 in Senate:
wanaotaka kuchukua vitambulisho, ni vizuri ikiwa wao watafanya kwa njia ya haraka sana. Tunajua machifu wanaishi na sisi. Jambo la kusikitisha, kama waliotangulia kusema hapo awali, ni kwamba ikifika wakati wa kijana wa Kikristo hakuna shida. Inakuwa ni haraka sana kuweza kumsajili na kumwambia aendelee kuchukua kitambulisho chake. Lakini ikifika kusajili kijana wa Kiislamu ambaye pengine hakupata nafasi ya kwenda kusoma - amekuwa akisoma katika Madrassa au misikitini ama hakupata nafasi hiyo - inakuwa ni shida. Anaanza kuulizwa mama yake ni nani na kama aliwachana na babake. Itakuwa namna gan? Anaanza kuulizwa aseme babu yake ni nani. Anaambiwa alete hati ...
view
12 Oct 2021 in Senate:
Asante, Bi Naibu Spika. Unaona kuwa Kiongozi wa Walio Wengi amenyamaza. Ndugu yangu Sen. Murkomen, Seneta wa Elgeyo-Marakwet ni Seneta shupavu sana. Amesema kwamba Sen. Poghisio, Seneta wa West Pokot, alimueleza kwamba yeye si Mkenya halisi.
view