Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1021 to 1030 of 2266.

  • 12 Oct 2021 in Senate: Nataka kuuliza kama matamshi kama hayo yako ndani ya Bunge. Ninauliza Sen. Poghisio kama yaliyosemwa na Sen. Murkomen ni ukweli ama si ukweli. view
  • 12 Oct 2021 in Senate: The Temporary Speaker, Sir, I was wondering whether I would get an opportunity to contribute to the amendment Bill. This debate will continue tomorrow, and I do not know whether we will have that chance. Looking at myself, I am- -- I need clarification. view
  • 12 Oct 2021 in Senate: Mr. Temporary Speaker, Sir, it is okay. I thank you so much for giving me that privilege, but I have not prepared myself properly. I guess I will do it at an appropriate time. Thank you. view
  • 5 Oct 2021 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda kwa kunipa kongole. Ningependa kumpongeza Seneta mteule, Sen. Nyamunga, kwa kupewa shahada hiyo sawa na mimi. Ninashukuru Bunge la Seneti kwa sababu lisingekuwa Bunge hili, pengine hatungezawadiwa medali hizi ya CBS. Bi. Spika wa Muda, Mswada huu wa Ushirikiano wa Umma na Wafanyibiashara Binafsi ni muhimu sana. view
  • 5 Oct 2021 in Senate: Bw. Spika wa Muda, nisamehe kwa sababu wakati mwingine ulimi unateleza. Niwie radhi. Mimi pia ni binadamu. Bw. Spika wa Muda, kwanza ninaunga mkono Mswada huu. Mswada huu unataka kutengeneza sheria mwafaka ambayo italeta uhusiano bora ulio katika misingi ya kisheria baina ya umma na wafanyibiashara binafsi. Waswahili husema ‘kidole kimoja hakivunji chawa.’ Hii ni kanuni kwamba Serikali au umma peke yake haiwezi kutekeleza miradi bila ushirikiano na wawekezaji wa kibinafsi. view
  • 5 Oct 2021 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 5 Oct 2021 in Senate: Kote ulimwenguni, tunaona serikali zina uhusiano na wawekezaji wa kibinafsi. Ni lazima Serikali ya Kenya izingatie sheria za kisasa kama hizi ambazo zitaleta uhusiano bora baina na umma na watu binafsi. Kitu ambacho tunaona ni mfano mzuri wa kuigwa ni kwamba tukiangalia hii barabara ambayo inatengenezwa hivi sasa ya Mombasa kwenda mpaka airport, na imeunganishwa mpaka huko Kawangware, hiyo ni kumaanisha wazi ya kwamba kidole kimoja hakiwezi kuvunja chawa. Hizi ni juhudi ambazo lazima sisi tuzitie mkazo na tuone ya kwamba zimekita mizizi ndani ya Serikali yetu ama ndani ya nchi yetu; ya kwamba tunaweza kuleta umma na wafanyabiashara binafsi ... view
  • 30 Sep 2021 in Senate: Asante Sana, Bw. Spika wa muda. Najiunga na wenzangu kwa yote waliyoyasema. Hivi majuzi, Sen. Olekina aliuliza swali kuhusu ndugu zetu wa Bara la Asia ambao wamekuwa wakiingia nchini kwa wingi mpaka kukawa na tashwishi ya kwamba pengine kutakuwa na mtafaruku wa amani. Swala alilouliza Sen. Olekina view
  • 30 Sep 2021 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 30 Sep 2021 in Senate: lilijibiwa magazetini na vyombo vingi vya habari. Hiyo sio taratibu ya sheria zetu za Kenya. Swali lolote likiulizwa hapa Seneti, Mawaziri wanafaa kujibu Seneti kwa heshima. Swali likiulizwa hapa Seneti, halifai kujadiliwa mahali pengine isipokuwa hapa ndani. Seneti kupitia Sen. Olekina alitaka kujua kama Wizara husika linajua kwamba watu wengi kutoka Bara la Asia wanaingi nchini kwa kuwa jambo hilo linawezakuleta mtafaruku wa amani. Ikiwa Mawaziri watakuwa wanajibu Seneti kupitia magazeti na vyombo vingine vya habari, nimngependa kusisitiza kwamba sio haki sisi kujibiwa na Mawaziri wakiwa wameketi katika ofisi zao. Seneti ikitaka mawaziri hao waje hapa kujibu maswali, lazima waje ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus