Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1031 to 1040 of 2266.

  • 29 Sep 2021 in Senate: Asante Bi. Naibu Spika. Ninamtolea kongole ndugu yangu, Sen. Githua Ngugi kwa kuteuliwa na kuja katika Bunge la Seneti. Yeye kama Seneta mteule ako na majukumu mengi ambayo anatakikana kuyatekeleza. Mrengo wa Jubilee ulikupa nafasi hii. Wewe ni kijana na uko na maisha marefu ya kuishi ndani ya hili Bunge kulingana na uwezo au utendakazi wako. Kwa hivyo, tekeleza wajibu wako uliokuleta hapa Seneti. Kuna mambo mengi utajifunza. Hili ndilo Bunge ambalo linajulikana Kenya nzima. Liko na wasomi kama wewe. Kwa hivyo, tuonyeshe ujasiri na elimu yako kulingana na vile utatendakazi hapa ndani ya Bunge la Seneti. Hivi sasa, ninaongea ... view
  • 29 Sep 2021 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 14 Sep 2021 in Senate: Asante, Bw. Spika. Kwanza ningependa kumpa kongole dada yetu, Sen. Kwamboka, kwa kuleta hii Taarifa. Kulingana na vile sisi na wananchi wanaona, Mheshimiwa Rais aliweka mkazo ili watu wawe wameenda nyumbani ikifika Saa Tatu. Lakini, tunaona kuwa kuna shida ya kutekeleza agizo hili kwa sababu kwa upande mwingine, wafanyabiashara wa aina mbali mbali wanafunga maduka yao Saa Mbili ili waweze kwenda nyumbani Saa Tatu na wafike kwa nyumbani Saa Nne. Wafanyabiashara wamepata taabu kwa upande wa ubaguzi. Ukiangalia upande wa Nairobi West, utaona kwamba watu wanalazimishwa kufunga biashara zao, na kwingine, watu wanaruhusiwa kuendelea. Hii yote inaletwa kwa sababu ya ... view
  • 14 Sep 2021 in Senate: Mhe. Bw. Spika, nasimama kwa hoja ya nidhamu. Sen. Olekina ni rafiki yangu sana, lakini ikifika kuendesha ratiba ya Bunge sawasawa tunatengana. Amesema kwamba yeye kama mmoja wa wale viongozi katika taifa hili kuna mahali wanapokwenda kustarehe mpaka saa kumi alfajiri na polisi wanapajua. Hatutaki kujuwa wanajivinjari na nani? Wanajivinjari mpaka saa hizo na wale ambao hawajiwezi, kwa mfano, wanaojivinjari pale Nairobi West, wanaambiwa wafunge hizo baa au sehemu za kustarehe saa moja jioni. Kama alivyosema wao hustarehe hadi saa nane ya usiku. Ukisema jambo kama hilo Bungeni ni lazima utaje mahali hapo. Je, ni haki kwake kuongea bila kutaja ... view
  • 14 Sep 2021 in Senate: Asante Bi. Naibu wa Spika. Kwanza ningependa kumpa kongole Seneta wa Mombasa, Mohammed Mwinyihaji Faki kwa kuleta Ripoti hii kuhusu hii Hazina. view
  • 14 Sep 2021 in Senate: Nina sababu tatu za kumuunga mkono. Kwanza ni kwamba hii ni Hazina ya Kuzama kwa sababu ni kitu ambacho kinatarajiwa kwa kuwa si kitu cha hivi sasa. Inasemekana kwamba Hazina hii itatuwezesha kulipa madeni ama mikopo ya siku za view
  • 14 Sep 2021 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 14 Sep 2021 in Senate: usoni. Hilo si jambo sawa kwa sababu huwezi kuchukua pesa sasa hivi ukaziweka kwenye shimo kisha useme kuwa zitakuwezesha kulipa madeni ya siku za usoni. view
  • 14 Sep 2021 in Senate: Jambo la pili ni kwamba hakuna hata siku moja ambapo Serikali ama nchi yetu imeshindwa kulipa madeni yake. Huwa tunafanya mipango ili madeni yote yalipwe. Sasa hivi kuna mabwenyenye wanaotumia akili. Kanuni za Hazina hiyo zinazotakikana kuwekwa na Benki Kuu ya Kenya ziko katika Hazina Kuu ya Taifa. Kuna watu katika Benki Kuu ya Kenya wanaotakikana kuhusika katika Hazina ya Kuzama. Wanafaa kuchangia na kuona kwamba sheria mwafaka zinafuatwa. Jambo la kusikitisha ni kwamba hawahusiswi katika kuangalia mambo ambayo yanaendelea katika Ofisi ya Fedha. Sababu ya mwisho ni kwamba usimamizi unaotakina kuangalia matumizi ya pesa sharti ufanywe kwa kuhusisha taasisi ... view
  • 9 Sep 2021 in Senate: Shukrani, Bi. Naibu Spika. Kwanza, ninampa kongole ndugu yangu, Sen. Kinyua, kwa kuleta Taarifa hii. Yeye ni Seneta mchapa kazi ambaye anawakilisha Kaunti ya Laikipia. Vilevile, ni mwenzangu katika kuzungumza Kiswahili mufti. Ni aibu kwamba leo hapa Kenya, jeshi letu haliwezi kuchukua hatua. Sasa hivi, tunavyoongea, familia 40 zimefurushwa kutoka makao yao huko Olmoran. Katika eneo la Kisii Ndogo, takrniban nyumba 50 zimechomwa na watu kufurushwa. Mkutano wa polisi ulikuwepo katika eneo hilo na kufanya mkutano mkubwa lakini huyu Bw. Natembeya na mkubwa wa polisi wa Kaunti ya Laikipia, wamezembea katika kazi yao. Kisii ndogo, kuna nyumba karibu 50 zimechomwa ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus