24 Sep 2024 in Senate:
barabara, shule za chekechea na maendeleo kadha wa kadha wanayotakikana waendelee nayo. Ni sisi tunaoelewa shida ambayo zinakuba serikali za ugatuzi na kazi zetu tulizonazo hapa. Ikiwa nitakupa taarifa, niruhusu niseme kwamba Kipengele cha 96, sheria ya kwanza, inasema kuwa kazi kubwa ya Seneta ni kuwakilisha kaunti na pia kuleta mahitaji ya kaunti ya ugatuzi na kulinda maslahi hayo. Hii ni kazi ambayo inahitaji uangalifu na udhalilifu wa hali ya juu sana kuona ya kwamba mahitaji haya yameweza kupatikana. Lakini cha muhimu zaidi kulingana na Mswada huu ambao upo mbele yetu, ni Kipengele cha 96(5) ambacho kinaongea juu ya taratibu ...
view
24 Sep 2024 in Senate:
Jambo la kusikitisha ni kwamba ikiwa huu Mswada utapitishwa vile ulivyo na tunawatuma hawa wenzetu ambao watatuwakilisha pale katika majadiliano haya, kuona ya kwamba wamesita, wameweka miguu yao kisawasawa kwa kusimama kidete na wasikubali hizi pesa ziweze kupunguzwa. Zikipuunguzwa, hatari itakuwa kwa watu waliochaguliwa kama Maseneta hapa kwa sababu wana swali la kujibu kule wanapotoka katika serikali za ugatuzi.
view
24 Sep 2024 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, nataka kumalizia nikisema kwamba shida za serikali za ugatuzi ni nyingi sana. Hivi sasa tunaona ya kwamba hata mishahara katika serikali za ugatuzi haijalipwa. Watu kule pia kama vile wafanyakazi wana haja za kulipa na kuna mengi ambayo wanatakikana kufanya kama wafanyakazi. Majukumu yote yanafanywa na serikali za ugatuzi. Kulipwa mishahara ni haki ya wafanyakazi.
view
24 Sep 2024 in Senate:
Hivi sasa utaona wako wasichana na wavulana ambao wameachishwa shule. Wengine wameshidwa kuenda vyuo vikuu kwa sababu baba zao bado hawajalipwa pesa. Ikiwa sasa hawajalipwa, itakuwaje sasa ikiwa hizi pesa zitapunguzwa?
view
24 Sep 2024 in Senate:
Hii ni kwamba sasa, hata kwa familia kama mtu mmoja alikuwa haendi shule, basi watoto wengine pia watafuata hiyo kauli. Hii ni kwa sababu hakuna pesa katika familia na lazima wao pia wakae nyumbani wasiende shule.
view
24 Sep 2024 in Senate:
Jambo ambalo nataka kusisitiza zaidi ni kwamba tusirudi nyuma. Tuangalie safari ya kuenda mbele. Tabia hii ya kuletewa Mswada na wale wenzetu na kusema kwamba The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate.
view
24 Sep 2024 in Senate:
tumepitisha pesa za juu, sisi tumesema tunataka shilingi bilioni 400 ziende katika serikali za ugatuzi. Naunga mkono kamati yetu iliyofanya kazi njema. Nawatakia kila la heri waweze kusimama kidete pale pale waliposimama.
view
19 Sep 2024 in Senate:
Asante Bw. Naibu Spika. Kwanza, ni jambo la kusikitisha ikiwa utatoa taarifa ambayo haina ushahidi wowote kutumia jina la mtu mwengine ambaye hakupewa taarifa yoyote. Kama ingewezekana, pia yeye angeitwa kwa televisheni wakajibizana ili ijulikane nani ni mkweli au muongo. Lakini si vizuri kuchukua upande mmoja kutoa taarifa ya kushambulia upande mwengine. Watu wengine na wengi wetu tuliopo hapa kama ndugu yangu, Sen. Kinyua, ni mtu aliyetengeneza jina lake kule Laikipia kwa miaka mingi mpaka sasa amekuwa Seneta. Bw. Naibu Spika, pia wewe kule Meru, umetengeneza jina lako kamili, kwa hiyo itakuwa ni makosa mtu akitaja jina lako kwa ubaya ...
view
19 Sep 2024 in Senate:
Ndio, niko barabarani kuelekea huko. Barabara ni ndefu sana. Tunalaani vikali kitendo kilichotendeka kwa taarifa ya habari. Nikirudi upande ule mwengine, ni jambo la kusikitisha vile vile kuona kwamba Kenya hii kuna watu wanaovaa magwanda ya kuficha sura na hatujui kama ni polisi ama majambazi. Kwa mfano, leo utapata mtu anakuja nyumbani kwako na humjui ni nani, na unapotoka kwa gari lako, anakuvamia na unatoweka. Tuliona kitendo hicho wakati Mhe. Alfred Keter alishikwa na polisi. Alishikwa akiwa barabarani wakati yeye ni mheshimiwa. Si jambo nzuri kwa Mkenya kushikwa kiholela akiwa Kenya. Nikija upande wa dada yangu, watu wake watatu wameshikwa ...
view