Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1431 to 1440 of 2266.

  • 12 May 2020 in Senate: No, Mr. Deputy Speaker, Sir. view
  • 12 May 2020 in Senate: Jambo la nidhamu, Bw. Naibu Spika. view
  • 12 May 2020 in Senate: Bw. Naibu Spika, nimesimama kwa sababu ninataka kumkosoa, Sen. Kihika. Je, kulikuwa na mapinduzi? Tunaambiwa kuwa kuliwa na coup. Tunavyoelewa ni kwamba wakati kuna coup, lazima kuwe na mapinduzi au mageuzi ambayo si ya kihalali. view
  • 12 May 2020 in Senate: Ahsante, Bw. Spika. view
  • 12 May 2020 in Senate: Bw. Spika, nataka kumpatia kongole ndugu yangu, Sen. Poghisio, kwa kuchaguliwa kama kiongozi wa walio wengi Seneti. Wahenga walisema ya kwamba, maji yakimwagika, hayazoleki. Kwa hivyo, nataka kumpatia nguvu dadangu Sen. Kihika na ndugu yangu, Sen. Murkomen na kuwaomba ya kwamba wakubali yale ambayo yametendeka. Wasitapetape hapa na pale. Wao ni Maseneta wa Elgeyo Marakwet na Nakuru. Kwa hivyo, wafanye kazi na juhudi zao zitaonekana na wale ambao waliowapigia kura. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 12 May 2020 in Senate: Kuna msomi mmoja aliyeishi miaka mingi iliyopita aliyekuwa anaitwa Machiavelli. Alisema ya kwamba, ‘usijifanye mwerevu kuliko bosi wako’. Leo, nikiwa mwanachama wa Ford Kenya, siwezi kuwa mwerevu zaidi ya ndugu yangu Sen. Wetangula. Hii ni kwa sababu ataniambia eti atanichapa kiboko na yuko na huo uwezo wa kunichapa. Kwa hivyo, tunajifunza mengi kwa wale wahenga. Vile vile, bosi wako ni bosi wako hata kama haukubaliani naye kwa sababu yuko na mbinu, njia na akili na hio ndio sababu ni bosi wako. Kwa hivyo, ningependa kuwatia moyo ndugu zangu na kuwaambia ya kwamba sisi sote tuko hapa kwa sababu ya vyama ... view
  • 12 May 2020 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika. Langu ni kuwatia moyo na kuwaambia ya kwamba maji yamemwagika hayazoleki. Tukubaliane na tuendele na maisha. view
  • 12 May 2020 in Senate: On a point of order, Mr. Deputy Speaker, Sir. view
  • 12 May 2020 in Senate: Mr. Deputy Speaker, Sir. If you notice, Sen. Were is not wearing her mask properly. Her nose is open. Secondly, the Deputy Minority Leader, my young brother, Sen. Malalah, is sitting in a place that is not marked that you can sit. That is, where you are not supposed to sit. They are discussing or consulting, which is good thing to do, but they are not in order. Are they in order to sit like that? view
  • 5 May 2020 in Senate: Asante sana, Bw. Spika. Kwanza, ninamshukuru ndugu yangu Sen. Sakaja kwa kuleta jambo hili. Cha muhimu zaidi ni kwamba kukitokea shida kama ile niliyoiona katika sehemu fulani ya Nairobi ambayo ameitaja, ni jambo la kusikitisha kuona watoto wachanga, akina mama na vijana wakihangaika sana. Niliona kama ni kitendo cha unyama ambacho hakijatendeka katika taifa hili; kuona mama na mtoto wakitupwa kando bila kujali kilicho ndani ya nyumba. Mali inatupwa na kuvunjwa. Hata sufuria ambazo pengine wangeweza kupikia baada ya hiyo ghasia, nazo pia zinatupwa. Hao Wakenya wenzetu ambao hata kama wameketi kwenya ardhi ambayo si yao, si vizuri kufurushwa kama ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus