5 May 2020 in Senate:
Langu ni kwamba, mkondo uliochukuliwa na Serikali kuwafurusha watu hapa Nairobi ndivyo ilivyo Kilifi. Juzi wametoa Malindi nzima wakapiga watu kila mahali. Wamenunua mijeledi ya kuchapa watu. Sijui ni sheria gani katika Serikali hii inasema polisi sasa wanaweza kutumia mjeledi kuchapa Mkenya mwingine. Ni lazima heshima iwepo. Mkenya ana haki ya kuishi hapa na kuheshimiwa.
view
28 Apr 2020 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika. Nilikuwa ninafikiria pengine unaona upande ule tu, na huku nyuma hakuna hata mmoja wetu ambaye ameitwa.
view
28 Apr 2020 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika. Ningependa kukubaliana na vile Sen. Orengo amesema kwamba kuna tabia ya kushika watu bila heshima.
view
28 Apr 2020 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika. Nilikuwa ninasema ya kwamba ni ukweli kwamba saa zingine vile ambavyo majina ya watu yanaharibiwa ndio huleta shida katika familia. Utaona ya kwamba haswa Kilifi imetajwa sana katika mambo haya ya COVID-19. Katika Kilifi, kuna naibu wa gavana ambaye alitajwa. Bw. Saburi ana mke na watoto watatu. Wale watoto watatu na mke wake walifanyiwa vipimo na hakuna hata mmoja alipatikana na virusi hivyo. Yeye pia ako na stakabadhi za hospitali za Kenyatta National Hospital, Nairobi Hospital na Mombasa Hospital. Vipimo hivyo vyote vilionyesha kwamba hana virusi hivyo. Tabia kama hiyo ni ya kuharibia watu majina. Hivi ...
view
17 Mar 2020 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii. Ninakubaliana na Hoja inayosema kwamba badala ya kuwa na siku 30, Bunge la Seneti liahirishe vikao vyake kwa siku 15 na hatimaye tuwe tukija hapa siku moja kwa wiki. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
17 Mar 2020 in Senate:
Kwanza namshukuru Waziri wa Afya, Mhe. Mutahi Kagwe, kwa ujasiri wake wa kueleza Wakenya kinachoendelea. Tunajivunia kwa sababu tulikuwa tunaketi naye hapa muhula uliokwisha. Ameonyesha ujasiri na ukakamavu katika Wizara ya Afya.
view
17 Mar 2020 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, kitu cha kwanza Serikali inafaa kufanya ni kuangalia vifaa vya kazi. Pole Bi. Spika wa Muda kwa sababu nimekurejelea kama Bw. Spika wa Muda. Sijui kama watu wanaelewa Kiswahili kwa sababu sikusikia point of order. Hata hivyo, nashukuru kwa sababu nimejirekebisha. Najua kuwa Sen. Wambua anatoka Kitui---
view
17 Mar 2020 in Senate:
Nimeshasema kwamba nimekosea.
view
17 Mar 2020 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda. Sijui kama hilo ni Jambo la nidhamu ama ni maelezo. Sisi sote ni binadamu na vile vile tunaweza kupatikana na Virusi vya Korona au COVID-19. Hakuna aliye mjasiri mbele ya ugonjwa. Kwa hivyo, ni muhimu pia sisi kuenda mashinani kukutana na wananchi tunaowakilisha katika Seneti, ili waweze kutueleza masaibu wanayoyapata.
view
17 Mar 2020 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, wakati ninaongea Maseneta wawili wako mbele yangu. Je, hii ni haki? Vifaa ambavyo viko katika hospitali ni nadhifu. Aidha havifai, haviwezi kuzuia ugonjwa ama havitoshi. Juzi tuliona kwamba katika hospitali ya Mbagathi na sehemu mbali mbali Kenya bado madaktari na wasaidizi wao wanaofanya kazi na mikono mikavu. Katika nchi zingine tunaona kuwa kuna vifaa vya kujilinda kutokana na Virusi vya Korona. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view