Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1451 to 1460 of 2266.

  • 17 Mar 2020 in Senate: Jambo la kwanza ambalo Serikali inafaa kuzingatia ni kwamba vifaa hivyo vinapatikana haraka iwezekanavyo, ili wanaowatibu wagonjwa wa Virusi vya Korona wanajikinga ili wasiambukizwe virusi hivyo vya Korona. Je, Kenya Medical Research Institute (KEMRI) inafanya nini? Kwa mfano, view
  • 17 Mar 2020 in Senate: ni ghali sana kwa mwananchi. Juzi nilinunua kwa bei ya Kshs2,000. Gharama hiyo inaweza kununua chakula cha siku kadhaa kwa mwananchi wa kawaida. Serikali inapaswa kuthibiti bei ya dawa hii ya kusafisha mikono ili virusi viweze kumalizika. Mwisho, namuunga mkono Sen. Olekina kwa kusema kwamba ndugu zetu wanaofanya kazi kule viwandani na kazi zingine za mapato madogo. Serikali inafaa kuchukua hatua ya kupanga mikakati ili watu kama hao wapewe nafasi ya kuvuta pumzi ili wasilipe kodi ya nyumba wanamoishi. Hii itahakikisha kwamba wanabaki nyumbani na kuepuka hili janga la Virusi vya Korona. Asante Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa wakati ... view
  • 12 Mar 2020 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Naunga mkono hii Ripoti ambayo imewasilishwa katika Bunge la Seneti na Mwenyekiti wa Kamati ya Barabara na Usafiri. Ni aibu kwamba zaidi ya miaka 50 tangu Kenya ipate Uhuru, tumejipata katika hali ya suitofahamu haswa katika upande wa uchukuzi. Hali hii imeathiri wafanyabiashara, wasafiri na wanaoishi katika sehemu hizo. Kulingana na Ripoti hii, kuna kilomita zaidi ya 20 ambazo hazijakamilika. Magari yanapewa kibali cha kusafiri baada ya siku mbili au tatu. Tunashuhudia hali hii kule Mariakani katika Kaunti ya Kilifi. Bw. Spika wa Muda, je, umewahii kusafari ukitumia barabara ya Nairobi- ... view
  • 12 Mar 2020 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 12 Mar 2020 in Senate: Ripoti hii ni muhimu na imekuja wakati unaofaa. Kamati husika inafaa kufuatilia ili kuona kwamba barabara zetu za mipakani zimetengenezwa ili kurahisisha usafiri. Ripoti hii imegusia kidogo tu eneo ambalo ninatoka. Mhe. Rais Uhuru Kenyatta alienda kule na watu walifurahi sana. Aliahidi kuwa barabara ya Bamba kwenda Mariakani, Ganze hadi Mji wa Kilifi itatengezwa. Barabara hiyo ni muhimu sana kwa watu wa maeneo ya Kaloleni na Ganze. Barabara yenyewe imetengenezwa tu kuanzia Mariakani na ikakomea Bamba. Kwa wale wanaosafiri kuelekea Ganze na Kilifi, hali yao ya usafiri ni ya utata zaidi. Unaweza kutumia masaa manne mahali pa kilomita 40. Barabara ... view
  • 12 Mar 2020 in Senate: Katika eneo lilo hilo kuna watu wengi sana. Watu wanazaana. Nadhani wanataka kuongeza idadi ya wananchi na leba katika nchi yetu. Akina mama wajawazito wanaoishi maeneo ya katikati ya Bamba, Ganze na Kilifi wanaweza kuathirika pakubwa kiasi kwamba mama au mtoto anayezaliwa anaweza kufa, ama wote wawili, kwa sababu ya kukosa usafiri wa haraka kwenda hospitali ya Bamba ama Kilifi. Ni aibu kwa Serikali yetu ya kwamba baada ya miaka karibu 60 tangu tupate Uhuru, mama anaweza kukosa usafiri wa kwenda kujifungua na afie barabarani. Bw. Spika wa Muda, ukiangalia maeneo ya eneo Bunge la Kaloleni, kuanzia Kaloleni, Maandani mpaka ... view
  • 12 Mar 2020 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 12 Mar 2020 in Senate: Kwa kumalizia, upande wa Rabai, kuna barabara ya kutoka Mazeras mpaka Kaloleni ambayo ilijengwa kwa miaka mingi sana. Ilijengwa zamani, zaidi sana ya miaka 20 iliyopita. Sasa hivi imeharibika kwa sababu ina mashimo kila mahali. Haijapanuliwa wala kufanyiwa ukarabati. Ni kama tu kichochoro. Kuna lami upande mmoja na ukivuka vibaya unaanguka. Hiyo ni aibu. Ripoti hii imeletwa katika Bunge letu la Seneti. Kwa hivyo, Kamati ya Barabara na Uchukuzi lazima ihakikishe kwamba hatua imechukuliwa na Serikali. Wanafaa kuhakikisha kuwa mapendekezo yote yanafanywa. Sisi tutakuwa nyuma yao kuona ya kwamba tumepitisha Ripoti hii na hatimaye hatua kuchukuliwa na Serikali. view
  • 11 Mar 2020 in Senate: Asante sana, Bw. Spika. Nashukuru ndugu zetu ambao wameweza kufika hapa kutoka Bunge la Afrika Mashariki wakiongozwa na Serjent-at- Arms, Bw. Migosi pamoja na Bw. Kikwae. Natumaini ndugu zetu wamejifunza mambo mengi katika Bunge la Seneti. Ni matumaini yangu kwamba wakirudi nyumbani, watapata ufahamu mzuri. Bunge la Afrika Mashariki ni Bunge muhimu sana kwetu sisi kwani huleta watu wote wa Afrika Mashariki katika kikapu kimoja ili tuwe na kuelewana na utangamano mzuri. Nawaomba wapeleke salamu zetu huko Jumuiya ya Afrika Mashariki. Tunaomba kwamba Bunge letu la Afrika Mashariki lizidi kudumu na kuleta uhusiano mwema katika Afrika Mashariki. Asante sana, Bw. ... view
  • 11 Mar 2020 in Senate: I am sorry, Mr. Deputy Speaker, Sir. It is not in my habit to interrupt, but I pressed the intervention button, so I was wondering whether my name is appearing. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus