Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1461 to 1470 of 2266.

  • 11 Mar 2020 in Senate: I thank you, Mr. Deputy Speaker, Sir. view
  • 11 Mar 2020 in Senate: Asante sana, Bw. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii. Ningependa kumshukuru ndugu yangu Sen. Cherargei ambaye ni Seneta mtenda kazi kutoka Nandi kwa kuleta Taarifa hii katika Bunge la Seneti, kuhusu kufungwa kwa kiwanda hiki cha Kibos. view
  • 11 Mar 2020 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 11 Mar 2020 in Senate: Ni jambo la kusikitisha kwamba mwaka 2020 ulipofika tuliambiwa ya kwamba watu 3,000 wamepoteza kazi zao na wakulima zaidi ya 10,000 wamebaki na mimea ya miwa katika mashamba yao. Hawana mbele wala nyuma na hawajui waende wapi na miwa yao inaozea mashambani. Si vyema kutojali wengine wanavyoumia kwa sababu hatuna mashamba kule. Mtu aliye na ekari zaidi ya 10 za miwa sasa hajui afanye nini. Hakuna faida tena ya miwa kwa sababu itaozea kwa shamba. view
  • 11 Mar 2020 in Senate: Bw. Naibu Spika, hiyo ni dhuluma iliyofanywa na the National Environment view
  • 11 Mar 2020 in Senate: ilipewa jukumu la kukaa na wakulima wa Kiwanda cha Sukari cha Kibos na kampuni nyingine ambazo zinaendeshwa na Wakenya ili kuwaeleza watu jinsi ya kufanya biashara zao zifaulu. Jambo kama hili ni la kusikitisha kwa sababu Kenya ni miongoni mwa mataifa yanayotegemea ukulima. view
  • 11 Mar 2020 in Senate: Jambo kama hili lilitendeka katika Kaunti ya Kilifi ambako ninatoka. Kulikukwa na wakulima kutoka maeneo bunge ya Ganze, Magarini, Kilifi Kaskazini, Rabai, na Kaloleni. Wakulima hao walikuwa wakipanda korosho. Mimea ya korosho ilikuwa imetapakaa kila mahali. Hali ya uchumi wa Kilifi ilikuwa juu sana kutokana na uuzaji wa korosho, kwa sababu kulikuwa na ofisi za Kenya Cashew Nuts Exporters and Suppliers kule Kilifi. view
  • 11 Mar 2020 in Senate: Vijana zaidi ya 5,000 wakiwemo akina mama walikuwa wakifanya kazi. Kampuni hiyo ilifungwa kwa njia sawa kama ilivyofanyika katika Kibos Sugar Factory. Kampuni hiyo ilipofungwa, zaidi ya wakulima 20,000, akiwemo baba yangu aliyekuwa akipanda korosho, waliathirika. Alikuwa anauza mazao yake kupitia kwa shirika hilo lililokuwa na ofisi kule Kilifi na kupata pesa za kumwezesha kukimu mahitaji ya familia yake na kusomesha watoto wake kama sisi tulivyosomeshwa. view
  • 11 Mar 2020 in Senate: Najua kuwa wakulima ambao wamekuwa wakipeleka miwa katika Kiwanda cha Sukari cha Kibos wana majukumu mbalimbali. Sasa ufukara ama umasikini utaingia katika eneo hilo. Haya yote yanaletwa kwa sababu mashirika kama haya yanafanya mipango na mabepari. Kuna kampuni nyingine ambazo ziko huko na hakuna haja ya kuzitaja. Ni dhahiri kuwa ni mpango wa kufunga Kiwanda cha Sukari cha Kibos ili mwingine apate faida zaidi. Ikiwa huo ndio mpango, Seneti hii lazima isimame imara ili kuzuia mipango yote ya NEMA kufunga kampuni hiyo. Tunafaa kumwita Waziri anayehusika na ukulima aje hapa atueleze kama amekubaliana na mambo hayo. Watu wengine husema; kama ... view
  • 11 Mar 2020 in Senate: Ndugu yangu amesema kuwa lazima tuwe na certificate of emergency . Alichomaanisha ni kuwa hatua inafaa kuchukuliwa kwa haraka lakini akatumia neno view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus