Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1521 to 1530 of 2266.

  • 20 Nov 2019 in Senate: kusema kwamba ataendelea kulipa mkopo huo, kuna umuhimu wa watu kama hao waambiwe ya kwamba watalipa deni mara moja ili pesa ambazo zitapatikana zitatumiwa kugharimia masomo ya wanafunzi kutoka familia maskini ambao hawajiwezi. Ni aibu kuona ya kwamba wewe uko katika Bunge la Jamhuri ya Kenya na bado unaendelea kulipa pole pole mkopo wa chuo kikuu. view
  • 20 Nov 2019 in Senate: Ninajua anaangalia runinga pale alipo na ninataka anisikize. Ikiwa wewe una uwezo afadhali ulipe mkopo huo mara moja badala ya kulipa pole pole ilhali watoto wa Kenya wako nyumbani bila kazi. Wengine wanadaiwa na wewe bado unalipa reja reja ilhali unaweza kulipa deni hilo mara moja. Ni jambo la kusikitisha kwamba watoto wetu sasa wameanza kujiingiza katika maswala mabovu mabovu ambayo yana madhara kwa Wakenya wenzao kama AlShabaab . Katika ufuo wa bahari, tunaona wengine wakivuta vitu ambavyo havitakikani kuvutwa. Kwa hivyo tunasema ya kwamba ikiwa hii HELB inaweza kupewa kama loan ya Serikali vile ambavyo vifaa vinavyotumika katika hospitali ... view
  • 20 Nov 2019 in Senate: On a point of order, Mr. Temporary Speaker, Sir. view
  • 20 Nov 2019 in Senate: Mr. Temporary Speaker, Sir, I do not know whether my ears heard right. Were you referred to as a brother or father-in-law? Is that the true position? view
  • 20 Nov 2019 in Senate: Asante, Bi Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili pia mimi niweze kuiunga mkono Ripoti hii iliyo na maendeleo ya nchi zote za Jumia ya Madola katika taratibu zao za kuendesha mkutano ambao ulifanyika Kampala, Uganda. Mambo yaliyozungumzwa katika mkutano huo yalikuwa mengi, haswa ikijulikana ya kwamba, taratibu na utendakazi wa bunge zote ambazo ziko katika Jumuia ya Madola; yaani Commonwealth countries ambazo taratibu zake zote katika ulimwengu huwa sawa. Ukiangalia nchi ambazo zilitawaliwa na Mwingereza kama vile Kenya, Uganda na Tanzania, taratibu za utendaji kazi ni sawa. view
  • 20 Nov 2019 in Senate: Bi. Spika wa Muda, nitaiunga mkono Ripoti hii ikiwa italetwa hapa tuijadili. Itakuwa jukumu la hili Bunge kuangalia jinsi ambavyo inaweza kukubaliana na mapendekezo ya Ripoti kutoka Kampala. view
  • 20 Nov 2019 in Senate: Mkutano huu uliongea juu ya mazingira ya nchi katika Jumuiya za Madola. Tumeona ni ukweli katika hii Ripoti kwamba sintofahamu nyingi sasa zinaelenda. Msimu ambao si wa mvua sasa umekuwa wa mvua. Msimu ambao watu hawafi katika mito mikubwa wakati masika, sasa wanakufa maji. Maji yanaenda kwa fujo muno na kufagia udongo unaofunika nyumba mabondeni. Kumekuwa na majanga mengi sana kulingana na Ripoti hii. Itakuwa heri kama Bunge la Seneti na Bunge la Kitaifa litaunga mkono Ripoti hii. view
  • 20 Nov 2019 in Senate: Tuliona vile mambo yalifanyika katika Mau Forest, hasa kule Kaunti ya Narok. Ilikuwa jambo muhimu sana kuzingatia kwamba mazingira yetu hapa Kenya yasiingiliwe kisha tuwe katika sintofahamu mbalimbali na kusababisha kukosa mvua kwa sababu ya ukataji miti katika Mau Forest. Ninampa kongole Seneta wa Kaunti ya Narok, Sen. Olekina, kwa sababu yeye alisimama kidete na Wakenya wakati mambo haya yalikuwa yakiendelea. Alisema kwaamba ikiwa unataka maji mazuri, mazingira bora, mvua na chakula, ni sharti tupande miti ndani ya Mlima wa Mau. Bi. Spika wa Muda, katika juhudi zake, ilimbidi Waziri wa Mazingira, Hon. Tobiko, aingilie kati na kupanda miti takribani ... view
  • 20 Nov 2019 in Senate: Mwisho, kuna utendakazi na heshima ndani ya Bunge. Kuna wasichana kwa wavulana wanaoajiriwa ndani ya Bunge zetu za Jumuiya ya Madola. Wakati mwingine utapata kuna kukoseana heshima aidha kati ya wafanyikazi na Wabunge. Mambo haya yalijadiliwa katika mkutano wa Kampala. Sisi Wakenya, hasa Bunge la Seneti, tulifanya jambo muhimu sana kumtuma Sen. Faki, Seneta wa Kaunti ya Mombasa. Alienda kutuwakilisha katika mkutano huo muhimu ambao utaangalia na kuleta Ripoti ambayo itatekelezwa na Serikali yetu. Bi. Spika wa Muda, nilipokuwa Hakimu katika Mahakama Kuu, tuliangalia mambo ya wafanyikazi. Wafanyakazi wa Bunge na Waheshimiwa ambao wanafanya kazi pamoja, ni lazima wawe na ... view
  • 20 Nov 2019 in Senate: Bi. Spika wa Muda, naunga mkono kwa dhati Ripoti hii ambayo imeletwa na Sen. Faki, 001, wa Kaunti ya Mombasa. Ripoti hii ni ya kufana sana na ni nzuri. Ninaiunga mkono ili Bunge letu liweze kutekeleza wajibu kulingana na Ripoti ambayo imewekwa kinaga ubaga mbele ya Bunge hili. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus