Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1501 to 1510 of 2266.

  • 10 Feb 2020 in Senate: Shukrani. view
  • 29 Jan 2020 in Senate: Asante sana, Bw. Spika. Pia mimi naunga mkono Hoja hii. Wahenga walisema mwerevu hajinyoi. Hii inaamanisha--- view
  • 29 Jan 2020 in Senate: Bw. Spika, jambo la kwanza ni kuwa mawakili wa Gavana Waititu waliofika hapa hawakuweza kuweka wazi stakabadhi zao za utetezi wake kulingana na mashtaka ya Serikali ya Mashinani ya Kiambu. Bw. Spika, walipoulizwa ni kwa sababu gani hawakufanya hivyo, wakasema wao walikuwa tayari kumtetea Gavana mbele ya Seneti. Walimwambia Gavana kuwa watakuja hapa na kutwaambia kupitia Preliminary Objection (PO) kuwa Seneti haina haki ya kusikiliza mashtaka au kesi ambayo imewakilishwa na Bunge la Kaunti ya Kiambu. Hapo ninaona ya kwamba walijaribu kujinyoa wenyewe na badala ya kumtumikia Gavana wao walikuwa wanatumikia nafsi zao. Kawaida ya sheria ni kuwa mtu akileta ... view
  • 29 Jan 2020 in Senate: Mimi nasisitiza ya kwamba Hoja hii ni muhimu na ni lazima iwe funzo kama vile Seneta Dullo alivyosema kwa wengi. view
  • 4 Dec 2019 in Senate: Asante, Bw. Spika. Kwanza ninakushukuru sana kwa sababu ya makaribisho yako mema kwa ndugu zangu kutoka Kilifi, ambao wanaongozwa na Mhe. Kadenge, akiwemo Kamlesh na wale ndugu zangu wote walioko kule juu. Nakuunga mkono na kukushukuru sana kwa makaribisho haya. view
  • 4 Dec 2019 in Senate: Jambo la pili ni kwamba, niko na imani kwamba yale ambayo wamekuja kujifundisha hapa ndani ya Seneti – kujua kanuni na jinsi gani kazi inavyoendelea ndani ya Seneti – wakirudi nyumbani, watakuwa wamejifundisha. Wakiwa wamejifundisha na kuelewa, basi wakirudi kwao, pia wataweza kutekeleza wajibu wao ambao walichaguliwa na watu mashinani ili waweze kuwasaidia ndani ya County Assembly . Vile vile, natumai kwamba wale wafanyikazi wataweza kupata nafasi kwenda katika ofisi mbalimbali ndani ya Seneti, na kuweza kujifundisha. view
  • 4 Dec 2019 in Senate: Bw. Spika, kitu muhimu ambacho nawaeleza ndugu zangu, wakiwa hapa ni kwamba, ile Ripoti ya Building Bridges Initiative (BBI) ikija kwao, inatakikana kila mtu apate nafasi aipitie, aisome na aielewe. Ikiwa kuna vipengele fulani ambavyo mngependelea pengine virekebishwe ama muweze kuweka kanuni zenu pale ndani, ili kanuni zenu ziweze kusiskika, tuko na “baba” yetu hapa, Mhe. Haji, ambaye ni Seneta na Mwenyekiti wa hiyo Tume ya BBI. Bw. Spika, nakushukuru sana kwa makaribisho hayo. Natumai kwamba watu wa Kilifi wamefurahi sana. Kumalizia, tutakapochukua Seneti Mashinani mwaka ujao, watu wa Kilifi wameniambia ya kwamba nikuombe kwamba Seneti Mashinani mwaka ujao iwe ... view
  • 4 Dec 2019 in Senate: Asante Bw. Spika. Pia mimi ninataka kumshukuru ndugu yetu Sen. Cherargei kwa kurudi na kuamka leo vizuri akitoka nyumbani kwake. view
  • 4 Dec 2019 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 4 Dec 2019 in Senate: Jana alikuwa mahabusu. Karibu sana ndugu yangu. Vile vile, nilikuwa nataka kusema ya kwamba, katika hilo swala ambalo limeulizwa kuongezwe; ni lini ile barabara ya kutoka Mombasa hadi Malindi itamalizika. Kwanza ile sio barabara. Ni barabara ambayo inasafirisha watalii wengi, lakini utaona kwamba, ile barabara imeachwa ni kama pwani sio Kenya. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus