Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1491 to 1500 of 2266.

  • 19 Feb 2020 in Senate: Kwa hivyo Bw. Naibu Spika, naomba utoe onyo kali kwa wale Waheshimiwa wa Jubilee, ya kwamba ni lazima waheshimu Bunge la Seneti na pia wafanye heshima kwa Wakenya waliowapigia kura kutoka sehemu wanazotoka. Na pia, view
  • 19 Feb 2020 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 19 Feb 2020 in Senate: kama kuna runinga, iangalie upande ule, na ione kwamba ni Seneta mmoja tu pekee aliye upande huo mwingine. view
  • 19 Feb 2020 in Senate: Mine is very clear. Bw. Naibu Spika, asante sana kwa kunipa muda huu. Pia ningependa kumpa hongera ndugu yangu kwa kutambua kuwa mimi ni mkubwa wake kiumri, na nilimtangulia kuingia katika Bunge la Seneti. Nampatia heshima kubwa sana Sen. Olekina. Ni watu wachache sana ambao wako na heshima kama hiyo. Ukiniona nikimshukuru ni kwa sababu Sen. Olekina anastahili kongole kubwa. view
  • 19 Feb 2020 in Senate: Bw. Naibu Spika, ningependa kumuunga mkono ndugu yangu, Sen. M. Kajwang’, ambaye pia ni mdogo wangu. Hii ni kwa sababu ameleta Mswada huu ambao ni wa maana sana, unaohusu mambo ya uchukuzi, ufugaji na biashara ya samaki. Nimetafakari mageuzi haya na nikaona kuwa yako katika mstari wa mbele. Kitu muhimu cha kunakili, ni kwamba hakuna chochote kinachotengenezwa cha samaki kisichohusu mvuvi. Mimi natoka katika eneo la Pwani. Ufuo wote wa Pwani ni ufuo wa bahari. Wengine wetu tulisomeshwa na wazee wetu kutokana na mapato ya uvuvi wa samaki. Vile vile, tuko na maziwa kama matatu hivi yanayojulikana Kenya. Ziwa kubwa ... view
  • 19 Feb 2020 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 19 Feb 2020 in Senate: Bw. Naibu Spika, uvuvi unaweza kuendesha uchumi wa nchi yetu mbele. Katika Mswada huu, kuna vitu vingi ambavyo Sen. Kajwang’ amevizingatia. Ninawakilisha eneo la wavuvi, na ninajua kwamba uchumi wa wavuvi ni nadra. Ina maana kwamba Serikali lazima isaidie wavuvi waliochini. Kuna wavuvi wanaotumia mitumbwi, madau makubwa au meli. Cha muhimu ni kwamba wavuvi hawapati msaada wowote kutoka kwa Serikali. Serikali yetu lazima izangatie swala la kuwainua wavuvi walio chini, ili nao wapate maendeleo. view
  • 19 Feb 2020 in Senate: Kwa kumalizia, ningependa kusema kwamba uchukuzi wa samaki una manufaa kabisa. Samaki iko na faida nyingi, hususan kwa watu kama sisi tuiliopita umri wa zaidi ya miaka 40 au 50. Mimi sio daktari, lakini nikikuangalia, najua kwamba ukila nyama kwa wingi katika umri wako, utakuwa na shida inayonipata mimi nikila nyama kwa sababu ya gout . view
  • 19 Feb 2020 in Senate: Bw. Naibu Spika, mimi na wewe ni mawakili. Wewe ni professa wa sharia, lakini madaktari wanatuhimiza kula samaki kwa wingi katika umri wetu, ili kuendeleza maisha yetu. Inafaa tuwachane na nyama ili tuwache kuteseka kiafya. Bw. Naibu Spika, naunga mkono Mswada huu ulioletwa na Seneta wa Homa Bay County, Sen. M. Kajwang’; pamoja na vitengo vyote alivyotenga kwa mambo ya uchukuzi na maendeleo ya samaki katika Kenya. Asante Sana, Bw. Naibu Spika. view
  • 10 Feb 2020 in Senate: Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii. Kwanza ninatoa rambirambi zangu kwa familia ya hayati Mzee Moi na marafiki wao, hususan ndugu yetu Sen. Gideon Moi kwa kumpoteza Mzee . Hili ni jambo la Mwenyezi Mungu na sisi binadamu tunasema analopitisha Mungu hatuwezi kulipinga. Nakumbuka mara ya kwanza kukutana na hayati ilikua mwaka wa 2000 wakati nilikuwa nime chaguliwa kama mwenyekiti wa chama cha wakulima nchini; AgriculturalSociety of Kenya (ASK). Hata wewe Bw. Sipka ulikuwa mmoja wa wanachama wake. Nilikuwa na wasiwasi na tashwishi ya jinsi vile ningeongea mbele ya Rais, maanake ilikua mara yangu ya kwanza kukutana naye. Aliniambia: ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus