Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1481 to 1490 of 2266.

  • 19 Feb 2020 in Senate: Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii ili niweze kujiunga na wewe kuwakaribisha waheshimiwa waliofika hapa kutoka Bunge letu la mashinani la Kisii. Ninaimani kwamba muda ambao wametumia hapa kujifundisha na kujionea, watarudi nyumbani ili wakaweze kuendeleza Kisii County kwa yale mafunzo waliyoyapata hapa. Hapa Seneti tunajivunia jabali mkongwe wa kisiasa aliyekomaa kisawasawa ambaye sisi tunamsifu sana, Sen. (Prof.) Ongeri, kwa uhudumu wake wa kuhudumia watu wa Kisii katika Seneti. Kitu ambacho nataka kuambia Waheshimiwa ni kwamba Katika zile kura sita mlizopiga, kama kuna moja muhimu mliyofanya, nyinyi kama wabunge wa Kisii, ni kura ya kumpigia Sen. (Prof.) Ongeri. ... view
  • 19 Feb 2020 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 19 Feb 2020 in Senate: Asante, Bw. Spika. Pia mimi ninaunga mkono Taarifa hii. Ninafikiria imekuja kwa wakati muafaka. Virusi vya Corona ni virusi ambavyo vimekua kama donda ndugu katika maisha ya Wakenya. Hii ni kwa sababu huwezi kujua tofauti kati ya wanaougua na wasiougua hivi virusi. Hivi sasa, kuna watu wamewekwa mahali ili kuchunguza kama wana huo ugonjwa. Kuna tashwishi kwa sababu ni kama siri inafanyika. Mpaka sasa, Kenya haijachukua msimamo kabisa kuwa wale waliochunguzwa wameingia wengi na wametoka wengi. Hakuna hata mmoja amesema amepatikana na Virusi vya Corona. Kwa hivyo, inaonekana kuwa kuna sababu fulani ya sisi kutoambiwa ukweli kuhusu janga hili. Rais ... view
  • 19 Feb 2020 in Senate: , ambayo imekua mess kubwa zaidi katika hayo maneno. Kwa hivyo, ikiwa Kenya haiko tayari kuangalia Virusi Vya Corona na kuangalia maneno yanayokuja, sababu zingine ni kama hizi. Mawaziri wengine wanazembea kwa kazi zao. Bw. Spika, mimi ninajua kuwa umesafiri sana na umefika sehemu mbali mbali za Kenya. Utaona kwamba ukiwa huko Mandera - na ninajua kuwa ndugu zetu wanatoka sehemu hizo - ni lango la kuingia na kutoka haswa kwa watu wanaotembea. Utashangaa kuwa lango liko wazi. Ukitoka Kenya kuenda Somalia ama kutoka Somalia kuja Kenya, unaweza kupita bila mtu yeyote kukuuliza unaenda wapi. Kwa hivyo, si mambo ya ... view
  • 19 Feb 2020 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 19 Feb 2020 in Senate: Unajua kuwa hakuna mwanya katika sheria za huko Uchina. Ukipatikana na hatia, wanakuweka korokoroni; hakuna mambo ya wakili ama jambo lolote. Hatujui kama wale Wakenya wamefungwa maisha ama watatolewa siku nyingine. Hatuna uhakika. Hatujui afya yao iko vipi, wala kama chakula kina shida. Bw. Spika, nataka kumaliza--- view
  • 19 Feb 2020 in Senate: Kwa hoja ya nidhamu, Bwana Naibu Spika. Ni jambo la kusikitisha katika Bunge letu la Seneti, ambalo ni hatari kubwa pia kwa heshima ya Wakenya waliowachagua viongozi walio wengi ndani ya Seneti. Ni aibu leo kwa upande wa waliowengi ya kwamba Bunge linaweza kuendelea bila wao. Hakuna Kiongozi, hakuna Naibu wa Kiongozi, hakuna wenyeviti wala Mweshimiwa Seneta yeyote. Hii ni aibu katika uongozi ndani ya Seneti. view
  • 19 Feb 2020 in Senate: Bw. Naibu Spika, katika historia ya Kenya, hili halijatokea. Kwa hivyo, tunataka kusema kwamba jambo hili lazima likome. Pia, inatakikana utuelekeze katika mwelekeo wa kwamba hata ikiwa watatoka wote kwa mipangilio waliyo nayo, ambayo hatuijui sisi--- view
  • 19 Feb 2020 in Senate: Anajua? view
  • 19 Feb 2020 in Senate: Yeye pekee! view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus